Mkutano wa CHADEMA Same wazuiliwa na polisi

simon james

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
283
140
Wapendwa ule Mkutano uliotangazwa kufanywa na mwenyekiti wa BAVICHA Taifa pale Stand ya Mabasi Same leo 10/05/2012 ulizuiliwa na jeshi la polisi kwa madai kwamba taarifa haikufika kabla ya masaa 48. Hivyo utafanyika siku ya Ijumaa tar 11/05/2012 palepale standa ya mabasi Same. Wakati tukiwa tunashangazwa na kizuizi hicho. Niwakumbushe Siku J.k alipo tangaza baraza lake jipya la mawaziri, na siku iliyofuata vijana wa CCM Vyuo Vikuu Dar Es Salam wakafanya maandamano ya kumpongeza na kutaka wahusika wa ufisadi uliofichuliwa na CAG Wapelekwe mahakamani. Hivi taarifa ilifika Polisi masaa mangapi? mbona hawakuzuia yale maandamano? Tunajua utaratibu lakini hakuna usawa
 
Poleni makamanda kesho sio mbali piteni PADECO,KIMWERI na KINDOROKO tangazeni sera ya ukombozi na uhuru wa KWELI.
 
pale Stand ya Mabasi Same leo 10/05/2012 ulizuiliwa na jeshi la polisi kwa madai kwamba taarifa haikufika kabla ya masaa 48. Hivyo utafanyika siku ya Ijumaa tar 11/05/2012

mi nilijuwa wamepiga marufuku.

hehehe, lazima wafuate masharti ya wanakoenda kutembeza bakuli. "ruhusu watu wafanye democrasia (hata kama hamprndi), vinginevyo tunawanyima misaada".

Pipoooooooooooooooooooooooooooz!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Haijalishi ni muda Gani Wataendelea kuwazuia makamanda wasielimishe jamii na kuwafungulia kesi zisizo kuwa na ushahidi kamwe hawatoweza kuzuia mabadiliko .watanzania wa leo sio wa jana na wala sio wa kesho .mapolisi na serikali kwa ujumla wanapashwa kusoma alama za nyakati .
 
Double standard, likini hata shetani hutumika kufanikisha mambo. Ijumaa imekaa viziri zaidi. M4C weekend.
 
Walivyozuia wameongeza kiu ya wananchi kusikia hotuba za ukombozi, itakuwa shangwe, muda waja!!!!!!
 
Msitie hofu, hiyo ni publicity tosha. Hapo Same sasa hivi kila mtu atakuwa anauzungumzia. Hata wale ambao wasingeweza kufikiwa na habari sasa zitawafikia.
 
Naona polisi sasa wameingiza miguu yote kwenye siasa. Itakuwa vizuri wakiingia ofisini kwa Tendwa kuomba usajili kama ccmC kuwasaidia CUF ili kulinda ccm na mafisadi
 
ipo siku polisi hawahawa watawagekia wao naombeni ujumbe huu uhifadhiwe
 
Back
Top Bottom