Mkulo na CCM kama ninyi ni wakweli kwamba mnataka kubana matumizi tunaomba at least tuone hili.

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Haingii akili nchi maskini kama hii inayotegemea ufadhili wa wazungu kiasi hiki kuona viongozi wake wanasafiri kwenye madaraja ya biashara - business class na ati wengine first class... utafikiri sisi tuko level moja na akina Bill Gate.

Kwa umaskini wetu tungependa wasafiri PM, Spika, Rais, Makamu! The rest economy class. Mtoto wa mkulima alishasema hatuwezi kufa kwa kufanya hivi. au sio.

Kama mko makini tuone hili haingii akili anayekufadhili anasafiri economy class na anayefadhiliwa anasafiria business class.

Nawasilisha.

Kasheshe
 
makosa yaliyofanyika ni ya ki sera zaidi kuliko ufadhili wa wazungu nayo ni kuwa na open ended spending policy. sera zetu hazina incentive
yeyote kwa kubana matumizi mfano mdogo leo hii ukimpa kiongozi yeyote zawadi ya dola 4000 kwenda washington dc kutembea kwa siku 2
unafikiri mheshimiwa atapanda daraja gani ?? obvious atapanda economy ili abakize hapo visenti ili ajiwekee akiba kwenye account akirudi
nyumbani kwa ajili ya matumizi yake mengine binafsi. wizara ilibidi ziendeshwe zikiwa limited trips za kwenda nje na limited amount of money
za kutumia wakiwa nje. mfano unaweza kusema waziri inabidi usafiri kwenda europe au america mara 3 kwa mwaka na spending yako ktk
trip hizi tatu hisizidi dola kadhaa kwahiyo hapo utamfanya waziri asafiri kwa trip ambazo ni muhimu tu na kutumia pesa ktk vitu muhimu kwa
sababu ya spending cap uliyomwekea.
 
Wengi huzidisha siku ili wapate fedha za ziada kama per diem. Yaani safari ya siku 2 mtu anakaa 5 days. Kwa nini mtu anaposafiri nje ubalozi wa Tanzania katika nchi husika uumtafutie hotel na malazi kwa siku zote
Then idara au wizara husika ilipe bills thru ubalozi. Hii itapunguza safari za nje kwa 60% kwani safari nyingi hazina maslahi kwa taifa bali kwa wahusika binafsi
 
Back
Top Bottom