Mkutano wa ccm pale jangwani unahusu nini?

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Ni uongozi mbovu au duni unaogopa kuamua au kutekeleza mambo yaliyokwisha kuamuliwa (Edward M.Sokoine, march.1983) Ndugu wana jf,nimemua kuanza na nukuu ya Sokoine ili tuweze kupima mwelekeo wa ccm.Ni kwa miaka sasa kama taifa tumeshuhudia ufisadi wa kupindukia,hali ngumu ya maisha,upungufu wa madawa hospitalini, malimbikizo ya madeni ya waalimu,mfumuko wa bei,ukosefu wa miundo mbinu ya kibiashara iliyopelekea migogoro baina ya machinga na jiji haswa Mbeya na Mwanza.Matatizo hayo ni kipimo tosha cha kushindwa au kutotekelezwa kikamilifu kwa sera za ccm.Sasa kesho nimesikia kuna mkutano wa ccm tena wiki moja tu baada ya CHADEMA kufanya mkutano eneo hilo hilo.CCM ni chama kilichoshika dola,hivyo kina kazi ya kuhakikisha sera zake zinatekelezwa kwa vitendo na siyo kwa ngonjera za jukwaani.Nataka wana ccm na wengine wenye kujua ukweli: CCM wanataka kuwaambia nini wananchi? Je,kutakuwa na ripoti ya utekelezaji wa sera ya kujivua gamba? Je,Nape ataeneza itikadi za kutorosha wanyama mchana kupitia KIA?
 
Pale buguruni wameweka bango kuwa "ccm itatoa msimamo juu ya mchakato wa katiba mpya" nadhani ndo ajenda yao baada ya Lissu kuharibu ile tar.26
 
Wanaenda kuishitaki chadema kwanini inaongoza nchi ili hali ikijua wao ndo chama tawala
 
Pale buguruni wameweka bango kuwa "ccm itatoa msimamo juu ya mchakato wa katiba mpya" nadhani ndo ajenda yao baada ya Lissu kuharibu ile tar.26

Ni upepo tu unapita, frankly speaking sasa naamini chama dume linakimbizwa kwa mbio staili ya kamata mwizi men. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeez!!!
 
Ni upepo tu unapita, frankly speaking sasa naamini chama dume linakimbizwa kwa mbio staili ya kamata mwizi men. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeez!!!

watakuja na mabango ya picha za mbgune wa ARUMENI MANENO ALIYOSEMA KUTAKA KUMWAGA SUMU! ILA WAKIANYA HIVYO NINADHANI MCD WANAZO STATEMENT NYINGI ZA CCM KAMA VILE KAMA NI MAJANI MTAKULA ILA NDEGE LAZIMA ININULIWE!
 
Hizi habari za Shibuda kurudisha kadi zina ukweli kadiri gani? Yule aliyewaambia wananchi wapige mbizi kama hawamudu bei ya kivuko naye ataongea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom