Mkullo watuambiani: Kulipa pango kwa dola za marekani??

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,599
435
Nisaidieni wenzangu hii sheria ya matumizi ya dola za Marekani.

Hadi sasa nyumba na viwanjwa watu wanauza kwa dola.

Bila woga matangazo yote gazetini kuhusu kupangisha nyumba ni kwa dola za Marekani. Je zinatoka wapi hizi?

Benki kuu mnatuambiaje kuhusu hizi transactions? Watanzania hamuoni kam tunafanyiwa maisha yawe magumu makusudi?
Hizi dola hizi ni vipi? Nataka kupanga nyumba kila sehemu naambiwa $350, $ 500 ! nitafanya nini mie?:crying:

NISAIDIENI
 
Kwi kwi kwi teh teh teh. Hata vijana wanavaa Kimerekani, wanaongea kimerekani, wanacheza kimerekani.

Mambo ya maendeleo hayo!
 
NA ndio maana Tsh yetu inashuka siku hadi siku, kwa sababu hizi demand ya dola inakuwa kubwa ndio maana inapanda kila siku, nashangaa sasa hivi dola imedhibitiwa siui serikali ilikuwa wapi tokea enzi hizo isidhibiti dola mpaka imefika hapa ilipo leo ! very sad!
 
Nisaidieni wenzangu hii sheria ya matumizi ya dola za Marekani.

Hadi sasa nyumba na viwanjwa watu wanauza kwa dola.

Bila woga matangazo yote gazetini kuhusu kupangisha nyumba ni kwa dola za Marekani. Je zinatoka wapi hizi?

Benki kuu mnatuambiaje kuhusu hizi transactions? Watanzania hamuoni kam tunafanyiwa maisha yawe magumu makusudi?
Hizi dola hizi ni vipi? Nataka kupanga nyumba kila sehemu naambiwa $350, $ 500 ! nitafanya nini mie?:crying:

NISAIDIENI

wanafanya hivyo kwasababu shilingi yetu haijatulia inashuka utafikili inatafuta kuwa mshindi wa kupolomoka thamani!

hata wafanyakazi wanatamani mishahara walipwe kwa dola kwakuwa hizi pesa zetu hizi leo utaambiwa mshahara laki tatu ikiwa inaweza kununua gunia tatu za mpunga baada ya miezi mitatu lakitatu inatosha kununua gunia mbili za mpunga kaaaaaaaaaazi kwelikweli!
 
ni jambo la kawaida pia kuona watu wanatembea na dola mkwenye wallet, ada za shule ni kwa dola, maduka makubwa hata nguo pia zinauzwa kwa dola ni kama tumeshakubali kutumia dola kama pesa ya transaction!
 
Wewe kwani hujui siku dollar ndio sarafu ya Tanzania na wenye hizo kampuni za kukodisha nyumba na kuuza nyumba au viwanja ni vigogo hao hao. Wakibana dollarisation unadhani wakale wapi? Vumilia tu mkuu ndio faida ya kuchagua CCM na bado mtakoma hadi mtoe machozi ya damu.
 
Ukiiba fedha nyingi zaumma mwisho unakuwa mshamba mkubwa.
Wezi wetu wa fedha za umma kwa ushamba wanaiga kila kitu cha ovyo na aibu.
Kuna Maseneta, Makongresiman na MaCEO Choko hapa Marekani, hii tabia chafu ni lazima hawa washamba na Vijisenti vyao wamesha iga wanapigwa tayari.

Sijui kwa nini hawaigi mabarabara, open space na viunga vya nguvu vilivyopo hapa Marekani?
 
Back
Top Bottom