Mkurugenzi abanwa kwa kugoma kumlipia Makamu wa Rais malazi

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,919
31,161
SAKATA la halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya baada ya aliyekuwa kaimu mkurugenzi wakati wa ziara hiyo, Majid Myao kutakiwa kutoa maelezo.

Myao aliitwa na mkuu wa wilaya ya Karatu, Mathew Sedoyeka hivi karibuni ili akatoe maelezo juu ya suala hilo hasa kutokana na halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja na chakula kwa ujumbe huo, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya maandishi ya Myao, yaliyopo katika barua yake ya Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.

Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.

“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,”alieleza Myao.

Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa jimbo la Karatu, Dk Wilbroad Slaa alisema ni halali kwani walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo na aliomba mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo asiwajibishwe kwa suala hilo.

Source:Mwananchi

Pongezi madiwani wa Karatu kwa kukataa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.Hizi ziara za Viongozi wa kitaifa zinapaswa kutengewa bajeti na ofisi zao na si kutumia fedha za halmashauri kwa ziara za viongozi wa kitaifa.
 
Hii safi!!

Yaani malazi na chakula siku 1 shs millioni 2?

Hii pesa sii bora ikajenga madarasa??

Kumbe hawa viongozi huzunguka mikoani kila siku kwa gharama za nani??

Hizi ziara zina manufaa gani?

Kwani Karatu ndo waliomwita Shein akatembee huko?
 
Hii imekaa vizuri.. :D :D

Hii ya tabia ya mtu anachukua per diem 'inaitunza' halafu anajitungia safari bila kuombwa mawilayani na ikome.
 
Hili jambo limekaa kisiasa zaidi kuliko kiutendaji. Ila inanishangaza sana kuona gharama za Makamu wa Raisi kula na kulala zingaramiwe na Halmashauri anayotembelea. Haya si ndio matumizi ya ofisi ya makamu wa raisi?
 
sakata la halmashauri ya karatu, kugomea kulipia malazi ya makamu wa rais, dk ali mohamed shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya baada ya aliyekuwa kaimu mkurugenzi wakati wa ziara hiyo, majid myao kutakiwa kutoa maelezo.

Myao aliitwa na mkuu wa wilaya ya karatu, mathew sedoyeka hivi karibuni ili akatoe maelezo juu ya suala hilo hasa kutokana na halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha sh2milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja na chakula kwa ujumbe huo, katika hoteli ya bougain villea ya mjini karatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya maandishi ya myao, yaliyopo katika barua yake ya machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.

Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.

“kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,”alieleza myao.

Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa jimbo la karatu, dk wilbroad slaa alisema ni halali kwani walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo na aliomba mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo asiwajibishwe kwa suala hilo.

Source:mwananchi

pongezi madiwani wa karatu kwa kukataa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.hizi ziara za viongozi wa kitaifa zinapaswa kutengewa bajeti na ofisi zao na si kutumia fedha za halmashauri kwa ziara za viongozi wa kitaifa.
very good!
 
Leo nafunga bar kwa kitengo hiki. Good move, i love it. Kweli Dr. Slaa ni mzalendo na Baba wa Taifa lakini wa pili
 
endapo mkuu kama huyo anatembelea sehemu........je utaratibu wa matumizi yake ukoje?
 
Afadhali amekataa maana baadaye yangekuja kumtokea kama yale ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kuangua kilio katika Kikao cha Baraza la Madiwani; kisa eti mkuu wa mkoa hamwelewi anaposema fedha za ujenzi wa shule zilitumika kugharamia ziara za Vigogo wa serikali kuu. Jamani kufanya kazi Halmashauri za Wilaya inahitaji moyo kwelikweli
 
endapo mkuu kama huyo anatembelea sehemu........je utaratibu wa matumizi yake ukoje?

Hapo siyo suala la utaratibu bali ni bajeti na uwepo wa fedha. Kwa wakati tulionao Tanzania tunatumia mfumo wa cash budget kwa maana kwamba ilishughuli itekelezwe lazima iwe ilishatengewa na kuidhinishiwa bajeti yake; halafu wakati wa kuitekeleza lazima kuhakikisha kuwe fedha ya kuitekeleza ipo. Makam wa Rais ana wizara yake ambayo kimsingi ndiyo yenye wajibu wa kumwandalia bajeti ya ziara zake kwani hao ndo wanafahamu atakuwa na ziara ngapi kwa mwaka.
 
