Mkurugenzi mtendaji Gotham ni Mkurugenzi wa utafiti na ICT - TIC

Mbona alishaodoka huko miaka mingi akiaga kuwa kapewa ukurugenzi wa mradi wa vitambulisho! Na bado mengi yatajitokeza. Hata huyo Jack alishatumwa kwa jamaa yangu mmoja na Membe ili amsaidie technical insights kuhusu nyanja za ID systems. Jamaa akamtolea nje Jack baada ya kuliona tangazao katika Daily News toka TISS likuwatahadharisha wananchi kuwa yeye siyo mtumishi wa TISS ingawa ana-claim hivyo.

Hiyo project study ya National IDs walioiandika ni Computer Science Department ya Chuo Kikuu. Wizara ya Mambo ya Ndani ikaikalia na ikawapa hao kina Jack wakaidandia na kui-massage na kuigeuza kuwa yao. Ndio mwanzao wa kumleta Kyaruzai kwa vile alikuwepo kwenye lile jopo la Chuo Kikuu mwanzoni. Usahaidi upo na kama Jack au Kyruzi au Wizari inabisha basi waiweke hiyo document hadharani (Project Writeup) watalaamu wa plagiarism waipitie. Za mwizi ni arobaini tu!


ZalendoHalisi


This is very serious. Asante sana Zalendohalisi kwa taarifa hizi. Naomba waandishi wa habari mlioko humu muanze kuandika habari kama hizi ili umma upate kufahamu hizi mbinu chafu. Kama ni failure kwa mradi mdogo kama chuo, then anaweza kuwa mfanisi katika mradi wa taifa???

Jamani wekeni hadharani kabla tender rasmi haijatolewa. This is a shame, sijui Tanzania tunataka nini cheap cheap cheap tu!!! Always tunashauriwa kufanya value for money projects lakini Tanzania wanaimba tu but utekelezaji halisi kapuni. Sijui nihamie nchi gani hasa, nimechoka na uozo wa humu. Kweli billion 200 na ushee tunataka kuzichezea illi kutajirisha wachache??? Sijui tuamini nani ndani ya system hii.
 
Samahani kukazia kwenye issue moja, hii ya magari yaendayo kasi kwenye jiji la Dar es Salaam nasuburia na mimi Mwenyezi Mungu anipe uhai nione mwisho wa huo mradi.[/QUOTE


Yaani hao DART (Dar es Salaam Rapid Transport) kila maonyesho hapo Tanzania wamo , Sabasaba, nanenane, ...... yaani moaka Sullivan Summit walikuwamo. Wanacho diplay katika banda ni ramani ya basi yatakapoita na michoro ya imagination ya jinsi mabasi yatakavyokuwa i.e kapicha ka muundo. Ukiwauliza maswali kila siku jibu ni hilo hilo tu...... tunamalizia mchakato na mradi unaanza mara moja!!!! Hapo mtu unapata kicheko maana kwanza barabara zenyewe bado (say miundombinu) ambayo itachukua muda sana kukamilisha. They are never realistic katika maelezo yao, ni wadanganyifu. Unajua Tanzania tumeshageuzwa babies maana baby unamwambia kuwa kula haraka paka huyo.... basi anaogopa wakati pengine paka hajawahi kumwona. It is too much now.

Media inatakiwa ifanye kazi sana. Please editors saidieni kunusuru hii nchi. Jamii inadidimia. Na ile RIPOTI maalum ya kina Jerry Muro (ITV) inasaidiaje hapa??? Please, rescue this national and its citizens/nationals.
 
Nashukuru kwa hoja yako na mfano uliotoa.

Kwa kuwa umetoa mfano wa kampuni ya kihandisi nami nakushauri uende ERB uweze kujua kuwa huwezi kuwa Consulting Engineer kabla hujafanya kazi field kama Professional Engineer kwa walau miaka mitatu. Kwa maana nyingine Consultant uelewa na uzoefu wako kuhusu mradi husika ni vyema uwe wa juu kuliko mjenzi. Sidhani kuwa project nyingine kama hii tunayoongelea itahitaji Consultant kilaza kwa kuwa tu yeye haendi kujenga. Tukienenda kwa mawazo kama ya kwako hakika mwisho wetu hautakuwa mzuri.


Mzee... kuonyesha naelewa naomba nikupe mfano mmoja tu...

Kuna kampuni inaitwa Norconsult, imekuwa inafanya kazi ya consultation kwenye miradi mingi mikubwa ya barabara kama consultant na wakati mwingine project manager.

Sasa swali. uliwahi kusikia lini hili kampuni lina matingatinga ya kutengeneza barabara, au wapi walitengeneza barabara ya KM moja?

Hivyo nasema kuwa consultant au project managers... sio lazima uwe na uwezo wa kujenga barabara.... hivyo Kyaruzi kufeli kama constructor au implementer sio lazima ashindwe pia kwenye consultation.
 
