Mkurugenzi wa wilaya mahakamani kubatilisha matokeo ya uchaguzi- Ushindi Chadema

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani chato mkoani kagera kimemburuza kortini mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chato Hamida Kwikwega kwa madai ya kubatilisha ushindi wa mwenyekiti wa kijiji cha Nyakakarango Zamda Kusoya (Chadema) aliyekuwa amechaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 15 mwaka huu.

Zamda S. Kusoya alishinda kwa kura 178 dhidi ya mpinzani wake John Athanas (CCM) aliyepata kura 155 na ushindi huo kutangazwa na kaimu mtendaji wa kijiji Peter George.

Baada ya kutangazwa ushindi huo inadaiwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo alitumia nafasi yake vibaya kupinga na kutotambua matokeo ya mwenyekiti huyo kwa madai uchaguzi haukuzingatia taratibu na kanuni ikiwemo kutoapishwa kwa msimamizi Peter George wa uchaguzi huo. Kutokana na hali hiyo Chama Cha Demokrasia na maendeleo kilimtaka Mkurugenzi huyo kuyatambua matokeo hayo na kwamba iwapo kuna kanuni ambazo hazikuzingatiwa hana budi kuweka pingamizi mahakamani na si yeye kubatilisha matokeo hayo.

Katibu wa Chadema wilayani Chato Mange Sayi amesema Chama chake kimelazimika kumburuza mahakamani mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa ameshindwa kuzingatia kanuni za uchaguzi kama zinavyomuelekeza. "Sisi kama Chadema tumelazimika kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato kwa kuwa amekuwa akishindwa kusimamia taratibu na kanuni za chaguzi kutokana na maslahi ya chama tawala".alisema Sayi

Aidha katibu huyo amesema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusomwa machi 14 mwaka huu katika mahakama ya wilaya hiyo.
Mbali na Mkurugenzi huyo kaimu mtendaji wa kijiji cha Nyakakarango Peter George ataunganishwa kwenye mashitaka hayo kutokana na kusimamia uchaguzi kisha kutangaza matokeo hayo na baadaye kushinikizwa na Mkurugenzi wa halmashauri kutomtambua mshindi halali.
 
Huyu mkurugenzi kama ana akili kama za dadake aliyewai kuwa mkuu wa wilaya ya kasulu<naye ni kwikwega> basi yote ni mab...gus
 
Uchaguzi wenyewe kumbe wa udiwani. Chadema wana njaa ya hatari sana.

Shameful comment!
Nini basi maana ya uchaguzi? Kuna haja gani ya kupoteza fedha za kuandaa uchaguzi na raslimali nyingine? Wewe ni muumini kweli wa Demokrasia au unatanguliza na kujali tu maslahi yako tu?
 
Aina ya hawa wakurugenzi ndo watasimamia mchakato wa kuandika katiba mpya? Kumbe bado sheria iliyopitishwa majuzi na Bunge haitafanya la maana! Yaani huyo amepindisha matokea live bado kuna kesi?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani chato mkoani kagera kimemburuza kortini mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chato Hamida Kwikwega kwa madai ya kubatilisha ushindi wa mwenyekiti wa kijiji cha Nyakakarango Zamda Kusoya (Chadema) aliyekuwa amechaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 15 mwaka huu.

Zamda S. Kusoya alishinda kwa kura 178 dhidi ya mpinzani wake John Athanas (CCM) aliyepata kura 155 na ushindi huo kutangazwa na kaimu mtendaji wa kijiji Peter George.

Baada ya kutangazwa ushindi huo inadaiwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo alitumia nafasi yake vibaya kupinga na kutotambua matokeo ya mwenyekiti huyo kwa madai uchaguzi haukuzingatia taratibu na kanuni ikiwemo kutoapishwa kwa msimamizi Peter George wa uchaguzi huo. Kutokana na hali hiyo Chama Cha Demokrasia na maendeleo kilimtaka Mkurugenzi huyo kuyatambua matokeo hayo na kwamba iwapo kuna kanuni ambazo hazikuzingatiwa hana budi kuweka pingamizi mahakamani na si yeye kubatilisha matokeo hayo.

Katibu wa Chadema wilayani Chato Mange Sayi amesema Chama chake kimelazimika kumburuza mahakamani mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa ameshindwa kuzingatia kanuni za uchaguzi kama zinavyomuelekeza. “Sisi kama Chadema tumelazimika kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato kwa kuwa amekuwa akishindwa kusimamia taratibu na kanuni za chaguzi kutokana na maslahi ya chama tawala”.alisema Sayi

Aidha katibu huyo amesema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusomwa machi 14 mwaka huu katika mahakama ya wilaya hiyo.
Mbali na Mkurugenzi huyo kaimu mtendaji wa kijiji cha Nyakakarango Peter George ataunganishwa kwenye mashitaka hayo kutokana na kusimamia uchaguzi kisha kutangaza matokeo hayo na baadaye kushinikizwa na Mkurugenzi wa halmashauri kutomtambua mshindi halali.
Mkuu nakwaminia kwa taarifa zilizo makini, hawa maghamba wanadhani Tanzania ya jana ni sawa na leo, wacha apambane na mkono wa sheria sasa!!!!
 
Back
Top Bottom