Mkurugenzi Mtendaji TANESCO asimamishwa kazi

Status
Not open for further replies.

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Robert Mboma amekataa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari unaotarajia kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, William Mhando.

Uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando unatokana na bifu linalosemekana kuwapo kati ya Mhando na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; lakini katibu mkuu huyo ametumia udhaifu wa serikali na tanesco kumwadhibu Mhando.

Inasemekana sababu inayotolewa na Katibu Mkuu ni kwamba Mhando alimdharau kwa kutompa taarifa kabla ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme wa hivi karibuni. Kwa mantiki hiyo, akamlima Mhando barua akisema anahujumu shirika. Hata hivyo, wananchi na watumishi wa Tanesco wanajua kuwa anayehujumu Tanesco ni serikali, ambayo inalinyima shirika hilo pesa ilizoahidi kwa ajili ya miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, na kulizuia shirika hilo kuuza umeme kwa faida, kwa sababu za kisiasa.

Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.
 
Bodi ya Tanesco imetangaza kumwachisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco kwa tuhumu za ubadhirifu na kushindwa kutatua mgawo wa umeme.
 
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Robert Mboma amekataa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari unaotarajia kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, William Mhando.
Uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando unatokana na bifu linalosemekana kuwapo kati ya Mhando na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; lakini katibu mkuu huyo ametumia udhaifu wa serikali na tanesco kumwadhibu Mhando.
Inasemekana sababu inayotolewa na Katibu Mkuu ni kwamba Mhando alimdharau kwa kutompa taarifa kabla ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme wa hivi karibuni. Kwa mantiki hiyo, akamlima Mhando barua akisema anahujumu shirika. Hata hivyo, wananchi na watumishi wa Tanesco wanajua kuwa anayehujumu Tanesco ni serikali, ambayo inalinyima shirika hilo pesa ilizoahidi kwa ajili ya miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, na kulizuia shirika hilo kuuza umeme kwa faida, kwa sababu za kisiasa.
Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.

source and updates please??
 
Tunasubiri Mkuu usikawie sana maana hii ni habari nyeti.
 
Ni habari niliyoipata kutoka kwa rafiki yangu Badra Masoud afisa habari wa tanesco ila hakunijulisha sababu na kuniahidi atanipa full habari muda si mrefu.
 
Toa habari zenye kukamilika. Amesimamishwa Na nani Na kwa kosa gani?
 
Amekosa nini jamani huyu kiumbe?, mbona anafanya kazi vizuri na anaimudu vyema kazi yake?.
 
hebu tungoje habari zaidi lakini huyu ni swahiba wa JK, sasa watakuwa wamechufuana katika migawo kwenye madili yao!
 
Ni kazi ya Prof. nini, maana ishakuwa hatari pale Wizarani (Raia Mwema trh 11-17 July, 2012). Safisha safisha Prof. maana Vilaza na vitope waliobahatika kujilimbikizia madaraka hata bila kuwa na sifa wanamaliza nchi yetu. Congzzzzzzzzzzzzzzz:A S 27:
 
Ni ile ishu ya Umeme Bungeni or, mbona vipaza sauti vilikuwa vinafanya kazi but taa ndio zilikuwa zimezimika, au hivyo vipaza sauti havitumii umeme, Mi nilidhani mule ndani walizima taa wenyewe wakijifanya umeme umekatika,(eti umeme umekatika) ili wamnyemelee Mnyika, but Mungu ni Mkubwa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom