Mkutano wa Chadema M4C-Iringa wasitishwa!

Sometimes naona kama serikali inaelewa inachokifaya kwa maana inataka CCM iondoke madarakani kiulaini!!!!!!!!!!!!!! Hivi vitendo vyake na serikali yake vya makusudi kuchukiza wananchi kiasi hiki vinazidi kuijenga upinzani hususani CHADEMA. Kama CCM na serikali wanadumisha demokrasia ya kweli mbona yote watendayo ni kinyume chake? CCM wajipange upya kwa kushirikiana na wadau wote kujenga taifa linalopiga hatua kijamii, kiuchumi na kisiasa tofauti na ilivyo sasa. Ni ujinga kung'ang'ania kutawala huku hukubaliki.
 
Saizi nasikia wimbo wa CHADEMA ukiimbwa na gari la matangazo hapa gangilonga jiran na ofisin kwangu. wanachama wanatangaziwa kua viongozi waingie ndani ya gari na wengine watawanyike
 
Jamani CCM tumeichagua sisi watanzania,nyie vimburu wachache mnakuja kusema itolewe madarakani. Sasa hiyo demokrasia iko wapi? Nyie siasa zenu za visasi na chuki ndio maana kila jambo mnalichukulia kifujo fujo.
Tanzania tunayo demokrasia ya kweli lasivyo hii JF isingekuwepo na hao kina mbowe,Slaa,lema,zitto wote wangekua wananyea debe sasa hivi. Lakini yote haya yatakwisha 2015 atakapo ingia EL ikulu. Ni miaka michache tu mbele,hata hao viongozi wenu wanalijua hilo. Kiboko yao yuko njiani.
 
CCM ni watu wakufuata sheria na wanajua sheria, ila wenzetu ni watu wakutumia nguvu na kuacha sheria, ndio maana wao hawauliwi kwani hawafanyi fujo. Hakuna maandamano bila kibali, sasa kibali mlikuwa nacho? na mliambiwa msiandamane ila mkalazimisha, huko sio kumwaga damu kwa dhamira za uchu wa madaraka?

Magamba Kazini! Hakuna marefu yasiyo na ncha na hakuna dola itakayodumu milele. Nani nyakati hizo angefikiri dola ya rumi ingesambaratika bila kuwepo hata masalia? Lakini anguko lenu magamba litakuwa na mshindo mkuu ambao kamwe haujawahi kutokea nchini, na lipo karibu kwa kuwa kuna kila dalili. Hamtaki kuvuliwa nguo kwa maovu mnayoyafanya, watu wanapopaza sauti zao dunia iujue unafiki wenu mnawaziba midomo kwa kutumia jeshi ambalo halina tofauti na la kikoloni. Maradhi mnayojaribu kuyaficha kifo kitawaumbua. Hakuna safari isiyokuwa na mwisho, na kweli siku zote itashinda!
 
Pole kwakufungwa akili na magamba pia pole kwakuwa gamba pia pole kwakuwa kwenye giza pia pole kwakuwa mfungwa kifikra ccm mwisho wake umefika believe or not
 
Intelejensia ya polisi wetu ni dhaifu sana, yani uwa inafanya kazi kwa mikutano ya CHADEMA tu.
 
chezea dola wewe

Unainua kichwa wanakigonga

Hii m4c naona imewabinya pabaya!maana kuna influx ya member wapya ambao ni wazi kama wamekurupushwa waje humu,maana utajuwa kabisa ni wapya kwa jinsi wanavyochangia.Member mgeni kama ana id nyingine utajuwa tu.

Halafu kuna wengine kama wewe,selemani,geniusbrain et al ambao huwa mukitokea humu nyakati za uchaguzi ama kashfa kubwa kubwa,sasa nashangazwa kuwaona mko mmerudi with a full force!najiuliza maswali sipati majibu.

My guts tells me it must be this m4c stuff.
 
Hii m4c naona imewabinya pabaya!maana kuna influx ya member wapya ambao ni wazi kama wamekurupushwa waje humu,maana utajuwa kabisa ni wapya kwa jinsi wanavyochangia.Member mgeni kama ana id nyingine utajuwa tu.

Halafu kuna wengine kama wewe,selemani,geniusbrain et al ambao huwa mukitokea humu nyakati za uchaguzi ama kashfa kubwa kubwa,sasa nashangazwa kuwaona mko mmerudi with a full force!najiuliza maswali sipati majibu.

My guts tells me it must be this m4c stuff.

mkuu, ukiwajibu hawa unakuwa unajishushia heshima yako. Sawa na kumjibu Nape. Afadhali uongee na bar maid kuliko kumjibu any of these 'things'
 
Jamani CCM tumeichagua sisi watanzania,nyie vimburu wachache mnakuja kusema itolewe madarakani. Sasa hiyo demokrasia iko wapi? Nyie siasa zenu za visasi na chuki ndio maana kila jambo mnalichukulia kifujo fujo.
Tanzania tunayo demokrasia ya kweli lasivyo hii JF isingekuwepo na hao kina mbowe,Slaa,lema,zitto wote wangekua wananyea debe sasa hivi. Lakini yote haya yatakwisha 2015 atakapo ingia EL ikulu. Ni miaka michache tu mbele,hata hao viongozi wenu wanalijua hilo. Kiboko yao yuko njiani.

EL? Leo posho hupati wewe, unataja EL wakati ajira amekupa Nepi?
 
Wewe ni crazyBrain!

Unataka kutuambia uhuru wa mipaka ni kuzuia maandamano ya CHADEMA lakini maandamano ya CCM ruksa!

Hivi for your tiny and small Brain, unafikiri Watanzania wote ni wapuuzi na wajinga kama wewe? Sahau! Watanzania wanajua wanachokifanya na kwa taarifa yako tu jinsi Policcm wanavyoendelea kuua na kujaribu kuzuia maandamano ya wapinzani hususan CHADEMA ujue tu CCM wanaendelea KUSAFISHA NJIA YA CHADEMA KUINGIA IKULU 2015!

Wewe subiri 2015 utaelewa ninachomaanisha.

Don't worry GeniusBrain is NO BRAIN at all. He is a lost cause. He thinks,breathes,smells,inhales,talks and walks stupidity! He is a child of total darkness and when the light is attempted on him he/she retreats into partisan cocoon, choosing to embrace headless chicken driven propaganda
 
Polisi wazuia mikutano ya Chadema Iringa
Tuesday, 28 August 2012 23:00

Waandishi Wetu
Mwananchi

VUTA nikuvute baina ya Polisi na Chadema imehamia Iringa, ambako jeshi hilo limezuia maandamano na mikutano yote ya chama hicho iliyokuwa imepangwa kufanyika kwa siku nane kuanzia jana.
Amri hiyo ya polisi imekuja siku moja baada ya kutokea vurugu kubwa mjini Morogoro, baina ya wafuasi wa chama hicho na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema jana kuwa wameamua kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema iliyopangwa kuanza jana kutokana na Sensa ya Watu na Makazi.
“Kutokana na hali halisi ya Sensa, tumeamua kuzuia maandamano na mikutano yote ya vyama vya kisiasa mkoani Iringa wakiwamo hawa watu wa Chadema,” alisema.
Alisema kabla ya kuwazuia, walikutana na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Iringa na kuwataka wazuie mikutano yao, jambo ambalo alisema walilikubali kwa ‘mbinde’.

Dk Slaa: Wametuomba
Awali, akiwa Mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi wamekiomba chama hicho kusitisha maandamano na mikutano yake iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kupisha Sensa ya Watu na Makazi.

Alisema Chadema imekubali ombi hilo lililotolewa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema hivyo kuamua kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa jana.


“Juzi Agosti 27, 1:00 usiku tulipata barua kutoka Jeshi la Polisi Iringa iliyokubali Chadema kufanya maandamano wakiwa ndani ya magari na si matembezi ya miguu, lakini baadaye saa 3:00 usiku, tulipigiwa simu na OCD wa Iringa akitujulisha kuwa maandamano yao yamebatilishwa na kutengua mambo yote tuliyoafikiana mwanzo,” alisema Dk Slaa na kuongeza:


“Asubuhi ya leo (jana) tulipigiwa simu na RPC (wa Iringa) na kudai kuwa wanataka kuonana na viongozi wa Chadema, huku wakiwa na hoja kuwa tuahirishe kufanya mkutano kutokana na Sensa.
Hoja nyingine ambayo mimi naona ni ya upuuzi ni ile ya kusema kwamba wananchi wa Iringa watakuwa wameathirika na kifo cha kijana aliyekufa Morogoro,” alisema Dk Slaa.


Alisema baada ya kutokubaliana na hoja hizo, alipigiwa simu na IGP Mwema akimwomba asitishe mkutano na maandamano ya mkoani Iringa kwa kuwa hiyo ni amri kwa vyama vyote vya siasa na si Chadema pekee.

“Nimeongea na IGP leo kwa dakika zaidi ya 40 akisema Dk Slaa sijawahi kukuomba hata siku moja, naomba nikuombe na usinikatalie kati ya siku nne hadi tano kuanzia sasa tumezuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwapo kwa Sensa naomba tuelewane,” alisema Dk Slaa akimnukuu IGP Mwema.

Vurugu za Morogoro
Juzi, chama hicho kikuu cha upinzani kilifanya maandamano mjini Morogoro na kuzua taharuki, baada ya kutokea vurugu wakati polisi walipoamua kuyasambaratisha na kusababisha mauaji ya mtu mmoja, Ally Zona (38) mkazi wa Kihonda

Akizungumzia kifo hicho, Dk Slaa alisema chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazishi ya kijana huyo kulingana na ratiba ya ndugu wa marehemu.

