Mkurugenzi wanyamapori afukuzwa kazi

Hii kali ya mwaka kwelikweli maana kufukuza watu 2 sioni kama ndio kumaliza tatizo la corruption in public sector that is rampant no doubt about it. Waziri kama kachukua uamuzi huo ni uonevu wa mkubwa maana huu utoroshaji wa wanyama hai akiwemo twiga ni kitu ambayo ina involve chain kubwa.

Wako wapi usalama wa Taifa, PCCB, Polisi, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA)Mamlaka ya Mapato ambao by virtue of checking should have approved list of what has to be imported and what what purpose.

When are the stakeholders in this saga. Walifanya nini kuzuia aibu hii isitokee. Ndege ya kijeshi ilitua kwanza ahalafu ndio twiga wakawindwa? Iliomba kibali kwa nani maana mkurugenzi wa wanyama poli asingweza kufanya hivyo.

Wadau naomba ili swala lifanyiwe scrutiny zaidi maana inaonyesha kuna yaliyofichwa na wanataka yaishie chini ya busati. NO! Tanzanians have been made cheap for so long by ruling and state functionaries but it's time to query to the apex of our voices.

Vyombo vya habari pazeni sauti kama ilivyofanya RAIA Mwema ili tufukue mengi na tupate majibu ya kina yanayolenga kutibu hiki kilema cha wizi.
 
Hawa watu ni kuwafukuza tu na kuwaachia waende zao kwa sababu wakienda mahakamani tunajua mahakama zetu zinavyonuka rushwa watatoa hela kesi itakaa mahakamani kwa miaka 5 alafu jaji atasema hakuna ushahidi wa kutosha kesi itatupwa na kwa hiyo miaka 5 pesa za walipa kodi zitakazotumia kuendesha hizo kesi ni nyingi mnoo...so kuliko kupoteza pesa zetu jamani hao watu wala wasipelekwe mahakamani, washapigwa chini inatosha nina uhakika wana majumba, viwanja mashamba, makampuni binafsi kwa hiyo hawatalala na njaa
Acha wafanye hivi kwa sababu itatuongezea uelewa mwingine wa jinsi mahakama nayo inavyonuka rushwa. Mkusanyiko wa mambo kama haya ndio utawaamsha wananchi kuleta mabadiliko ya utawala yanayoihitajika hivi sasa
 
ningewaona wa maana kama wangerudsha wanyama we2 na jamaa apelekekwe akanyee ndoo
 
Amefukuzwa tu? Hakuna kosa la jinai hapo?

Step by step bro, unaondolewa ofisini kwanza ili uchunguzi ufanyike.

Uchunguzi unafanyika wakati wewe upo home, unaweza kukuta amesimamishwa kwanza hajafukuzwa. Then uchunguzi ukikamilika ndio mahakamani. Kama kweli anahusika na usafirishaji wanyama wetu mimi naona afungwe tu.
 
ningewaona wa maana kama wangerudsha wanyama we2 na jamaa apelekekwe akanyee ndoo!!
 
Hii Serikali gani hiii.........eti Imewafukuza Kazi THEN what Next?

Inatakiwa Kuwafukuza kazi , Wafilisi kila walicho nachoo na mwisho Unawaweka Ndani (Sero).

Watu wakiona hv Hakuna atakayechezea Mali ya Umma.....Wooooooote watashika Adabu
 
Hii kali ya mwaka kwelikweli maana kufukuza watu 2 sioni kama ndio kumaliza tatizo la corruption in public sector that is rampant no doubt about it. Waziri kama kachukua uamuzi huo ni uonevu wa mkubwa maana huu utoroshaji wa wanyama hai akiwemo twiga ni kitu ambayo ina involve chain kubwa. Wako wapi usalama wa Taifa, PCCB, Polisi, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA)Mamlaka ya Mapato ambao by virtue of checking should have approved list of what has to be imported and what what purpose........
Mamlaka ya viwanja vya ndege na Polisi hawawezi kuzuia mnyama asisafirishwe wakati kuna baraka zote za Wizara husika. Wanyama pori kuuzwa au kusafirishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine sio jambo la ajabu.Tatizo hapa utaratibu uliotumika.
 