Naomba kuchangia kama ifuatavyo:

1. Nimesoma makala ya RAIA mwema, na kwa maoni yao Huu mradi usimamishwe na fedha ihamie ktk Kununua matrekta. kwa Billion 200, Kilimo tutakuza Mno. na hapo wananchi watakuwa na uwezo ktk mifuko yao. Tumekaa muda bila vitambulisho, lkn hatuwezi kukaa bila chakula cha uhakika, na serikali imeshatangaza Upungufu wa chakula.

2. Kwa wale Wanaompinga Dr.Kyaruzi sina hakika na augument zao za kweli au la. tu-assume Kyaruzi si Dr. na ameshindwa masomo ya kuwa Dr, that means anayo Masters Degree ya Computer Science, kwa Kigezo hicho tu anafaa kuwa mshauri wa mradi hata kama software engineer pia ...

Labda tuangalie U-Dr inakuwaje, nafikiri sina hakika mnaweza weka sawa U-Dr unachukua muda kuupata na hata kama ukiukosa bado nafasi wapewa ya kuendelea nayo, lkn pia ikiwa amejiita Dr. bila kuwa nayo, UDSM inabidi waje clean kwani wanaruhusu waalim wao watumie u-Dr wakati bado hawajamalizia masomo? au wao hawajamuidhinisha U-Dr....Sijui ni ktk kuwekeana vigingi au la, alikuwepo Dr. Koda computa science nae imemchukua muda kuupata, lkn still wanafunzi walikuwa wakimwita Dr.

Kingine tujiulie Tanzania Tunae proffessa wa Computa science? pale UDSM miaka ya nyuma alikuwepo mmoja tu, nae alikuwa Mbulgaria, sasa kaondoka na Je Mr. Dr wa Computer Science tunao wangapi?...wanaompinga Kyaruzi kwa uwezo lazima waje na wengine wenye sifa kumzidi kyaruzi...

Smart Card..Nijuavyo Idea ya smart kadi ilikuwa yake...na kama ameshindwa kuufanikisha Mradi yapasa UDSM waje watufahamishe nini kilikwamisha, otherwise itakuwa majungu.

Pia wale wanaosema Mchanganuo ulitolewa na department ya Computa science, lazima watufahamishe ilikuwa lini na wahusika kina nani, kwani Kyaruzi pia alikuwa Department ya Computer science.Inawezekana yeye ndie alietengeneza au alikuwa akishirikiana na wenzake wote kwa pamoja.

Kuhusu Uwezo Kyaruzi anaweza kuwa nao. nafikiri kama kuhoji tuhoji mengine ya logistics za tender na ufisadi kama upo.otherwise itakuwa Majungu.
 
Naomba kuchangia kama ifuatavyo:

1. Nimesoma makala ya RAIA mwema, na kwa maoni yao Huu mradi usimamishwe na fedha ihamie ktk Kununua matrekta. kwa Billion 200, Kilimo tutakuza Mno. na hapo wananchi watakuwa na uwezo ktk mifuko yao. Tumekaa muda bila vitambulisho, lkn hatuwezi kukaa bila chakula cha uhakika, na serikali imeshatangaza Upungufu wa chakula.

Bahati mbaya hapa unazungumzia kipaumbele. Unajaribu kuonesha kuwa tunaweza kuweka kipaumbele na umuhimu kwenye kitu kingine badala ya vitambulisho, hili wenzio hawalikubali, vitambulisho ni lazima vije kwani pamoja navyo ni ulaji mzuri tu kwa kundi la watu wachache.
2. Kwa wale Wanaompinga Dr.Kyaruzi sina hakika na augument zao za kweli au la. tu-assume Kyaruzi si Dr. na ameshindwa masomo ya kuwa Dr, that means anayo Masters Degree ya Computer Science, kwa Kigezo hicho tu anafaa kuwa mshauri wa mradi hata kama software engineer pia ...

Kama yeye siyo Dr, je anajitambulisha kuwa ni Dr? Kama ndiyo basi tayari hapo lina tatizo kuhusu uaminifu, ukweli, na uwazi. Kama ameshindwa kuwa muwazi kwenye taaluma yake ni muwazi kwa mambo mengine?


Labda tuangalie U-Dr inakuwaje, nafikiri sina hakika mnaweza weka sawa U-Dr unachukua muda kuupata na hata kama ukiukosa bado nafasi wapewa ya kuendelea nayo, lkn pia ikiwa amejiita Dr. bila kuwa nayo, UDSM inabidi waje clean kwani wanaruhusu waalim wao watumie u-Dr wakati bado hawajamalizia masomo?

Yaani UDSM ndiyo wanaruhusu watu wajiite ma Dr? Nadhani kama Kyaruzi anajua yeye siyo Dr. basi ni yeye wajibu wake kusema kuwa "samahani msiniite Dr". Kuna rafiki yangu pale UDSM ni mhadhiri wa mambo ya hesabu, niliwahi kumuita Dr. (kwa sababu alipokuwa hapa US alikuwa anamalizia shahada yake) akanikatalia na kusema hakumaliza programu yake.. akasema nimuiite "Mwalimu" tu..

au wao hawajamuidhinisha U-Dr....Sijui ni ktk kuwekeana vigingi au la, alikuwepo Dr. Koda computa science nae imemchukua muda kuupata, lkn still wanafunzi walikuwa wakimwita Dr.

Yeye mwenyewe angetakiwa kukataa.

Kingine tujiulie Tanzania Tunae proffessa wa Computa science? pale UDSM miaka ya nyuma alikuwepo mmoja tu, nae alikuwa Mbulgaria, sasa kaondoka na Je Mr. Dr wa Computer Science tunao wangapi?...wanaompinga Kyaruzi kwa uwezo lazima waje na wengine wenye sifa kumzidi kyaruzi...

Hili wazo kwamba mtu mmoja ni indispensable ni mawazo ya hatari sana. Wapo Watanzania wengi tu wamesomea mambo ya Computer science.. watoe nafasi watangaze uone watakaoibuka..

Smart Card..Nijuavyo Idea ya smart kadi ilikuwa yake...na kama ameshindwa kuufanikisha Mradi yapasa UDSM waje watufahamishe nini kilikwamisha, otherwise itakuwa majungu.

Kyaruzi na wenzie ndiyo waliufanyia utafiti mradi wa smart card na ni wao wamegeuka kuwa washauri wa mradi, siwezi kushangaa kama baadaye wakaja na kampuni nyingine ya kuweka database!! Kwa sababu hakuna Watanzania wengine.
Pia wale wanaosema Mchanganuo ulitolewa na department ya Computa science, lazima watufahamishe ilikuwa lini na wahusika kina nani, kwani Kyaruzi pia alikuwa Department ya Computer science.Inawezekana yeye ndie alietengeneza au alikuwa akishirikiana na wenzake wote kwa pamoja.

Jibu langu hapo juu linahusika.

Kuhusu Uwezo Kyaruzi anaweza kuwa nao. nafikiri kama kuhoji tuhoji mengine ya logistics za tender na ufisadi kama upo.otherwise itakuwa Majungu.

Sidhani kama ni hekima kuwachagulia watu cha kuhoji, kama watu wameamua kuhoji kuhusu Kyaruzi, nadhani la maana ni kutoa majibu ya maswali yale ili mwenye kuridhika aridhike, mwenye maswali ya ziada aulize na mwenye kutoridhika basi aishie zake.
 
Naomba kuchangia kama ifuatavyo:

1. Nimesoma makala ya RAIA mwema, na kwa maoni yao Huu mradi usimamishwe na fedha ihamie ktk Kununua matrekta. kwa Billion 200, Kilimo tutakuza Mno. na hapo wananchi watakuwa na uwezo ktk mifuko yao. Tumekaa muda bila vitambulisho, lkn hatuwezi kukaa bila chakula cha uhakika, na serikali imeshatangaza Upungufu wa chakula.

2. Kwa wale Wanaompinga Dr.Kyaruzi sina hakika na augument zao za kweli au la. tu-assume Kyaruzi si Dr. na ameshindwa masomo ya kuwa Dr, that means anayo Masters Degree ya Computer Science, kwa Kigezo hicho tu anafaa kuwa mshauri wa mradi hata kama software engineer pia ...

Labda tuangalie U-Dr inakuwaje, nafikiri sina hakika mnaweza weka sawa U-Dr unachukua muda kuupata na hata kama ukiukosa bado nafasi wapewa ya kuendelea nayo, lkn pia ikiwa amejiita Dr. bila kuwa nayo, UDSM inabidi waje clean kwani wanaruhusu waalim wao watumie u-Dr wakati bado hawajamalizia masomo? au wao hawajamuidhinisha U-Dr....Sijui ni ktk kuwekeana vigingi au la, alikuwepo Dr. Koda computa science nae imemchukua muda kuupata, lkn still wanafunzi walikuwa wakimwita Dr.

Kingine tujiulie Tanzania Tunae proffessa wa Computa science? pale UDSM miaka ya nyuma alikuwepo mmoja tu, nae alikuwa Mbulgaria, sasa kaondoka na Je Mr. Dr wa Computer Science tunao wangapi?...wanaompinga Kyaruzi kwa uwezo lazima waje na wengine wenye sifa kumzidi kyaruzi...

Smart Card..Nijuavyo Idea ya smart kadi ilikuwa yake...na kama ameshindwa kuufanikisha Mradi yapasa UDSM waje watufahamishe nini kilikwamisha, otherwise itakuwa majungu.

Pia wale wanaosema Mchanganuo ulitolewa na department ya Computa science, lazima watufahamishe ilikuwa lini na wahusika kina nani, kwani Kyaruzi pia alikuwa Department ya Computer science.Inawezekana yeye ndie alietengeneza au alikuwa akishirikiana na wenzake wote kwa pamoja.

Kuhusu Uwezo Kyaruzi anaweza kuwa nao. nafikiri kama kuhoji tuhoji mengine ya logistics za tender na ufisadi kama upo.otherwise itakuwa Majungu.

Mimi ninapendekeza Jamaa Moja anaitwa Hussein, alikuwa hapo Computing Centre Miaka ya 90 , sasa Nafikiri Dr Assad anamfahamu, uzuri wa huyu jamaa si Fisadi , labda kama sasa hivi kabadilika. Na pia Tunakaribisha Majina Mengine na Sifa za hao watu.
 
Media inatakiwa ifanye kazi sana. Please editors saidieni kunusuru hii nchi. Jamii inadidimia. Na ile RIPOTI maalum ya kina Jerry Muro (ITV) inasaidiaje hapa??? Please, rescue this national and its citizens/nationals.

Hivi wandugu naomba kuuliza, hayo mabasi yaendayo kasi, sijui hewani au ardhini yakishafika pale fire... makutano ya Morogoro na Umoja wa Mataifa. hiyo kasi yake itakuwa yanaenda wapi.

Kama kuna mradi ambao naona ni wa kipuuzi ni huu... Ni heri hiyo hela itumike kuweka lami barabara zote za mitaani Dar es Salaam... Hii itafanya kila mtaa wowote ufikike na kila mtu asiene shida kuweka ka-ofisi kake kule mwananyamala.
 
Mzee... kuonyesha naelewa naomba nikupe mfano mmoja tu...

Kuna kampuni inaitwa Norconsult, imekuwa inafanya kazi ya consultation kwenye miradi mingi mikubwa ya barabara kama consultant na wakati mwingine project manager.

Sasa swali. uliwahi kusikia lini hili kampuni lina matingatinga ya kutengeneza barabara, au wapi walitengeneza barabara ya KM moja?

Hivyo nasema kuwa consultant au project managers... sio lazima uwe na uwezo wa kujenga barabara.... hivyo Kyaruzi kufeli kama constructor au implementer sio lazima ashindwe pia kwenye consultation.

Unaweza usiwe na uwezo kwa kujenga barabara kwa maana ya kwamba huna vifaa, capital n.k but certainly una uwezo in terms of brainpower wa kujenga hiyo barabara!!! Naamini Norconsult wakipewa zana wanaweza tu kujenga barabara else hawafai kuwa consultant.


Nafikiri the other way around ndiyo ingekuwa kweli. Akili ya kawaida inaniambia kuwa Consultant anatakiwa kuwa mjuvi zaidi kuliko Constructor ndio maana akawa Consultant wa Constructor. Sasa Constructor kashindwa, kesho ndiye awe Consultant mzuri wa Constructor? Atamshauri nini? Sielewi hapa!!!
 
Nimeiona kwenye Rai Leo sasa Sijui kama ni habari Mfuu or zilizo hai.
Naomba ikae hapa kwa Muda kabla ya Kuunganishwa na Thread Husika


Sasa Serikali yaanza kumchunguza Gotham
SAKATA LA VITAMBULISHO VYA TAIFA:

:: Wizara husika yaanza upekuzi
:: Uzoefu wa wakurugenzi wajaa utata

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Patrick Rutabanzibwa, amesema wizara yake inachunguza kuona uhalali wa Kampuni ya Gotham International kupewa kazi ya ushauri kwa Serikali juu ya mradi wa vitambulisho vya kitaifa.

Katika mahojiano maalumu na Rai ofisini kwake Dar es Salaam wiki hii, Rutabanzibwa alisema mambo ya msingi yanayoangaliwa ni uwezo wa kitaalamu na kifedha wa kampuni hiyo ili kuona kama inastahili kusimamia suala hilo, hasa katika hatua hii ya kutengeneza kanuni atakazotumia mzabuni atakayeshinda tenda ya kutengeneza vitambulisho hivyo.

Kampuni ya Gotham International ilipewa tenda hiyo katika mazingira ambayo yamewatia shaka watu wengi, wakihoji uwezo wa kampuni hiyo ambayo haijawahi kutengeneza kitambulisho katika nchi yoyote duniani. Wengi wanadai kampuni hiyo itakuwa ikifanya kazi hiyo kwa majaribio.

Akizungumzia hali hiyo, Katibu Mkuu Rutabanzibwa alisema kabla ya kuiidhinisha kampuni hiyo kwenye hatua inayofuata, ni lazima ajiridhishe mwenyewe kwanza ndipo amshauri waziri ambaye ndiye atapeleka mapendekezo yake Serikali Kuu.

"Kazi ninayoifanya ni ya kutaka kujiridhisha juu ya kampuni hii. Kwanza naangalia kama ana technical capacity (uwezo wa kiufundi) na financial capacity (uwezo wa kiuchumi). Tunaangalia pia kama anao staff (wafanyakazi) wenye uzoefu wa kutekeleza miradi ya aina hii. Hatutaki watu wanaokuja kujifunzia kwetu," alisema Rutabanzibwa.

Alisema kazi ya kuwaangalia watendaji wa kampuni hiyo kwa kurunzi kubwa, itaenda sambamba na kumwangalia Mwenyekiti Mtendaji wa shughuli hiyo kama anao uwezo na uzoefu wa kuongoza timu ya wataalamu katika suala hili zito na nyeti.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti huyo, Jack Steven Gotham alisema ana ubia na Kampuni ya FootPrint Africa Business Solution na kwamba kampuni yake pamoja na kampuni hii ndiyo kwa pamoja walipewa kazi na Serikali.

Hata hivyo, katika mahojiano na gazeti hili wiki mbili zilizopita, Gotham huyo huyo alisema hana ubia na kampuni yoyote isipokuwa FootPrint ilimpa mtu mmoja ambaye alikuwa na uzoefu wa kutengeneza vitambulisho kutoka nchi kadhaa za Kiafrika.

Gotham hapendi kuzungumzia kuhusu wataalamu wa ndani alio nao katika kampuni yake ingawa kumbukumbu za Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ina wakurugenzi wanne; wawili wao wakiwa wana hisa na wengine wakiwa wakurugenzi wa kuteuliwa.

Wenye hisa ni pamoja na yeye mwenyewe Jack Steven Gotham mwenye hisa 4,000 na Jesse J. G. Steven ambaye ana hisa 2,000 kati ya hisa 10,000 za kampuni hiyo. Wengine wasio na hisa ni Daniel I. Nyerere na Salum Mpugusi. Hata hivyo, utaalamu wa wakurugenzi hawa wanne hauonyeshwi popote kwani hata search engine ya Google, haimtambui yeyote kati yao.

Ni kumbukumbu hizo za BRELA zinazoonyesha kuwa ofisi kuu ya kampuni hiyo ipo Mtaa wa Msichoke, Nyumba Namba 13, Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam. Nyumba hiyo ndiyo inatambuliwa kisheria na kwa mujibu wa kifungu cha 92 cha Sheria ya Makampuni (Cap 212). Tangu kampuni hiyo isajiliwe mwaka 2001, haijafanya marejesho ya hesabu zilizokaguliwa na marejesho ya kawaida ya mwisho yalifanywa miaka miwili iliyopita.

Akizungumzia mazingira ambayo kampuni hiyo ilipewa tenda, Katibu Mkuu Rutabanzibwa ambaye ameingia wizarani hapo kutokana na mabadiliko ya makatibu wakuu yaliyofanywa mwishoni mwa mwaka jana, alisema anataka kujiridhisha kwanza kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya kuishauri Serikali chochote.

Alisema kimsingi, ni jambo gumu kupata taarifa katika wizara hiyo lakini bado anaendelea kupekua nyaraka mbalimbali kuangalia uhalali wa Kampuni ya Gotham kupata kazi hiyo.

"Nikisema naangalia uhalali, simaanishi nimewaharamisha. Mimi ni mgeni katika ofisi hii. Lakini kelele nyingi zinapigwa zikituonya juu ya kampuni hii. Hatuwezi kunyamaza. Nakuhakikishia kila kelele inayopigwa, sisi tunaifanyia kazi. "Habari zinazoandikwa na vyombo vya habari ni taarifa muhimu sana kwetu, kwa hiyo baada ya kujumlisha mambo hayo na kuchambua ndipo nitakapoweza kuwa katika nafasi nzuri ya kumshauri waziri hatua inayofuata," alisema.

Alipoulizwa kama hashangazwi na hatua ya Idara ya Usalama wa Taifa kuwatahadharisha Watanzania na mtu huyo lakini katika mwezi huo huo wizara yake ikampatia kazi nyeti kama hiyo, Rutabanzibwa alisema hilo ni mojawapo ya mambo makubwa anayofanyia kazi. "Huwezi kupuuza taarifa nyeti kama hii. Kwamba Julai 14 kitengo muhimu cha usalama kinatoa taarifa za tahadhari na miezi miwili baadaye serikali inasaini naye mkataba. Nitawatafuta GSO watueleze. Tutataka kuona tangazo lao linatuathiri vipi. Ni sehemu ya inquiry (uchunguzi) yetu. Siwezi kwenda kumshauri waziri wangu bila ya kuwa na hili," alisema.

Akizungumzia juu ya Kampuni ya Gotham kuwa au kutokuwa na mkataba, Rutabanzibwa alisema kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo wizarani kwake, Gotham ana Memorandum of Understanding aliyoingia kati yake na Wizara ya Mambo ya Ndani hapo Novemba 10, 2004. Na kwa mujibu wa kumbukumbu hizo Memorandum hiyo inaeleza kuwa kampuni hiyo itaisaidia Serikali kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na baada ya hapo itafanya menejimenti ya mradi.

