Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Sidanganyiki N'go!

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,237
9,871
Leo asubuhi nimepokea ujumbe nikiitajika kuandika barua ya kudai hela ya muda wa ziada kazini (extra duty allowance) Nimeambiwa kabla ya saa sita leo mchana niwe nimeandika barua ya madai! Swali nililojiuliza ni hivi Yesu karibia anarudi hawa jamaa wanajuta dhambi zao? Haijawahi kutokea kwa miaka yote niliyofanya kazi hapa,hata hivyo mbona ni fasta fasta?tena unapigiwa simu wakati watu walishaacha madai hayo kwani huwa ni zengwe tu,iweje leo?
Mwana JF mwongozo wa malipo kwa kada za afya huwa ni hivi: wafanyakazi wenye degree ni sh. 10,000/ kwa siku, diploma 5000,na cheti 3000. Nimekataa,kama mnataka ku-Jairo digits yaani kuongeza 1 mbele ya 10,000
ili iwe 110,000/ mimi sidanganyiki! Kanunue dawa za wagonjawa, sitaki allowance zenu.
 
we daktari ama? kama ndio kwann ukatae stahili yako? kwani usipochukua watakula wao
kwani hakuna kitengo cha kununua madawa?
 
Sema unakataa kwa msingi gani?
Kuwa hukufanya OT?
Au kwamba walizibana ili malimbikizo yawe makubwa kisha wananihii nini?
 
we daktari ama? kama ndio kwann ukatae stahili yako? kwani usipochukua watakula wao
kwani hakuna kitengo cha kununua madawa?

hata kama ni stahili yangu,mbona siku zote naidai na sipati?iweje naambiwa mwisho wa kuiomba ni saa 6 mchana. Jiulize unadai hela za miaka mitatu nyuma na unaambiwa udai malipo ya kuanzia jan.mpaka julai 2011 tu! Hapa ni kudhalilishana tu,
 
Mambo ya bajeti broda financial year...keep your records for future!
Kawaida ya haki huwa ni kuzidai kwa nguvu tu!...kwa hiari utazisikia redioni!
 
Back
Top Bottom