Mkurugenzi wa ATCL David Mattaka astaafu Rasmi, Amrushia Dr Slaa Kijembe

Ogwari

Member
Apr 14, 2011
26
15
Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Bw David Mattaka leo ametangaza kuwa amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60

Amewaambia wanahabari ofisini kwake kuwa amelazimika kutangaza hadharani jambo hilo kufuatia tetesi kuwa ameshinikizwa kujiuzulu na Dr. Slaa pamoja na nguvu ya UMMA kutokana na ufisadi
 
tumegee vizur mdau, ni lini Dr Slaa alimlipua huyo? anadhani kustaafu mapema anaweza kuokoka kama kweli alikua fisadi? au ndo kubebana kama alivyobebwa mjomba Beni?
 
dah, afadhali vijana wetu wa kiume sasa watapumzika maana naskia jamaa alikua ........... dah
 
Kinachouma shirika kasaidia sana KULIFIKISHA LILIPO=LIMEPIGA MAGOTI kama siyo kuwa ICU...Na hakuna anachofanywa!! Mafao yake atapata na inawezekana wakati wa party ya kumuaga ukasikia wanampatia SIFA YA UTUMISHI ULIUOTUKUKA!!!! Jamani tuwe na mechanism ya kuwajibisha MIJIZI HII:-(
 
Atapewa uenyekiti na ujumbe wa bodi nyingi tu za wakurugenzi wa mashirika / mamlaka mbalimbali ya serikali.
 
Habari zilizo tufikia hevi punde zina sema mkurugenzi wa kampuni ya ndege ya atcl amejiuzulu rasmi kuyanziia leo kwa habari zaidi tutawaletea baada ya kuzungumza na press.
 
Habari zilizo tufikia hevi punde zina sema mkurugenzi wa kampuni ya ndege ya atcl amejiuzulu rasmi kuyanziia leo kwa habari zaidi tutawaletea baada ya kuzungumza na press.

Mkuu Pdidy unaharakishia wapi? mbona unaandika kiswahili kama kijaluo? asante kwa taarifa though!
 
Tanzania hamna kustaafu...mtashangaa anapewa kitengo ingali kuna vijana wamesoma na hawana hata ajira yoyote,nchi hii!
 
Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Bw David Mataka leo ametangaza kuwa amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60

Amewaambia wanahabari ofisini kwake kuwav amelazimika kutangaza hadharani jambo hilo kufuatia tetesi kuwa ameshinikizwa kujiuzulu na Dr Slaa pamoja na nguvu ya UMMA kutokana na ufisadi

Mkurugenzi wa ATCL yenye ndege 2 bora kama amempunzika maana alikuwa analipwa tu pesa za walipa kodi huku shirika likiwa ni mzigo
 
Back
Top Bottom