Hapo dawa ni sera ya majimbo tu ama sivyo hao maofisa wa karatu watatishiwa mpaka wakome, au watahamishwa kabisa vituo vyao vya kazi. Haiwezekani mkurugenzi wa wilaya akateuliwa na serikali kuu badala ya serikali za mitaa ambayo ndio anaitumikia. Sasa anawajibika kwa nani, kwa Kikwete au kwa Karatu. Hata hao wakuu wa wilaya nao, ni vibaraka tu wa Rais huko wilayani. Sera ya majimbo itaondoa huu ukoloni wa serikali kuu kuongoza kwa kutumia vibaraka wanaojiita wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa

SM
 
Hapo siyo suala la utaratibu bali ni bajeti na uwepo wa fedha. Kwa wakati tulionao Tanzania tunatumia mfumo wa cash budget kwa maana kwamba ilishughuli itekelezwe lazima iwe ilishatengewa na kuidhinishiwa bajeti yake; halafu wakati wa kuitekeleza lazima kuhakikisha kuwe fedha ya kuitekeleza ipo. Makam wa Rais ana wizara yake ambayo kimsingi ndiyo yenye wajibu wa kumwandalia bajeti ya ziara zake kwani hao ndo wanafahamu atakuwa na ziara ngapi kwa mwaka.

Hilo hapo juu (highlighted in red) may be ndio jibu la swali langu......sikuuliza kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa bajeti ndani ya halmashauri na matumizi yake.......taratibu Mkuu!
 
SAKATA la halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya baada ya aliyekuwa kaimu mkurugenzi wakati wa ziara hiyo, Majid Myao kutakiwa kutoa maelezo.

Myao aliitwa na mkuu wa wilaya ya Karatu, Mathew Sedoyeka hivi karibuni ili akatoe maelezo juu ya suala hilo hasa kutokana na halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja na chakula kwa ujumbe huo, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya maandishi ya Myao, yaliyopo katika barua yake ya Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.

Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.

“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,”alieleza Myao.

Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa jimbo la Karatu, Dk Wilbroad Slaa alisema ni halali kwani walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo na aliomba mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo asiwajibishwe kwa suala hilo.

Source:Mwananchi

Pongezi madiwani wa Karatu kwa kukataa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.Hizi ziara za Viongozi wa kitaifa zinapaswa kutengewa bajeti na ofisi zao na si kutumia fedha za halmashauri kwa ziara za viongozi wa kitaifa.
Halmashauri kama 40 zingeongozwa na CHADEMA pengine maendeleo yangeonekana katika nchi hii, maana ni rahisi hata zile zinazoendeshwa kibwegebwege zingeiga mifano hai hata kwa kulazimishwa.
 
Hii ni safi ya Mwaka,
Hongereni sana karatu. Watumishi wa ngazi za juu wa serikali wamekuwa wezi na wadanganyifu kwa muda mrefu. Wamekuwa wakilipwa masurufu yao wanaposafiri (per deims) kabla ya safari lakini wanapofika wilayani wanashinikiza wilaya kulipia tena. Huu ni ubakaji wa haki za wanyonge kwa kiasi cha kutisha, hebu fikirini uanzie ziara ya rais, m/rais, waziri mkuu, mawaziri, mkuu wa mkoa na ghasia nyingine zote za viongozi wakuu, wote hawa jumbe zao zinakomba fedha yote ya maendeleo ya wilaya husika.

Aibu kubwa kabisa kwa serikali, kutenga fedha kwa halmashauri kwa mkono wa kulia na kuwaibia kwa mkono wa kushoto!
 
siku moja m2 akikaa wiki duh maumivu kwa wilaya husika inauma sana.
Safi sana madiwani kwa uamuzi wa busara.
 
Saafi sana ndugu Mkurugenzi, fuata sheria tu. Kama hawaitaki sheria hiyo waende kuibadilisha. By the way, kama tukifuata monetary value ya ziara ya Vice Pres. ni hasara tupu, labda alikuja akakagua shamba la mahindi na kufungua tawi la CCM na kuondoka, Hajaja na mbolea, hajaja na mabati ya nyumba za walimu, hajaleta umeme, hajaleta mkandarasi wa barabara, labda kusumbua watu tu kuja kumpokea na kusimamisha watoto wa shule siku hiyo kumuimbia kwaya. What a waste !!
 
Aisee huyu acting DED amefanya kitendo cha kupigiwa mfano. Maana bila kufuata sheria hakuna haki. Lakini pia ile Halmashauri iko chini ya CHADEMA so madiwani hawana cha kupoteza hivyo wametekeleza majukumu yao kwa kutoidhinisha matumizi ambayo hayapo kwenye budget yao. Inabidi kuwe na halmashauri nyingi zaidi ili iwe kawaida kwa hawa jamaa wanapotembelea huko wawe wakwenda kwa budget zao.
 
Mathew Sedoyeka anadhani Majid Myao amesahau yaliomtokea Elly MlakiKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wlaya ya Kishapu, Elly Mlaki, ameangua kilio ndani ya kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, baada ya kushindwa kujibu swali la mmoja wa madiwani.

Tukio hilo lilitokea jana mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambamo kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dokta Yohana Balele, kilifanyikia.

Hatua ya Mkurugenzi huyo kuangua kilio, Ilikuja baada ya Diwani wa Magalata, Albert Kapongo, kumuliza swali lililohusu jinsi ofisi yake ilivyotumia Sh 120 milioni, kununulia lori la Idara ya Elimu.

Hata hivyo mkurugenzi huyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu swali hilo, jambo lililomsukuma Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,kuingilia kati na kutaka ufafanuzi wa kina juu ya swali hilo.

"Ndugu mkurugenzi naomba kupata ufafanuzi wa matumizi ya Sh120 milioni zilizotumika kununulia lori la Idara ya Elimu,"alisema.

Akijibu swali hilo mkurugenzi huyo alidai kuwa lori hilo halijanunuliwa na kwamba fedha hizo zimetumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mandalizi ya ziara mbalimbali za viongozi wa kitaifa.

"Nataka utoe ufafanuzi wa jinsi fedha hizo zilivyotumika," ling'aka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, hatua iliyomlazimisha mkurugenzi huyo kuendelea kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu fedha hizo.

Alidai Sh 2 milioni katika kuwa fedha hizo zilitumika kununulia kapeti la rais na Sh 5 milioni, zilitumika kuwalipa walimu tarajali.

Hata hivyo mkuu wa mkoa alizidi kumbana zaidi mkurugenzi kuhusu fedha ambazo kimsingi, hakizikupaswa kutumika kwa shughuli nyingine.

"Hizo fedha zingine zilizobaki zikowapi,"aliuliza mkuu wa mkoa.

Kufuatia kubanwa kwa maswali hayo, mkurugenzi huyo aliaanza taratibu kutoa kwikwi na baadaye kuangua kilio hadharani kwa sauti kubwa na kuwafanya madiwani kushikwa na butwaa.

Hali hiyo ilipoendelea mkuu wa mkoa alimwomba mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuahirisha kikao hicho kwa vile haikuwa rahisi tena kuendelea nacho wakati kuna kilio

Hongera sana Majid japo lazima utolewe kafara na Sirikali ukizingatia hapo STRONGHOLD ya CHADEMA!!!:confused::confused::confused:
 
Yaa guys

i would first like to say im happy that i have joined this wonderful forum.
Ningependa pia kuwapa moyo zaidi wanajamii wajitume zaidi kupigania nchi yao kwa namna zote, tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni hiki kizazi cha rushwa, kizazi chenye madhara ya ukoloni. But if we put more pressure like this atlast we will reach where we want.

Personally nimefurahishwa na kitendo cha madiwani hawa si tu kwa sababu wamemkatalia makamu wa raisi bali kwa kwa kuwa na ujasiri unaotakiwa wa kiutendani na uongozi wa kisheria walioufanya.
 
Hongereni sana kama wizara husika(makamu wa rais)wametia ndani au ndio kawaida yao...sasa limesanuka...wana bajeti wale kama wanawatishaa halmashaurii ili walipe wao wana wakilisha risiti fake....na badoo...wale wa JK ndio kabisaaaaa.......wakirudi wanahaha mjini kutengeneza risiti fake....
 
Back
Top Bottom