Mkutano wa CHADEMA ndani ya Mbeya Leo

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
[h=6]Habari za jioni wadau!

Hivi sasa ndio natoka katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Ukumbi wa Mtenda Sunset 1 uliopo Jijini Mbeya,Maeneo ya Soweto.

Mkutano huo umefanyika katika harakati za CHADEMA katika kuwaelimisha wananchi kuhusu mchakato wa kuipata Katiba unavyoendesha na serikali,na jinsi CHADEMA inavyoshiriki katika mchakato huo.Mikutano kama hiyo imefanyika nchi nzima katika makao makuu ya mikoa.

Mikutano hiyo inafanyika katika kumbi badala ya kwenye viwanja vya wazi kwa sababu Polisi imesitisha mikutano yote ya hadhara.Kwa hiyo CHADEMA katika kukabiliana na hilo,imeamua kutumia mbinu hiyo.Watu walikuwa wengi sana,na kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha.Watu waliohudhuria na kujiandikisha kwenye karatasi ya mahudhurio ni watu 1020,achilia mbali watu ambao mara nyingi hawapendi kujulikana pamoja na ndugu zangu wa Usalama wa Taifa aka Usalama wa viongozi.

Katika mkutano huo,mgeni rasmi alikuwa Mhe.Joseph Mbilinyi aka Sugu,Mbunge wa Mbeya Mjini (wanamwita Rais wa Mbeya),wakati watoa mada wakuu walikuwa ni Katibu wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Taifa,Mama Kihaula (ambaye ni mama mzazi wa GK,Msanii wa muziki wa hiphop pande za East Coast),na Basili Lema.

Mada kuu katika mkutano huo,ilikuwa ni mchakato wa katiba,kwanini wabunge wa CHADEMA walisusia majadala wa muswada huo,makubaliano yao na rais,na hatua wanazochukua kukabiliana na kile wanachokiita "uhuni wa CCM".

Mengi yanajulikana na watanzania wengi,labda nizungumzie hatua ambazo chama kinachukua ili kuhakikisha wananchi wanajua kilichopo katika sheria ya uanzishwaji wa tume ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi.Kwanza chama kimeamua kuweka mikutano ya hadhara kutoka ngazi ya Mkoa hadi vijiji.Tarehe 14/12/2011,mikutano kama hiyo itaendesha kwa kila wilaya,tarehe 21/12/2011,kila kata na tarehe 28/12/2011,kwa kila kijiji.Baada ya hapo,Chadema Taifa litawaelekeza nini cha kufanya wananchi hasa pale kama maoni yao hayatasikilizwa.Kikubwa zaidi,ni kwamba kama hakutakuwa na mabadiliko ya sheria hiyo katika kikao cha Bunge cha mwezi Januari/Februari,basi CHADEMA itasusia mchakato wa Katiba na People's Power itachukua mkondo wake.

Zaidi ni maoni/ushauri na maswali ya wananchi waliohudhuria mkutano huo ndiyo yaliyonigusa sana.Wananchi waliopata nafasi ya kuzungumza wameongea kwa hisia kali sana.Pamoja na maneno ya hamasa na kutia moyo katika safari ya kulikomboa taifa letu,waliuliza maswali,hasa kwanini VIONGOZI WA CHADEMA waliamua kukutana na rais Ikulu ilihali wanajua ni ndumila kuwili,nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa katiba,ongezeko la posho kwa wabunge (suala hili lilivuta hisia za watu wengi) na kwamba kama WABUNGE WA CHADEMA wameshiriki katika kujiongezea posh hiyo,basi sio wenzao tena.

Wakijibu kwa pamoja,watoa mada wamekanusha kuhusu taarifa zilizotolewa na Spika jana kwamba posho ya wabunge imeongezwa.Wanasema hiyo imekuwa njama ya CCM kuwahamisha wananchi kwenye suala la katiba ili sasa wajadili kuhusu posho hizo hasa ikizingatiwa kuwa msimamo wa CHADEMA kuhusu posho hizo ni kwamba zifutwe.Wanasema hakuna mbunge hata mmoja wa chadema aliyepokea posho hiyo,na kwamba hata Rais hajaidhinisha malipo ya posho hiyo.

Wanasema,hawalalai hadi kieleweke,kikieleweka CCM chali.Ni harakati za mtu kwa mtu,mlango kwa mlango,nyumba kwa nyumba,kaya kwa kaya,kijiji kwa kijiji,wilaya kwa wilaya,mkoa kwa mkoa,hadi Taifa.
[/h]
 
lakini mkuu mkutano kufanyika ndani ya ule ukumbi utakuwa na walengwa?kwa nini wasingefanya mkutano wa hadhara kwa wote?
 
lakini mkuu mkutano kufanyika ndani ya ule ukumbi utakuwa na walengwa?kwa nini wasingefanya mkutano wa hadhara kwa wote?
Ameeleza kuwa polisi wamepiga marufuku mikutano ya hadhara. Haraka ya nini?
 
lakini mkuu mkutano kufanyika ndani ya ule ukumbi utakuwa na walengwa?kwa nini wasingefanya mkutano wa hadhara kwa wote?
Amejibu soma para ya 3.
Wanasema,hawalalai hadi kieleweke,kikieleweka CCM chali.Ni harakati za mtu kwa mtu,mlango kwa mlango,nyumba kwa nyumba,kaya kwa kaya,kijiji kwa kijiji,wilaya kwa wilaya,mkoa kwa mkoa,hadi Taifa.
Nafikiri ungemalizia hadi taifa kwa taifa.
 
Hata kama watawachanganya watu kwa kutumia mbinu za kiintelenjesia lakini watanzania wa leo si wa jana kabisa. Wacha waanzishe mambo ya posho na upuuzi mwingine lakini hautaepusha jokoo kuchinjwa siku ya sikuuu.
 
Good summary am praying for Chadema kuwaka zaidi na nuru iwasaidie wote walioko gizani .
 
Hata kama watawachanganya watu kwa kutumia mbinu za kiintelenjesia lakini watanzania wa leo si wa jana kabisa. Wacha waanzishe mambo ya posho na upuuzi mwingine lakini hautaepusha jokoo kuchinjwa siku ya sikuuu.

Ni kweli mkuu,muda ukifika hakuna mtu anaweza kuzuia mabadiliko.Aluta continua.
 
Tarehe 14/12/2011,mikutano kama hiyo itaendesha kwa kila wilaya,tarehe 21/12/2011,kila kata na tarehe 28/12/2011,kwa kila kijiji.Baada ya hapo,Chadema Taifa litawaelekeza nini cha kufanya wananchi hasa pale kama maoni yao hayatasikilizwa.Kikubwa zaidi,ni kwamba kama hakutakuwa na mabadiliko ya sheria hiyo katika kikao cha Bunge cha mwezi Januari/Februari,basi CHADEMA itasusia mchakato wa Katiba na People's Power itachukua mkondo wake.

hapo ndio patamu.....ki ukweli elimu ya uraia vijijini ni zero...watu hawajui katiba ni nini...watu hawajui siasa ya vyama vingi....watu mpaka sasa wanaamini wakichagua vyama vingine kinachofuata ni vita tu...ki ukweli katika ili tuhakikishe tunatekeleza..."GOD BLESS TANZANIA AND BLESS CHADEMA"

[/QUOTE]
 
nawashauri hawa wenzetu wa pipoz pawa,huko kwenye mikutano zile kadi za uwanachama tusizisahau . !
Hapo tuko pamoja shavu kwa shavu, na jino kwa jino until further notice . .
 
Asante kwa summary nzuri mkuu. Mimi pia nilikuwepo kwenye kongamano la leo kwa hamasa ya watu waliohudhuria kongamano hili ninaiomba serikali ya ccm, kwa swala la sheria ya mchakato wa katiba mpya iache kuwasha kiberiti kwenye dumu lilo jaa petroli. Kwa ujumla Mbeya wako tayari kwa lolote kuhakikisha katiba sahihi inapatikana.
 
Cha ajabu kwa sababu ya kongamano la CHADEMA kufanyika katika eneo la Soweto, eneo lote la soweto lilikatiwa Ngeleja kuwaadhibu wakazi wote wa soweto mpaka jioni!
 
E bana hii ni kali sana, e mola wabaliki chadema watufikishe uko salama, najua magamba (ccm) hawataamini, walijua maandamano ndo njia yao chadema lakini hii ni nimeipenda pia ni kali kuliko, naomba ratiba kigamboni mtakuja lini kwani lazima nihudhurie, e mola wabariki chadema daima na milele, nape upoooooooo....
 
cha ajabu kwa sababu ya kongamano la chadema kufanyika katika eneo la soweto, eneo lote la soweto lilikatiwa ngeleja kuwaadhibu wakazi wote wa soweto mpaka jioni!
e bana poleni kwa kukatiwa umeme, lakini izo ndo harakati za ukombozi, viva Soweto, viva chadema
 
Mi nipo naangalia ngoma inavyochezwa, lakini all in all "CCM is directly propotional to CDM".
 
e bana hii ni kali sana, e mola wabaliki chadema watufikishe uko salama, najua magamba (ccm) hawataamini, walijua maandamano ndo njia yao chadema lakini hii ni nimeipenda pia ni kali kuliko, naomba ratiba kigamboni mtakuja lini kwani lazima nihudhurie, e mola wabariki chadema daima na milele, nape upoooooooo....
tunaomba ratiba kanda ya ziwa tunawasubiri kwa hamu sana.
 
Back
Top Bottom