ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Bw. Nehemia Mchechu
Pengine inatafsiriwa kana kwamba Bw. Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) ameonekana kana kwamba anajitafutia umaarufu wa haraka katika nyaja ya uongozi na hasa kupitia vyombo vya habari kwamfano:
Alitumia waandishi kuwapa semina yenye kugharimu mamilioni ya Fedha za shirika kuwafundisha waelewe shirika ikwemo kumtumia Mjomba Mpoto kwenye matangazo.
Sasa amekuwa akionekana katika vyombo vya Habari hasa TBC 1 akitangzana mikakati ya shirika nk kwa kutumia fedha za shirika hilo ambalo mpaka hivi sasa limejikita zaidi kujenga na kukarabati nyumba maeneo ya mjini na kukosa kuwafikia wanyonghe walio wengi.
katika Gazeti la Mwanachi leo tarehe 13 Septemba, 2011, Bw. M.R.J. Sabodo ameandika makala ya malalamiko na kuhoji uhalali wa maswali ambazo NHC limeandaa kwa ajili ya kuuliza wapangaji wake. Maswali hayo mengi yanaoekana hayana mantiki yoyote ya kuboresha huduma za shirika hilo la Taifa. Kwa maoni ya Sabodo, ni ya kibaguzi na hata alipoongea na Mhe.
Waziri Mkuu nae ameshangaa kuona maswali kama hayo. Ukiyasoma maswali hayo utaona yanataka kuwaanika wapangaji wake kihali na kiuchumi. Maswali hayo yanataka kujua pamoja na mengine yanataka kujua taarifa binafsi za wateja (utaifa,uasili wa wapangaji kwa kuuliza "wewe ni mtanzania wa asili ipi (ulaya, asia, mweuisi nk) (originality), makazi yao, unahudumiwa na Benki gani, shule wanazosoma watoto, nk.
Kwa maoni ni kuwa Kama wao NHC wanataka kukusanya mapato zaidi, waweke mfumo unaoeleweka, hizi taarifa wanazotaka wapangaji watoe ni taarifa ambazo kimsingi zilipaswa kuwa sehemu yan mkataba wa pango na sio sasa wakati tayari mkataba unaendelea. Huu ni uelewa mdogo wa Mkurugenzi wa NHC, hizi taarifa hajui zinaweza kutumiwa vibaya dhidi ya wapangaji?
Kuna madai kuwa Mkurugenzi huyu alipatikana kimagumashi tu na hakuna uhakia kama anajua jinsi gani mashirika ya umma yanapaswa kuendeshwa.
Kuna madai kuwa pale NHC sasa kuna mikataba mingi ya hovyo ya wajiriwa toka ndani na nje ya nchi walioletwa na Uongozi mpya, na mingi itakuja kuwa mzigo kwa taifa...tusipoangalia, badala ya kufufua shirika, Shirika litaangamia kwa Mipango ya Kusadikika ya Huyu Mkurugenzi wa sasa.