Mkutano Mkuu Wa CCM - Matarajio Ya Kujiokoa?

...wakati mkutano mkuu wa ccm unaanza leo kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA imebadilishwa na sasa mabango yanasomeka MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAKUJA KWA KUJITUMA NA KUFANYA KAZI!! ..yetu macho...

tunautakia fanaka na mafanikio mkutano mkuu wa CCM...WAJUMBE watuletee viongozi waadilifu wasiotokana na na rushwa.."KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA WAADILIFU WASIOTOKANA NA RUSHWA NA UFISADI INAWEZEKANA..."
 
Afadhali Wamekubali Ukweli Kuliko Kuwadanganya Watumishi Wa Bwana ,,niliwambia Hawa Wanaitaji Maombi Mungu Atawabalidisha
Hii Ndio Ccm Bwana ''iliokuwa Aiongeleki Hivi Sasa Butiku Anawachungulia ,,tupige Goti Jamani Mambo Mengi Yanakuja,,baada Ya Uchaguzi Wa Leo Kuna Waungwana Watakuwa Awapendi Kwa Kutokuchaguliwa Kwao Watatupa Mengi Sana
Mugu Awabariki
 
Oh... it sounds like the old Benja's "MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE"! Je ina maana hawana kitu kipya?
 
...wakati mkutano mkuu wa ccm unaanza leo kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA imebadilishwa na sasa mabango yanasomeka MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAKUJA KWA KUJITUMA NA KUFANYA KAZI!! ..yetu macho......"

Kujituma na kufanya kazi kwa mshahara gani!? Kama huo wa kulaliwa ambao unapigiwa kelele na wafanyakazi katika kila kona ya Tanzania basi umaskini ndio utaendelea kukithiri. Hii ni kwa sababu ongezeko la gharama ya maisha lina kasi kubwa ukilinganisha na kipato kidogo cha wafanyakazi wa Tanzania. Ni mafisadi, wala rushwa, viongozi wanaojilimbikizia mali ndio wataendelea kuyafaidi maisha bora kupitia migongo ya walipa kodi.
 
Hivi kweli Watanzania hawajitumi jamani? Ni wangapi ambao kile kukicha wanahangaika kufanya kweli katika shughuli zao, vibustani, vioski, hadi wanawatuma watoto kwenda kuuza mchicha.. wanaposema kujituma wanataka wajitume kufanya nini?
 
Naomba ufafanuzi wa kauli mbiu Hii - hasa tukimtazama mkulima kijijini na huyo mlalahoi - Msukuma Mkokoteni...
 
Mkandara, wasipoangalia watawapa watu tafsiri potofu ya kujituma sana hasa kama wao ndio mfano wa kujituma huko.
 
Hivi kweli Watanzania hawajitumi jamani? Ni wangapi ambao kile kukicha wanahangaika kufanya kweli katika shughuli zao, vibustani, vioski, hadi wanawatuma watoto kwenda kuuza mchicha.. wanaposema kujituma wanataka wajitume kufanya nini?

Mwanakijiji, hawa viongozi siku zote wanataka kuwatupia lawama za umaskini Watanzania badala ya sera zao mbovu na ubinafsi uliokithiri. Miaka ya nyuma kabla ya Watanzania kuanza kwenda kufanya kazi kati nchi zilizoendelea, vingunge walidai kwamba Watanzania ni wavivu. Baada ya Watanzania kuanza kufanya kazi katika nchi hizo, Watanzania wakajiuliza iweje wavivu waliozaliwa na kulelewa Tanzania waende kufanya kazi nchi zilizoendelea na kuwa na mafanikio makubwa. Mafanikio ya Watanzania hao yakanyamazisha kelele za "Watanzania ni wavivu." Sasa wamekuja na mpya lakini jibu lake ni kwamba hata Watanzania wakijituma vipi kamwe hawataachana na umaskini kwa kuwa mishahara yao ni ya chini mno kulinganisha na nchi mbali mbali duniani, hata za majirani.

Iweje Botswana, Namibia na nchi nyingine za jirani zinaweza kuwachukua madaktari wetu na kuwalipa mishahara mizuri? Nchi hizi zimetuzidi nini kikubwa mpaka ziweze kuwalipa vizuri madaktari wetu wakati Tanzania inaendelea kuwalalia na kuwadharau?
 
Watanzania naomba tuwaombee viongozi wetu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Taifa kwa mwaka huu limekuwa likipatwa na majonzi mengi, na tumwombe Mungu atuepushe na machozi, na wale watakaoangushwa wasiumie mioyo na kudhurika afya. Tumwombe Mungu watakaoshindwa wakubali kushindwa kwa mioyo ya ucheshi! Wingu la huzuni na litanduke toka Anga la Dodoma!
 