Mwaka jana mwezi kama huu aliyekuwa waziri wa wizara hiyo (Maige) alitangaza ndani ya bunge kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo. Mwaka mmoja baadaye katika mazingira yanayofanana (ndani ya bunge) waziri mwingine wa wizara hiyo anatangaza kufukuzwa kazi kwa mtu huyo huyo.

Swali la kujiuliza ni kuwa baada ya kusimamishwa na Maige alirudi kazini baadaye ama alikuwa bado kasimamishwa. Kama alikuwa bado kasimamishwa mbona uchunguzi umechukua muda mrefu hivyo!!!

Ama kweli Tanzania ni zaidi ya tunavyoijua!!

http://www.mwananchi.co.tz/componen...-wasimamishwa-kazi-kashfa-ya-wanyamapori.html
 
Mkuu Mwitongo na Mods,
Tafadhali badilisheni Heading ya hii post. Kwa Sheria ya Sasa ya Ajira na Mahusiano Kazini, hakuna adhabu inayoitwa 'kufukuzwa Kazi', bali 'kuachishwa kazi'.

Kuna tofauti kubwa sana ya kimsingi na kimantiki kati ya Summary Dismissal na Termination of Employment, bila kujali kosa lililofanywa ni gross kiasi gani.

Kama GTs, tujitendee haki!
 
Huu ni uonevu mbaya kuliko wote unaofanywa na wanasiasa dhidi ya watumishi wa serikali,ni vigumu kuamini lakini imetokea kama wakienda mahakamani Kagasheki hana uwezo wa kumfukuza kazi,huyu madudu kayakuta kazi anafukuzwa kwa makosa ya wengine,au sasa waseme ukweli kuwa Rais anahusika katika sakata hili?

Iweje ndege ya Jeshi QATAR ARMY ije nchini isubiri mzigo kwa mwezi mzima Muheshimiwa sana asijuwe na kinachotokea ndani ya nchi,wanyama wamekamatwa kweupeee tena kwa shinikizo la Ikulu na kupakiwa katika magari msururu hadi uwanja wa ndege na kupakiwa katika hilo dege la kijeshi chini ya maofisa usalama tena ikulu ikiwa na habari, kwa nini wamemtorosha yule mpakistani aliyekuwa na hiyo order ya hao waarabu?passport mlimrudishia ya nini si ili asiseme ukweli.

Mbona hamsemi hao wanyama wamepelekwa wapi kila siku inafichwa eti hawajulikani walipo ni uongo tu ikulu inajua kila kitu.sasa naamini yale aliyokuwa akisema EL kuwa na mkuu anahusika namba moja katika Richmond ila yeye katolewa sadaka ni kweli kabisaaaa.ila huu si uungwana kama umeshika kigoda ukiboronga jitetee utetee na wengine siyo kujifanya msafi kwa kuharibia wengine maisha wakati uozo unaanzia hukohuko Ikulu.

Mbona Mkapa alikuwa anawatetea watumishi ikiwa wamefanya makosa yatokanayo na utendaji wake wa kazi.hivi ni Twiga wangapi wanauwawa na majangili kwa ajili ya kitoweo kila siku hapa nchini na je serikali imekusanya kiasi gani kutokana na zoezi hili la kijangili, hao Twiga wawili tu waliosafirishwa tena kwa kutoa fedha serikalini ndiyo inakuwa sababu ya kufukuzisha watu kazi tena Twiga mwenyewe ni nembo ya taifa bila kibali cha rais hawezi kukamatwa wala kuwindwa,

Hili halikwepeki mzigo wote ni wa mkuu kabisa ila hawa watendaji wanatolewa kafara kuficha maovu wakati walikuwa wanatekeleza maagizo ya wakubwa hao wanasiasa tena kwa kulazimishiwa: kama hautaki kazi wacha usifanye hiyo kazi niliyokuagiza", au kuogopa kusemwa vibaya, haya limetokea kwa nini mtumishi huyo huyo usimteteee badala yake unajisafisha kwa kuwatumia watumishi haohao tena kwa ubaya mbaya kabisa lakini ikumbukwe kuwa haki ya mnyonge haipotei hata siku moja iko siku ataipata tu.

