Mkulo azitamani fedha za Watanzania walio nje

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Mkulo azitamani fedha za Watanzania walio nje

na Mwandishi Wetu, Arusha
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, ameonekana kuzitamani fedha za Watanzania walio nje na kuiagiza mifuko ya hifadhi za jamii nchini kuweka utaratibu maalumu utakaoiwezesha kunufaika na fedha hizo.

Akifungua mkutano wa 18 wa mwaka wa wanachama wa PPF mjini hapa juzi, Mkulo alisema kuwa kwa jumla, Waafrika walio nje ya bara hili, huingiza kiasi cha dola za Marekani bilioni 12 kila mwaka.

Akizungumza katika mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa AICC, Mkulo alisema nchi kama Burundi na Rwanda, zimeweka taratibu maalumu ambazo zinawezesha fedha hizo kusaidia nchi hizo kutokana na fedha za wananchi wake walio nje ya nchi.

"Kuna hii kitu kinaitwa diaspora… watu walio nje wanaingiza kwa mwaka dola bilioni 12. Ni vema na sisi tujifunze kutoka kwa wenzetu wa Rwanda na Burundi jinsi ya kuzipata fedha hizi. Hii itawasaidia wale wanaozileta pale watakaporejea na pia kuisaidia mifuko yetu ya hifadhi za jamii," alisema.


Kwa upande mwingine, Mkulo alisema kuwa wanachama wa PPF wana wajibu mkubwa kuhakikisha kuwa mfuko unatimiza malengo yake kwa kuuwezesha kukabiliana na changamoto zilizopo.

Alisema kwa kuwa moja ya changamoto hizo ni ukusanyaji wa michango, ni vema waajiri wakahakikisha kuwa wanawahisha michango yao PPF na kuhakikisha kuwa wanawaandikisha wafanyakazi wao wote bila kuchelewa.

"Kwa kuwa kikwazo hapa kinaweza kuwa sheria, nafurahi kuwafahamisha kuwa rais tayari ameshasaini sheria kuhusiana na uendeshaji wa mifuko ya hifadhi za jamii.

Pia, iwapo itaonekana kuwa sheria hiyo bado haina nguvu sana, nipo tayari kupokea mapendekezo ya kuifanyia marekebisho," alisema.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, alisema kuwa kumekuwa na maendeleo katika uendeshaji wa mfuko huo na kubainisha kuwa thamani ya mfuko imepanda kutoka sh milioni 97 mwaka 1979 na kufikia sh bilioni 461 mwishoni mwa mwezi uliopita.

"Idadi ya wastaafu wanaolipwa pensheni ya kila mwezi imeongezeka kutoka 23 waliokuwa wanalipwa jumla ya sh 12,000 kwa mwezi mwaka 1979 hadi kufikia sh 18,502 waliolipwa jumla ya sh 1,026,815,081 kwa mwezi Septemba mwaka huu," aliongeza.

Hata hivyo, alisema kuwa licha ya mafanikio hayo, mfuko huo bado unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya uelewa mdogo juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa upande wa wananchi.

Pia alisema kuna changamoto ya waajiri ambao wanakwepa kuwaandikisha wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii na baadhi ya waajiri kutowasilisha kabisa michango ya wanachama.

Wakati huo huo, PPF jana ilimzawadia Waziri Mkulo kompyuta ya mkononi (lap top) kutokana na changamoto aliyoipatia PPF wakati huo akiwa mkurugenzi mkuu wa NSSF.

Kabla ya kuingia katika siasa, kwa muda wa miaka 14, Mkulo aliliongoza shirika hilo na wakati akiitambulisha zawadi hiyo, Erio alisema kuwa utendaji wa Mkulo akiwa NSSF, uliipa changamoto PPF jinsi ya kuboresha shughuli zake, ili kushindana na yanayofanywa na NSSF.

Hiyo ilikuwa ni moja ya zawadi ambazo watumishi wengine kadhaa wa PPF, wakiwemo wakurugenzi watatu waliowahi kuuongoza mfuko huo, Revelian Kabakama, David Mataka na Naftali Nsemwa, walipewa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu PPF ianzishwe mwaka 1978.
 
Huyu jamaa MBA yake ni fraud. Kichwa kimajaa ujamaaa. Spread the wealth mentality. Yeye anajua jinsi tunavyozitafuta hizi fedha?
Yeye ndie anae jua the best way ya kuinvest pesa za watazania walio nje, kwa nini asitafute the best way kuinvest pesa za Watazania katika hiyo mifuko yao hewa, ili ziwasaidie wazazi wetu walio retire.

This guy is tra*****
 
Wapitishe sheria ya uraia wa nchi mbili kwanza...

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Watanzania walioko nje hawana uzalendo wa kutosha kuruhusiwa dual citizenship, lakini pesa zao tunazitaka!
 
Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Watanzania walioko nje hawana uzalendo wa kutosha kuruhusiwa dual citizenship, lakini pesa zao tunazitaka!

Hawana shida ya pesa hao
Kama wngekuwa nayo si bora wafute misamaa ya kodi yote isiyo na manufaa kwa nchi.
Sijawahi kuona kitu rahisi zaidi ya kuomba na hicho ndio tutaongoza kuwa wa kwanz kwenye rank
 
Utawapa wakusaidie kuinvest lakini siku ukizitaka itakuwa issue kuzipata, kwani kila anayeusika atataka umpe rushwa kidogo pamoja na kuwa pesa ni yako.

waweke utaratibu mzuri kwanza kwa mambo ambayo tayari yako mikononi mwao the ndo wafikirie kuanzisha kitu kipya na sensitive kama hicho maana mtu kesharudi na anataka pesa yake atanue wewe unamletea za kuleta.
 
Back
Top Bottom