katika hari isiyo ya kawaida watanzania wanaendelea kuibiwa na kampuni ya TIGO ambayo hukopesha watu vocha ya shs. 400 na kuwataka walipe shs 440 ndani ya wiki hii ni sawa na riba ya 10% kwa wiki na kama tukiipeleka kwa mwaka ni sawa na riba ya asilimia 521% , mambo hayo yakiendelea katika nchi yenye kitengo cha udhibiti mfumo wa fedha na riba katika mikopo inayotolewa ndani ya nchi yetu, kitengo hiki kipo chini ya BOT ambayo nayo ni sehemu ya wizara ya fedha ya bwana MKULO, cha kushangaza hakuna kauli yeyote ambayo imetolewa na kitengo hiki wala waziri husika ndipo tunapotambua waziri mkulo naye anahusika katika kushiriki kuwaibia wananchi masikini wa tanzania kwani kama ameshindwa kusimamia watendaji wake wanaohusika na kudhibiti riba ya mikopo atangaze ameshindwa kuongoza na yeye ni mshirika wa wizi huu dhidi ya jamii ya kitanzania