“Endapo familia itaamua kusoma dua hapa Morogoro na kuzika hapa, tutashiriki kikamilifu. Tumejadiliana na wanafamilia kuna mambo ya msingi tumekubaliana na walichoomba ni kusaidia kusafirisha mwili. Hatutajali itikadi aliyokuwa nayo marehemu,” alisema.


Nchimbi achunguza
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi ametuma kikosi maalumu mkoani Morogoro kuchunguza mauaji ya kijana huyo anayedaiwa kupigwa risasi na polisi katika vurugu hizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo hivyo itahakikisha uchunguzi unafanywa na hatua kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika.

Alisema polisi walipata taarifa ya kuwapo kwa mtu mwenye majeraha umbali wa mita 300 kutoka eneo la tukio na kwamba wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitali ambako alifariki dunia.
Aliishutumu Chadema kwa kukaidi amri ya polisi iliyowataka wasiandamane.

UVCCM yalaani
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekishutumu Chadema ukisema kimehusika na mauaji ya kijana Zona yaliyotokea juzi mjini Morogoro.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema: “Tunatoa pole kwa vijana na wananchi wa Morogoro kwa kuondokewa na kijana wao na tunataka uchunguzi ufanyike haraka ili wajulikane waliofanya kitendo hicho.”
“Haiingii akilini kusema Jeshi la Polisi linahusika wakati wafuasi wa Chadema walikuwa wanaonekana vizuri kwa sare zao halafu wawaache na kwenda kumuua mtu aliyekuwa anaendelea na shughuli zake za uuzaji wa magazeti.”

Habari hii imeandikwa na Nora Damian, Tausi Ally, Habiba Yahya na Lilian Lucas na Clement Sanga.

 
Nimeona ITV habai za saa sasa hivi msafara wa CDM umezuiliwa kuingia Iringa baada ya wananchi kukusanyika kandokando ya barabara.

Baada ya kuzuiliwa msafara wao waliamua watembee kwa mguu lakini pia walikataliwa kwa hofu ya kutoa tafsiri ya maandamano.

Nimeona watu wakiwazomea polisi bila woga wowote wakati polisi hao walipokuwa wakisubiri amri zaidi huku wakiwa wamezuia njia. labda habari hii itakuwepo saa mbili mnaweza usiku kwa kirefu.

Nilichojifunza: Chadema wanapewa umaarufu na vyombo vya dola.
 
Haya tena hata wakitembea ndani ya nchi yao wanawahofia? kwani msafara una viongozi gani?
 
Nimeona ITV habai za saa sasa hivi msafara wa cdm umezuiliwa kuingia iringa baada ya wananchi kukusanyika kandokando ya barabara.

Baada ya kuzuiliwa msafara wao waliamua watembee kwa mguu lakini pia walikataliwa kwa hofu ya kutoa tafrisi ya maandamano. nimeona watu wakiwazomea polisi bilsawoga wowote wakati polisi hao walipokuwa wakisubiri amri zaidi huku wakiwa wameziua njia. labda habari hii itakuwepo saa mbili mnaweza usiku kwa kirefu.

Nilichojifunza: Chadema wanapewa umaarufu na vyombo vya dola.
dah,[polis wananishangaza sana,sasa waliwataka hao chadema wapae na kujikuta wako ndani ya nyumba.
kweli polis wanaisaidia sana chadema kwenye harakati za ukombozi,
maana hata kama hukuwa na nia ya kufatilia chadema,inabidi tu ufatilie ili ujue hawa chadema kwanini wanapingwa hivi!
 
Polisi wakisikia makamanda wa Chadema wameingia ktk eria yao basi matumbo jooto,hivi hawa polisi wanashinikizwa au wanajituma wao kuyafanya haya wanayoyafanya?Kwani Chadema wamekosa nini mpaka wazuiwe kuingia ktk ardhi ya nchi yao huko Iringa?
 
nimeona itv habai za saa sasa hivi msafara wa cdm umezuiliwa kuingia iringa baada ya wananchi kukusanyika kandokando ya barabara.

Baada ya kuzuiliwa msafara wao waliamua watembee kwa mguu lakini pia walikataliwa kwa hofu ya kutoa tafrisi ya maandamano. Nimeona watu wakiwazomea polisi bilsawoga wowote wakati polisi hao walipokuwa wakisubiri amri zaidi huku wakiwa wameziua njia. Labda habari hii itakuwepo saa mbili mnaweza usiku kwa kirefu.

nilichojifunza: Chadema wanapewa umaarufu na vyombo vya dola.

yote haya, yanapangwa na kina mwigulu, wakidhani wanaihujum chadema, kumbe wanaipaisha
 
Back
Top Bottom