Mkutano wa CHADEMA Same wazuiliwa na polisi

Kwanza nakosoa:

1. Siku nyingine lazima mfuate masharti maana wenzenu wameshika MPINI na nyie mko kwenye makali. Pelekeni riport mapema na ikibidi hata siku nne kabla ili wakose la kusema. Mtasaidia kupunguza bughudha kama hizi kwa Wanachama.

2. Chadema ni chama MAKINI kama mnavyosema siku zote. Basi muwe makini hadi kwenye lugha jamani. Hilo neno SINTOFAHAM maana yake nini? Huwezi kutumia neno la kawaida ili na sisi Washamba wa SIKONGE tuelewe?

Namalizia kwa kukupa HONGERA nyingi sana kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha zoezi hili. Anzeni na Mungu na mtamaliza na Mungu siku zote. Kila la kheri katika mkutano wenu na muende na makapu mengi tupu ya kuvunua na mavuno Mungu akipenda yatakuwa mazuri sana.
Sintofaham hii ndiyo iliyo nichelewesha kuwajulisha kilichokuwa kinaendelea.
 
Matayo na Kilango kesho lazima wavue gamba wavae gwAnda hakuna kulala mpaka kieleweke!!! Halafu nackia uyo mwenye bar ya padeco ni gamba sugu MkUU naomba apelekewe GWANDA ili ajue saa ya UKOMBOZI ni SASA!
 
PAMOJA SANA MAKAMANDA USISAHAU UPDATES ZA NGUVU PAMOJA NA PICHA A. town tunafuatilia mno M4C

BIG UP
 
Kesho kaz ni moja tu. Kuvuna wanachama
Hongera sana simon james kwa kujituma nafikiri kesho mambo yatakuwa mazuri.

Kama ukiweza kuwafikia viongozi wa chama taifa hasa Mbowe waambie kesho waaulize, CCM walikuwa na maana kusema Kikwete ndiye anayemjua rais ajae, na pia waulize kauli ya kuwa rais hatatoka Kaskazini ilikuwa na baraka na uongozi wa juu? mbona hatukusikia uongozi wa juu ukikemea. Ngoja nimtafute Heche kwenye wall yake.
 
ukisema uongo leo basi kesho itakugharimu kuusema ukweli.
Hilo linalozuiwa kusemwa na CDM leo litasemwa kesho,
jeshi la polisi linajaribu kukinga mkuki kwa kutumia kipande cha shuka.
 
Sasa sisi cdm tufahamu kabisa kuna hayo mambo! Tena raia wakifahamu polisi wamezuia mkutano, wanakasirika; halafu hasira za wananchi ni mtaji kwa cdm.
 
All the best makamanda hyo kesho,lakn kwa haya wayafanyayo police siku moja watakuja jilaumu sana lakn itakua too late.
 
Poleni makamanda, walichokifanya hao magamba ni kama "usiku wa deni", yani kesho au kesho kutwa au mwisho wa mwezi, utafika tu... wanachokifanya ni kusogeza mbele kudhalilika kwao...
 
na Inteligensia ya usalama wa taifa ni kufacilitate wizi wa kura...huku wanayama wakubwa kama twiga,tembo na wengineo wengi wakikamatwa porini na kupakiwa kwenye ndege.....,
lakini mikutano na maandamano ndo wanaona tuu......!
 
polisi ingekua iko huru na fair kwa kila mtu ungekuta leo hii viongozi wengi wa ccm walishakamatwa na kufunguliwa mashtaka bt again we r in bongo... hapa mambo ni kibongo bongo
 
Wapendwa ule Mkutano uliotangazwa kufanywa na mwenyekiti wa BAVICHA Taifa pale Stand ya Mabasi Same leo 10/05/2012 ulizuiliwa na jeshi la polisi kwa madai kwamba taarifa haikufika kabla ya masaa 48. Hivyo utafanyika siku ya Ijumaa tar 11/05/2012 palepale standa ya mabasi Same. Wakati tukiwa tunashangazwa na kizuizi hicho. Niwakumbushe Siku J.k alipo tangaza baraza lake jipya la mawaziri, na siku iliyofuata vijana wa CCM Vyuo Vikuu Dar Es Salam wakafanya maandamano ya kumpongeza na kutaka wahusika wa ufisadi uliofichuliwa na CAG Wapelekwe mahakamani. Hivi taarifa ilifika Polisi masaa mangapi? mbona hawakuzuia yale maandamano? Tunajua utaratibu lakini hakuna usawa
. simon james tupe updates za mkutano.
 
Last edited by a moderator:
Mgangamale Makamanda kuuchimba mbuyu kwa mikono kunahitaji kazi ila kama lengo ni kuungoa hata mwenzi mzima utangoka tu cha muhimu hapo ni juhudi na ujasiri
 
RPC/RCO/OCD nk wangeulizwa na Ridhiwani ni kwa nini wameruhusu mkutano wa kuibomoa CCM yao ufanyike.

So, kwa shingo upande unaelewa bila kukubali, kuwa hawa wachumia tumbo (polisi) nao wanahitaji vijikaratasi kumwonyesha bosi wao Riz! Angalau utaratibu uonekane ulifuatwa na hawakuwa na njia nyingine ya kuwazuia CDM labda kama IGP angeruhusu silaha za moto zitumike.

Hayo ndio malipo ya woga, unafiki, incompetence na ujinga ambao tunalipa gharama zake kila siku
 
Leteni updates,zikiandamana na picha tafadhali na katibu wa cdm wilaya ya same c yumo humu,,juzi kati hapa aliitisha harambeeee ya michango
 
Back
Top Bottom