Mkurugenzi Mtendaji TANESCO asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.
Unajidai rafiki yako hata jina lake hulijui? ni Badra.

Mkuu na hii inaonesha kuwa huyu kapata taarifa kwingine anajifanya kapatia jikoni. Halafu habari kama hizi zinatakiwa kuwa za kina, maana ni tofauti na kifo ambacho mtu husema fulani is no more inatosha ila habari ya pink slip maana yake kuna more details. Otherwise inaweza qualify kuwa ni uzushi.
 
Amesimamishwa na bodi ya wakurugenzi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za shirika, msaidizi wake pi kasimamishwa
Na maafisa waaandamizi wengine ili kupisha uchunguZi wa tume huru.

Chanzo
Radio one
 
Amesimamishwa na bodi ya wakurugenzi kutokana na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka Pia wako maofisa wengine wa ngazi za juu.

ITV.
 
Watanzania watu wa ajabu sana, watu wa kuridhika na matatizo.

Wamekosa habari kwa sababu radio na TV zilizima, umeme ulikata, na ndio kawaida.

Kesho yake wanaamka na taarifa kwamba, mkubwa wa kampuni inayoshughulikia umeme kawa fired, wanauliza "kafanya nini?
"
 
Bodi ya Wakuregenzi ya TANESCO yawasimamisha kazi maafisa wake waandamizi kadhaa akiwamo na Mkurugenzi wake Mkuu Mhandisi William Mhando kwa kuhusishwa na Ubadhilifu na utumiaji mmbaya wa madaraka yao
 
Bodi ya wakurugenzi ya tanesco imemsimamisha kazi mkurugenzi mkuu na manaibu wawili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa mali za umma na matumizi mabaya madaraka. source taarifa ya habari ya TBC.
 
Watanzania watu wa ajabu sana, watu wa kuridhika na matatizo.

Wamekosa habari kwa sababu radio na TV zilizima, umeme ulikata, na ndio kawaida.

Kesho yake wanaamka na taarifa kwamba, mkubwa wa kampuni inayoshughulikia umeme kawa fired, wanauliza "kafanya nini?
"

Hapo mkuu umelenga,na akisimama jukwaani watakuwa wa kwanza kudai kuwa kaonewa.
 
Hii nchi kila mwaka kila sehemu imejaa watu wasio waaminifu, yaani inaliwa sana sana...kuna hizi idara za Procurement hilo ni genge linalofilisi hii nchi, utashangaa kitu cha laki 2 serikali inanunua kwa sh laki 8 mara 4 zaidi y bei halisi!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom