Mkureugenzi Wa AICC asakwa na polisi kwa tuhuma za wizi

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Katika pita pita zangu hususan katika kituo cha mikutano cha Aicc nilikutana na njagu wawili waliovalia kiraia .Kwa kawaida kunapokuwa na events kama mkutano ulioisha wa AFDB usalama huwekwa mbele. kwa hiyo niliona kawaida tu. Hata hivyo baada ya kusalimiana na jamaaa wakanitonya kuwa kuna mtu wanamsaka. kama kawaida nichokonoa nipate details zaidi na ndipo waknitonya eti Mkuu wa Idara ya Miradi na nyumba wa Aicc anasakwa kwa wizi wa projector screen kubwa ambayo ilikodishwa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Afdb uiliokuwa unafanyika eneo maalum la nje kwenye hema.

Kuibiwa kwa screen hiyo kulilifedhehesha taifa baada ya waangalizi wa afdb kujua hilo na kulalamika kuwa screen hiyo ilikuwa maalaum sana kwa mkutano huo na kushangazwa namna ilivyotoweka.

Kaitka uchnguzi imeonekana bwana Ndosi anahusika kwani baada ya mkutano na baada ya amri ya kumsaka mwizi kutolewa Ndosi ambaye ni mkurugenzi wa Idara amekuwa suspect number one, kwa hiyo anatakiwa atiwe nguvuni na ikithibishwa ashitakiwe mahakamani.

MY TAKE. Kama vingozi wakuu wa taasisi kama hizi wanajihusihsa na udokozi wa aina hii, wanaaminiwaje? Inatia kichefu chefu , kweli magamba hayawezi kuacha wizi duh. CAG kazi kwako , mulika mwizi.

Source mm mwenyewe , unaweza kucrosscheck na RPC ARUSHA.
 
Hakuna shida atashikwa afu watalindana atapona. Tabu itakuja kwa ndugu zangu walinzi na walomsaidia kubeba.

Utabisha sababu ni mapema mno ila tutarudi hapa baada ya yeye kukamatwa na story itakuwa the same
 
Katika pita pita zangu hususan katika kituo cha mikutano cha Aicc nilikutana na njagu wawili waliovalia kiraia .Kwa kawaida kunapokuwa na events kama mkutano ulioisha wa AFDB usalama huwekwa mbele. kwa hiyo niliona kawaida tu. Hata hivyo baada ya kusalimiana na jamaaa wakanitonya kuwa kuna mtu wanamsaka. kama kawaida nichokonoa nipate details zaidi na ndipo waknitonya eti Mkuu wa Idara ya Miradi na nyumba wa Aicc anasakwa kwa wizi wa projector screen kubwa ambayo ilikodishwa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Afdb uiliokuwa unafanyika eneo maalum la nje kwenye hema.

Kuibiwa kwa screen hiyo kulilifedhehesha taifa baada ya waangalizi wa afdb kujua hilo na kulalamika kuwa screen hiyo ilikuwa maalaum sana kwa mkutano huo na kushangazwa namna ilivyotoweka.

Kaitka uchnguzi imeonekana bwana Ndosi anahusika kwani baada ya mkutano na baada ya amri ya kumsaka mwizi kutolewa Ndosi ambaye ni mkurugenzi wa Idara amekuwa suspect number one, kwa hiyo anatakiwa atiwe nguvuni na ikithibishwa ashitakiwe mahakamani.

MY TAKE. Kama vingozi wakuu wa taasisi kama hizi wanajihusihsa na udokozi wa aina hii, wanaaminiwaje? Inatia kichefu chefu , kweli magamba hayawezi kuacha wizi duh. CAG kazi kwako , mulika mwizi.

Source mm mwenyewe , unaweza kucrosscheck na RPC ARUSHA.

Nimepata tetesi kwamba huyo mheshimiwa ni mdogo wa Mbuge wa Bahi baba mmoja tumbo mbalimbali
 
hii taarifa ni ya kishabiki sana.mkurugenzi wa aicc ni ndg elishilia kaaya.
 
Hv kweli ataaminiwa nani

Nchi hii ndani ya utawala wa

JK? Wanakuwa wezi mpaka wao kwa wao?
Hebu tusubieni na tuone watafikishana wapi!
 
walidai lema ndiye mvunjifu wa amani, je huyo kiongozi wao na lema nani anayetia aibu mkoa na nchi? Mkutano ni wa dunia ila ulikuwa mahususi kwa afrika, je waandaji watamuelewaje mzee wa mipasho? Anajisifia watu wa arusha wamewapokea wageni vizuri, alaaa kumbe kumwibia mwenzako ni kitu kizuri!
 
Edit kichwa cha habari manake kimekaa kishigongoshigongo hivi! Mkurugenzi wa AICC (Elishilia Kaaya) sio huyo 'Mkuu wa Miradi' unaemuongelea.
 
Ni kweli sio Ceo wa AICC bali ni mmoja wa Wakurugenzi wa Aicc ..Paul Ndosi .aliwahi kufanya kazi TBA. Kiswahili wakati mwingine ni kizuri , na mwingine ni utata. sorry
 
Hakuna Mtanzania aliye safi ni fursa za kupata nafasi ya kufanya/kuchukua kitu tunakosa.
 
Huyu bwana anaitwa Ndossa na siyo Ndosi.Mnashangaa hiyo?Jamaa amefanya shirika kama shamba la bibi.Vifaa vyote vya ujenzi ni mali yake.Huyu mzee anachukua kila kitu anapeleka nyumbani badala ya godown ambayo ni sehemu maalum
vinapohifadhiwa.Inatakiwa shirika hili lichunguzwe la sivyo litafilisiwa na huyu mtu.
 
Back
Top Bottom