Watanzania naomba tuwaombee viongozi wetu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Taifa kwa mwaka huu limekuwa likipatwa na majonzi mengi, na tumwombe Mungu atuepushe na machozi, na wale watakaoangushwa wasiumie mioyo na kudhurika afya. Tumwombe Mungu watakaoshindwa wakubali kushindwa kwa mioyo ya ucheshi! Wingu la huzuni na litanduke toka Anga la Dodoma!

Mkuu,
What exactly did you mean by this ?
Mengine nimekuelewa perfecto !
 
Haki ya nani!!! ni ujinga uliokithiri kama si uzuzu kwa anaesema na anaeamini kuwa maisha bora yanakuja kwa kauli tu!!!!

Sera nzuri+Umakini na uadilifu ktk utekelezaji wa sera+uchapa kazi na uwajibikaji (Viongozi na wananji pia) = Maendeleo = Maisha bora

Ni ukweli usiohitaji kufikiri kuwa Viongozi wetu wengi ni wababaishaji na si waadilifu lakini pia waTZ bado tuna tabia ya uvivu na kupenda short cuts. Hapa ni biashara ya Mbwa kala Mbwa!! Viongozi na Wananji wote tubadilike kifikra!!!

Hebu mida ya J3 muda wa kazi pita vijiweni utakuta watu wanapiga story, pita Samora utakuta watu kama wanne watano wapo ktk kioski cha kuuzia magazeti, shoe shiner au kibanda cha simu. Ni upuuzi gani huu??? halafu tunasema Wahindi wanafaidi matunda ya nji hii?? Hali hiyo kwa sasa hata vijijini ipo, kilimo ni cha wazee tu! nenda buseresere, kijiji katika mpaka mwa MZA na Kagera utakuta vijana wanacheza pool mchana kweupee wengine wanazungusha wese la magendo (Disel ya wizi), hali hiyo ni kawaida kwa vijana wa vijiji vingi vilivyo ktk barabara kuu. Tatizo la Tabia ya uvivu, uzembe lipo wajameni!!!! Na kwa mtaji huo maisha bora kwa kila MT ndoto.
 
Siasa safi, Uongozi bora, ndivyo vitu vinavyokusekana katika kufanikisha maisha bora ya Mtanzania. Nafikiri mazingira ya sasa hata tukijituma vipi watafanikiwa wale tu ambao wanajituma katika njia zisozo halali. Tusubiri mpaka pale wale wale wanaopinga mambo ndani ya CCM na mpaka sasa wamekuwa waoga,kwa maneno mengine bado hawajaamua kuwa viondozi wa kweli watakapo choka na ama kutoka ndani ya CCM au kuanzisha vita wakiwa ndani ya waziwazi kama ilivyo kenya ndio tutaona mabadiliko ya kweli Tanzania, Vinginevyo ni maneno na usanii tu.

Namsikitikia JK kwani ananipa taswira ya kiongozi anayetamani mambo bora kwa Watanzania lakini anashindwa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti marafiki ndani ya Uongozi wake wasiharibu matarajio yake,matokeo yake imani za watu zinapotea kwa kasi dhidi yake. Kitu ambacho nafikiri asichojua pamoja na wasaididizi wake kwamba Wwatanzania wechoshwa na wanaelewa kinachoendelea kwani hata Vijijini watu wamechoka na maneno matamu bila matendo.

Mungu bariki Tanzania yetu na uibadilishe mioyo hii migumu ya viongozi wetu wapate tambua tunaelekea pabaya.

Ameni
 
kujituma huku kulikokusudiwa labda kwenda kuiba!! tujitume kiasi gani.

wanataka kutupiga changa la macho tu, kila siku wanakuja na hadithi nyengine, waonyeshe vitendo sio maneno matupu
 
Watanzania naomba tuwaombee viongozi wetu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Taifa kwa mwaka huu limekuwa likipatwa na majonzi mengi, na tumwombe Mungu atuepushe na machozi, na wale watakaoangushwa wasiumie mioyo na kudhurika afya. Tumwombe Mungu watakaoshindwa wakubali kushindwa kwa mioyo ya ucheshi! Wingu la huzuni na litanduke toka Anga la Dodoma!

Tuiombee nchi na wananchi ambao viongozi ni sehemu yao! Tuombe Mungu pia atujalie busara za kuchuja pumba na mchele ili tuweze kuchagua viongozi wazuri.
 
Back
Top Bottom