Inauma sana kwa wanasiasa kuchezea ajira za watumishi kwa maslahi yao.
 
Sijafurahia hii habari ya kufukuza watu kwenye idara ya wanyama pori. Sijafurahia kwasababu kufukuza mtu kazi sio suluhu ya matatizo ya kimfumo yaliyopo kwenye idara ya wanyama pori na idara nyingine za serikali.

Kwa wanaokumbuika alikuwepo mkurugenzi makini pale wanyamapori kwa jina la Severe kama sikosei, alifukuzwa kazi na watu walishangilia sana wakidhani matatizo yameisha. Sasa wamemfukuza na huyu then atakuja mwingine naye atafukuzwa?

Kuna wakongwe wa biashara hizi ambao ni watu wazito nchini wala hawaguswi. Mfano lile sakata la pembe zilizokutwa Vietnam liliashaje?

Na Dr. Komba ambaye kwasasa ni balozi wetu pale Uganda, aliondolewaje maliasili na kwenda kusoma magazeti wizara ya mambo ya nje kwa muda mrefu tu? Hapa kuna wakongwe wameachwa kama ilivyokawaida kwa serikali za Africa na kutafuna wadogo.
 
Kafara hiyo. Mipapa imeachwa vidagaa vinatolewa kafara. Kagasheki be careful!!!!
 
Hii kali ya mwaka kwelikweli maana kufukuza watu 2 sioni kama ndio kumaliza tatizo la corruption in public sector that is rampant no doubt about it. Waziri kama kachukua uamuzi huo ni uonevu wa mkubwa maana huu utoroshaji wa wanyama hai akiwemo twiga ni kitu ambayo ina involve chain kubwa......
You are very right,Rais alikuwa anajua kila jambo katika ukamataji wanyama na anajua walipo hawa wanyama na hii ilikuwa ni tenda yake na alikuwa anasimamia kikamilifu zoezi hili pamoja na vyombo vyote ulivyovitaja vilikuwa na habari hii kua kuna mkono wa Ikulu kwa nini awafukuze kazi?

Dege la jeshi tena QATAR ARMY linawezaje kukaa nchi au kuingia nchini na kusubiri muda mrefu hao wanyama bila kubughudhiwa na kutorosha wanyama? Sasa watumishi lazima wajipange siyo kila jambo litokalo Ikulu ni jema kumbe mengine ni mabomu ya wakubwa.
 
Na mashita wafungukiwe sio kuachiwa tu mtaani vifua mbele wakiendela ku-collude na wanaobaki kazini kuendeleza uhalifu!
 
Na mashitaka wafunguliwe sio kuachiwa tu mtaani vifua mbele wakiendela ku-collude na wanaobaki kazini kuendeleza uhalifu!
 
Mtu kushangilia hatua hii ni kutoona upeo kamili wa skandali hili. Hapa ni zaidi ya "wizi" wa kawaida wa maliasili. Huu sio ujangili wa kawaida. Ni ngazi ya Ikulu (na Usalama wa Taifa) tu ndio wanaoweza kuondoa wingu hili. Na wana watu sehemu zote zilizohusika na mwondoko mzima.

Hivyo, Kuanzia watendaji wakuu Wizarani hadi ngazi za Ikulu hawana budi kuanguka na kisha Ikulu ikatolea ufafanuzi wa sakata zima na hata, ikibidi, kutuahidi kwamba hujuma ya aina hii (kwa maliasili na usalama wa nchi yetu) haitajirudia tena.

Manake ni kama hatuna nchi vile bali mkusanyiko wa watu maslahi binafsi tu. Ukiunganisha na mapya kama ya kupepeza bendera ya nchi kwenye meli za Iran - hatuna nchi hapa!

We certainly need to rein in the guys at the very top. Nini kuishia kumtimua kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori na watendaji wenzake?
 
Back
Top Bottom