Mkutano wa Chadema M4C-Iringa wasitishwa!

ukweli nikwamba polisi wanashindikizwa na chama cha mapinduzi wakiofia chadema kupata wanachama wapya kwakufanyamikutano but watambue kua watanzania sio mabwege na tumeshaianza safari no turning back wajifuunze kuua tunajifunza kufa
 
Asubuhi hii nimepita maeneo ya mjini iringa, nikafika sehemu kupata supu, akaingia jamaa mmoja akakaa meza moja na mimi, mara simu yake ikanza kuita, akawa anaongea kwa hasira na uchungu. Mwishowe akawa anamtia moyo huyo mpigaji kuwa msikate tamaa, hawa jamaa wahuni wanaweza kuzua kisingizio hata wakamtumia daktari kudanganya watu kuwa kuna magonjwa ya mlipuko, ili mradi chadema wasifanikiwe kufanya mkutano.

Alipomaliza kuongea nikaanza kuongea naye, akaniambia kuwa mkutano wa chadema unazuiliwa tena, ila sababu ya msingi haionekani. Nilipotoka pale nikapita maeneo ya m.r. Hotel, nikakuta magari ya m4c yamajazana pale na wanatimu kibao wakiwepo kashidye wa igunga. Lakini sikuona shamra shamra zozote, inaonekana kama wanajaadiliana jambo.

Samahani kwa kutokuweka picha ila kama nilivyosema, ni tetesi tuu, naendelea kufuatilia.
 
Dk, zile siku tatu ulizokaa kimya wakati watu wakisubiri kauli yako, utamke neno baada ya matokeo ya uchaguzi kuchakachuliwa, madhara yake ndiyo haya.

Kumbuka, hekima yako ni tunu kwetu, lakini si wote wanaujua ustaarabu.

Tamka neno sasa, ukichelea tena, hutaeleweka.

Tanzania, mashujaa wetu wajifunze kusimama.Isiwe kama yule daktari aliyepotea!
 
Kuna watu wanafikiri hii ni nchi yao peke yao, uoga wa M4C umewafanya washindwe kifikiri kabisa. M4C haitasimama mpaka kieleweke. Cha moto mtakiona.

Habari ndio hii hapa chini. Na inakuja Iringa

483695089.jpg

HAHAHAHAH ccm kazi mnayoo na huu ni mwanzo,, mnakimbiza jet kwa miguuu
 
Wangekuwa wanatumia nguvu hizi wanazo pambana na chadema kudhibiti wizi na uporaji wa raslimali zetu basi nchi yetu ingekuwa mbali sana!

Wanachokifanya kwa sasa ni kuiongezea chadema speed ili izidi kupaa kwenye mioyo ya wananchi.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
 
UMEPANGWA KUFANYIKA TRH 9.9.2012 Jipangeni vyema!

Hiyo tarehe wasije wakasema tena kuwa ni tarehe maalumu maana itakuwa siku ya tisa tisa ambayo ni siku ya kuazimisha birthday ya kamanda wa polisi mkoa wa Iringa.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
 
Back
Top Bottom