Fisadi Mtoto
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 639
- 79
Nimeshangga sana kugundua kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Safi na Maji taka Moshi ,Bwana Antonny Kasonta ambaye miaka minne iliopita alilalanikiwa na Mh. Halima Mdee kuwa ni mbadhirifu na mwizi aliepelekea mpaka ofisi ya MUWSA kukopa hela za mshahara baada ya kufuja mapato anaendelea na kazi. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa amefunguliwa kesi kwa makosa ya uhujumu uchumi na kesi ya pili ki kwa kosa la ubadhirifu na wizi na kosa la tatu kwa kumfukuza kazi mzalendo aliemripoti Takukuru na kwa viongozi wa Chadema.mwaka jana katika Bunge Mh Halima Mdee aliuliza kwa nini akiwa anakabiliwa na kesi zote hizo tatu bado anaendelea na kazi na jibu la serikali kupitia kwa Mwandosya ni kuwa hata kama kashtakiwa kwa wizi lakini mamlaka yake ya uteuzi hailazimishwi kumsimamisha kazi kungoja majibu ya kesi yake...hapa si ajabu hata hawa mawaziri wote pia wakabaki.........Ni nchi ya ajabu kidogo ambako serikali inashindana na vyombo vyake yenyewe kutetea watuhumiwa.