Alipoulizwa kama kuna tofauti yoyote kati ya Memorandam of Understanding na mkataba, alisema hilo ni suala la kisheria.

Rai ilitaka kupata ufafanuzi wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mmoja aliyebobea juu ya mambo ya mikataba. Mwanasheria hiyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake kutajwa gazetini, alisema katika masuala ya mikataba na majadiliano ya kimataifa (international negotiations), ukimtuma mtu ambaye hana madaraka ya juu, yale mambo yanayozungumziwa mpaka pale anapofungia, inaitwa memorandum of understanding.

"It is not meant to bind (haijafungwa), maana yake ni kwamba hapa tumeshafikia hatua nzuri na haturudi nyuma. Lakini hakuna jambo linaloweza kutekelezeka katika hatua hiyo mpaka umalize kitu kizima, uingie katika mkataba," alisema mwanasheria huyo na kuongeza:

"Lakini kuna dhana nyingine ya MoA imo katika mikataba ya kawaida ambayo lengo lake ni kutengeneza exclusivity (upekee). Mfano mzuri ni kwamba kama tumeshaingia katika majadiliano na kwamba unipe eneo fulani nichimbe mafuta. Wakati mnahangaika huyo anatafuta fedha, mnatengeneza memorandum of understanding kwamba asipewe mtu mwingine. Kwa mfano wakati it is still valid, huwezi kwenda kwa mtu mwingine."

Alifafanua kwamba kusema Memorandum of Understanding ni mkataba au si mkataba, inategemea dhamira na wale walioitengeneza walivyoandika.

"Na katika suala hili, yapo mambo mengi ya kuangalia. Inategemea walioiandika walikuwa na makubaliano gani. Kwa hiyo huwezi kusema si contract au ni contract. Wakati mwingine ukienda mahakamani na memorandum of understanding, unaweza ufike mahali mahakama ikakwambia hii ni agreement kwa sababu mahakama haiangalii jina, bali inaangalia vifungu vyake. Kama mmejipangia majukumu ya kufanya, mahakama inaweza kusema ni mkataba. Mahakama itaangalia maudhui yake na wala si jina lake," alisema.

Alisema hili suala linaweza lisiwe kosa kama hakuna sheria inayoelekeza vingine. "Kwa mfano kama mimi na wewe tunaingia katika makubaliano ambayo hakuna sheria nyingine inayotulazimisha kuingia katika taratibu nyingine, memorandum of understanding ni mkataba kama inaonyesha wajibu na majukumu ya kila mmoja ya kufanya." Hata hivyo, mwanasheria huyo alisema hili linaweza kuwa kosa iwapo jambo hilo lipo chini ya sheria fulani. "Katika suala hili la Kampuni ya Gotham na Serikali, ipo Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004. Hii imetoa ufafanuzi wa nini kifanyike. Lakini pia sheria hii inakataza mtu mmoja kupewa kazi bila kushindanishwa, kwa hiyo hili si suala la kusema ni sahihi au si sahihi.

"Linahitaji umakini zaidi na hasa kwa kuwa mambo haya yamepita mikononi mwa watu wengi, na yametembea katika korido za wizara nyingi," alisema.

Rai imefanikiwa kupata Memorandum of Understanding hiyo na sehemu yake inasema: "The Ministry of Home Affairs on behalf ot the United Republic of Tanzania with offices in Dar es Salaam (the GoT) entered into an agreement with FootPrint Africa Business Solutions Ltd and Gotham International Ltd with offices in Dar es Salaam (the Consortium) and the parties established a Memorandum of Understanding (MoU) in undertaking project management consultancy for the establishment and implementation of the National Identification and Registration of the Persons (NIRP) system in the United Republic of Tanzania to assist the GoT to solicit funds for implementation and establishment of a National Identification and Registration System.

The parties, held discussions in Dar es Salaam from November 13th to 18th 2004 with a view to determine the general financial and operational commitments towards smooth execution of the National Identity Card Program in the United Republic of Tanzania for the period of 2004 through 20014 for the purpose of implementing the National Identification and Registration System, it was agreed that the consortium will assume the Role of the Project Management Consultancy," sehemu ya MoU hiyo inasema.

Hata hivyo, kinachoshangaza ni kwamba hayo yakifanyika, Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 inayoelekeza utaratibu wa kutoa huduma serikalini na kwenye mashirika yake kwa kupitia zabuni za ushindani ilishapitishwa na Bunge.

Kwa upande wake, Rutabanzibwa alisema mazingira ya kutolewa kwa Memorandum of Understanding, ni moja kati ya mambo anayoyafanyia uchunguzi ili kujiridhisha.

