Mkutano wa CHADEMA viwanja vya NMC Arusha

CDM inapaswa kuachana na Arusha sasa... Arusha kimeshaeleweka siku nyingi! kwa ninavyoijua arusha ccm hata waende mbinguni hawawezi kuchukua arusha! Nguvu nyingi zipelekwe Tabora, Dodoma na sehemu zingine ambapo inaonekana wananchi bado wamelala.. nadhani kina nanyaro, Ben, zitto na wengineo mnaelewa nasema nini, kuna sehemu zinahitaji uamsho na sio arusha, mbeya au mwanza
 

Shida mnaanzisha thread halafu kuleta updates hamleti mkitegemea wengine wafanye hivyo! Kama huwezi kuleta updates pamoja na picha tafadhali kaa pembeni waachie wenye nia na uwezo wafanye hivyo. Hata thread yenyewe maelezo nusu nusu - hayajitoshelezi. Ungekuwa serious ungetueleza yafuatayo:-

- Muonekano na matayarisho hapo uwanjani kwa ujumla yakoje hadi sasa - bendera za chama, majukwaa, vikundi vya ngoma, dansi, n.k.
- Viongozi gani wanatarajiwa kuwepo kwenye huo mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k.
- Viongozi gani mpaka sasa wameshawasili au wako maeneo ya mkutano - viongozi wa wilaya, mkoa, taifa, madiwani, wabunge, n.k.
- Mwitikio na hamasa ikoje - waliovalia mavazi na nembo zingine za chama, gari ya matangazo, vipeperushi, mabango, n.k.
-Jamaa wa intelijensia vipi? Wameshaanza kuranda randa maeneo ya karibu, migari yao ya kuwasha, n.k.
- Ni mambo gani hasa makubwa yanayotarajiwa kujiri katika mkutano wa leo - wengine tunasikia kuna maelfu ya wana-CCM watakaorudisha kadi; Je, ni kweli? n.k.

Halafu, kwa taarifa yako sio "Mpango" ni "Operesheni".

2po wengi arusha,sio lazima mimi kila kitu.
 
CDM inapaswa kuachana na Arusha sasa... Arusha kimeshaeleweka siku nyingi! kwa ninavyoijua arusha ccm hata waende mbinguni hawawezi kuchukua arusha! Nguvu nyingi zipelekwe Tabora, Dodoma na sehemu zingine ambapo inaonekana wananchi bado wamelala.. nadhani kina nanyaro, Ben, zitto na wengineo mnaelewa nasema nini, kuna sehemu zinahitaji uamsho na sio arusha, mbeya au mwanza

Azimio la Arusha, tunakomba vidagaa vyote.
 
Hukusikia Geita, Mwanza, Mbeya...Subiri mambo yakiiva tutatua hapo Dar mpaka Kikwete anajivua gamba...

Kila siku Arusha tu Makamanda jaribuni kujitanua kitaifa zaidi kuliko kikanda.

Lini tutasikia Chadema wameweka kambi maeneo mengine kama.

Kilwa.
liwale.
Ruangwa.
Nachingwea.
Newala.
Nanyumbu.
Tandahimba.
Ngara.
Karagwe.
Muleba.
Kyerwa.
 
Arusha Mambo itatangaza moja kwa moja [Live] mkutano huo kutoka Arusha, visit www.arushamambo.com kisha click "Sikiliza Arusha Mambo FM......" page ya tunein ikifunguka click LIKE ili kusikiliza,

Source: Arusha Mambo
 
Jamani twendeni lindi,mtwara,tanga,tabora,unguja sii kila siku arusha.arushwa wameshaelewa maana ya m4c!
Strategies za kivita, kama huwezi kuteka nchi nzima kwa mara moja teka sehemu muhimu kabla ya kuelekea kumiliki mapori, usije kuwa na tamaa na kuondoka kabla ya kujiweka sawa utaikosa miji yote.
 
Kila siku Arusha tu Makamanda jaribuni kujitanua kitafa zaidi kuliko kikanda.

Lini tutasikia Chadema wameweka kambi maeneo mengine kama.

Kilwa.
liwale.
Ruangwa.
Nachingwea.
Newala.
Nanyumbu.
Tandahimba.
Ngara.
Karagwe.
Muleba.
Kyerwa.

Mkuu ritz,
Ni lini tutasikia na CCM imepiga kambi Arusha, Mbeya, Mwanza na maeneo hayo uliyoyataja?

 
Last edited by a moderator:
Pamoja sana MAKAMANDA kwa A-town sina shaka kabisaa najua ntapata updates za kila kitu mwanzo mwisho.
 
Operation vua gamba vaa gwanda nadhani ndiyo itayoitokomeza CCMkanda ya kaskazini.
 
nasikia James Millya ameachana na uamuzi wake wa kuhamia CDM na amekiomba radhi chama chake cha CCM. na hii ni baada ya Nanyaro kumwambia atakaa benchi kwa muda usiopungua miaka 5 bila hata cheo cha m/kiti wa kata CDM.

Mwendo mdundo mpaka Ritz avue gamba. Na uhakika atavua tu. Kiguu ndio mwepesi sana huyu, anahitaji kuelimishwa kidogo tu.
 
Pamoja sana Makamanda lakini mbona kila siku Arusha tu Tanzania kubwa.

Nimependa sana Mchango wako leo.... Coverage ya Arusha ni kubwa.. Ndiyo maana inaoneka M4C ipo kule tu
 
Back
Top Bottom