"Wapo wanaosema hakushindanishwa na yeyote. Tunaangalia kama ilikuwa sahihi kufanya single sourcing."

Habari za jinsi Kampuni ya Gotham ilivyopata kazi hiyo ni nyingi na nyingine zikihusisha watendaji katika sekta nyeti za nchi hii. Mmoja kati ya watu wanaotajwa tajwa, alijitokeza katika mkutano wa Gotham wa mwishoni mwa wiki akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa. Habari zinapasha kuwa kwa kuwa Gotham hana utaalamu wowote na masuala ya vitambulisho, alilazimika kuwatafuta watu wa kumbeba na mmojawapo ni yule aliyekuwa naye kwenye mkutano na waandishi wa habari, ambaye kwa nafasi yake nyeti serikalini na kazi anazofanya za kumkutanisha na watu wengi wa nje, alimtambulisha Gotham kwa kampuni moja ya Afrika Kusini iliyokuwa ikiitwa Intrinsic na kwa sasa inaitwa Business Connexion BCX.

BXC ni wasambazaji wa bidhaa na waliamua kwa makusudi kufadhili utafiti wa ambao ripoti kadhaa zinaeleza kuwa ni mkusanyiko wa ripoti kadhaa ikiwamo ya COWI Consult, na ile ya Kitengo cha Biashara cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Economic Research Bureau) pamoja na vipande kutoka kwenye mtandao wa kompyuta (internet) na kuviwasilisha serikalini kama feasibility study yao.

Na katika kipindi chote hicho, Jack Gotham amejaribu kuwa karibu mno na mawaziri kadhaa pamoja na makatibu wakuu wakimpa taarifa nyeti za Serikali kuhusu mradi huu.

Habari zinaeleza kuwa katika kipindi hicho, baadhi ya watendaji serikalini walio karibu na kampuni hii ya Gotham International walifanya safari kadhaa kwenda Afrika Kusini, Malaysia na Singapore wakitembelea baadhi ya kampuni zinazotengeneza vitambulisho ambazo nyingine zinadaiwa kuwamo kati ya zile sita ambazo zimeteuliwa kwa ajili ya ushindani wa mwisho.

Baadhi ya vivuli vya vitambulisho kutoka katika kampuni hizo vilipokewa na Serikali bila swali lolote na vimetumiwa kama sehemu ya vielelezo kwenye Evaluation Report and Recommendations for Prequalification of Applicants ukurasa wa sita wa Appendix C: Training Materials.

Habari zaidi zinaeleza kuwa masharti yaliyotengenezwa yalilenga kuziengua baadhi ya kampuni ambazo zingekuwa tishio. Kwa mfano habari hizo zinaeleza kuwa kitendo cha kuchagua teknolojia ya Smart Card iliyopendekezwa na Gotham na kukubaliwa na Serikali, ndicho kimemfanya Mpigachapa Mkuu wa Serikali kushindwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho, ingawa yeye alikuwa na gharama ya chini ambayo inaendana na hali ya uchumi wa nchi kwa sasa.


© New
Je Ziara ya Mama Ikulu Inahusiana na Hili????
 
Duh!!! Njemba ilishindwa mradi wa smart card pale UDSM sasa inapewa kazi ya kusimamia mradi wa smart card wa nchi nzima!!!! Ama kweli mafisadi wameiteka nyara nchi!!!!
 
BAK, unajua muda wao ndio unazidi kuwapa mkono, soon.... very soon wote wataonja joto ya jiwe!!
 
Natamani kufa sema basi tu mimi ni kifo!
1. Dr. J.J.Kyaruzi naye ni mtaalamu wa smart card!!??Do you know PhD yake aliyofeli ilikuwa ya nini?? Alikuwa anafanya PhD ya smart card kwa ufadhili wa UDSM-amefeli masomo(hakumaliza PhD),amefeli mradi wa smartcard udsm,amefeli kufanya research TIC....still u want him??
2. Walishirikiana na maimu kutengeneza mradi wa MaIT experts pale UTUMISHI ambao hawakuleta chochote serikalini--Uliza Wizara ya Sayansi,Elimu,Mambo ya Nje,Sheria,Afya nk watakuambia hao experts wa mradi wa Maimu/Kyaruzi walifanya nini??
3. Background mbaya ya Computer Science/IT aliyonayo kyaruzi -alisoma Bsc Gen Science, Msc GS ......do you think ataweza mambo,wapo watz kibao wana elimu na uzoefu wa hayo mambo--Bank nyingi hapo homu zina smartcard technology je hao wanaoendesha hiyo tech ni wazungu kwenye bank zote hizooo?/
4.Kyaruzi was a classmate of my fiancee ktk PhD,hana uwezo we know him well na hata hizo ambitions zake - mradi wa udsm for instance,alikuwa hajui hata technologia gani atumiea..jiulize hivi smartcard unaweza kutumia ms sql 1997
5.Maimu sijui alifikiria nini kujihusisha na huyu jamaa kwa sababu vile nafahamu wao ni marafiki sana na maimu ndio alimpigia cross ya kwenda TIC-maimu akiwa utumishi so ubishi wa baadhi kuwa hawana urafiki waulizeni wale vijana tuliowapa kazi za IT experts watawaaambia,nikirudi home tanzania nitasema ukweli wote siku moja
6. Kyaruzi alianzisha au kufufua African Virtula University pale mlimani ambayo aliifanya kama ng'ombe wake wa maziwa kulikuwa na certificate zinatolewa pale kama njugu(UDSM hawakuapprove-wabishe nitoe minutes) akishirikiana na vijana wake -kwakweli huyo ni mtu dubious sana kupita tapeli wetu hapa marekani aliyechukua mahela bank
 
Kumbe hii ishu ilianzia huku.
Duuh bonge la kaburi
Pamoja na maelezo hayo yote kuhusiana na mapungufu yaliyooneka, bado mradi uliendelea, pesa zikatolewa na kuliwa, na mradi ukawa Hoi bin Taaban. Mwana ndo huyo tuliyemlea akatuvuruga tukimwangalia tu, sasa tunabaki kulia kama wajukuu.
 
Binafisi nilipoona Kyaruzi yumo ndani ya Gothamu nilishangaa ndio nikajua kumbe ndio maana wamepata hiyo kazi.

Kifupi ni kuwa, huwezi kumutenganisha Maimu na Kyaruzi. Wanafahamiana vizuri na wameshashiriki kwenye madudu mengi wakati Maimu akiwa pale Utumishi.

Hawa jamaa ni "majambazi" wa kutupwa na binafsi sijui serikali inafanyaje kazi na watu hawa.
Kwa kweli imenishitua sana kumbe Kyaruzi ndio Gotham.

Kwa kweli NCHI hii imekwenda kubaya sana.

KYARUZI=GOTHAM=MAIMU=KYARUZI
Loh imetimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu baba enock,
kama mdanganyika nimelifwatilia sana hili swala mpaka kufikia kwenda kujifanya mwandishi na kuzama ndani ya hiyo press confrence waliotisha hao kina gotham,kudhibitisha,yule kubenea aliingia na islam wa thisday pamoja,yule lina denny wa channel10 aliondoka mapema,nilipata hadi handout ya presentation,nilistuka kumskia sarah mossi sijui wa RAI kusema,kwamba aliwaambia wenzake kuhusu ukweli wa gotham wao wakasema tumbamize tu anajifanya mjanja!!kama kuna mwandishi humu ndani aliudhuria atakumbuka hilo,mlangoni kulikuwa na wakribishaji wawili mmoja mrefu mmoja mfupi(sijui wa hoteli au wa gotham)

sasa,mie hapo juu niona ni kuchafuana tu,amna swali la msingi,mara wizi mtupu(hii ishakuwa komedi)mara kyarusi sio DR( halafu?) swala hapa ni vitambulisho vya utaifa hili jamvi ni juu zaidi ya mtu yeyote hapa,mie naweza kuscan page mbili za hiyo presentation ya hao kina gotham iliyosimama(inajieleza) je wewe na hizo shtuma zako unaweza kuthibitisha au habari kutoka mtu wa tatu?

hapo nyuma nilisema tuache kupotoshana,hilo naona kwako wewe imekuwa ngumu umechukuwa hili personal(eti mie mzalendo kweli?) sasa uoni hapo unataka tuache mada tuanze kujadiliana?

basi wewe ni mzalendo zaidi yangu maradufu,je umeweza kupata usingizi?
Aisee. Mkuu bado upo? Karibu utuambie mtazamo wako mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi imetafunwa sana hii kama haina wenye macho. Hivi wananchi wanaokatwa hizo kodi wanaonewa huruma kweli? Hao walio kwenye hizo nafasi tena wameaminiwa ndiyo wanakuwa vipofu hivyo na kufunika kombe hadi pesa zikapigwa ile mbaya? Hadi leo JPM na Kangi Lugola waje kufukua makaburi na kubembeleza hela zirejeshwe? Hadi akina Modestus Kipilimba waende kule NIDA kusafisha uchafu na kufukuza wafanyakazi kwani walikuwa wanakaa tu bila kazi tena wameajiriwa kindugu? This is too much ....Mother Tanzania anabakwa mno bila huruma na wadanganyika hatujui ufumbuzi na ukombozi utapatikana lini hata kwa jambo lililo uchi kama hili la Gotham na J.J. Kyaruzi, Maimu na NIDA yenye aibu. Tunashangaa NIDA haina hela walifanya kazi kupiga wananchi kwa kujitolea na kuazima mashine za kadi za NEC na hizo kadi za vitambulisho vya taifa wananchi hatujavipata!!! Asanteni wadau kwa kufukua kaburi hili lenye thamani ya mabilioni ya Dollars.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom