Mkullo: Maisha yangu yako hatarini!

..kwanini anataka akodi ndege kisirisiri?

..kwanini kuwe na usiri ktk matumizi ya fedha za walipa kodi?

..kwanini anafikiri maisha yake yako hatarini ikiwa anatekeleza majukumu yake kwa haki na uadilifu?

Just when others are fighting to have transparency in their governments, ours is preaching opacity... what bunch of loosers are leading this country...
 
Jamani ccm haihusiki, hili ni ni suala la Serikali kupitia wizara ya fedha

Asingekua hapo kama hakupata ubunge kupitia mlango wa CCM. Kwani kulikua hamna mbunge mwingine wakugombea huko kupitia hiki chama anayejali watu kuliko huyu? Au ndio mambo ya Masha yakupita bila kupingwa! Kati ya wabunge wote wa CCM Kikwete hakuona mtu mwenye uchungu na rasilimali za nchi anayeweza kuwa waziri wa fedha zaidi ya huyu? Si ameshafanya naye kazi for sometime ameona utendaji wake: au na Kikwete ni wale wale. It is real hard kuwatofautisha hawa watu, they always connect directly or indirectly kwa uwezo wao wakufikiri, na matendo yao.
 
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amewashukia watendaji wa ofisi yake kwamba wanahatarisha maisha yake kwa kuvujisha siri za wizara hiyo.

Mkulo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili hivi karibuni kuripoti kuwa alikodi ndege kwenda Dodoma na kumuagiza dereva wake amfuate kwa shangingi lake aina ya G8.



Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo kwenye ukumbi wa BZ, ulioko nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Bila kutaja majina, waziri huyo mwenye dhamana ya fedha, alisema utafiti wake umeonyesha kuwa wavujishaji wakuu wa siri katika wizara yake ni wakurugenzi, makamishina na watendaji wa kati..

“Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo,” alisema.

Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.

Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.

“Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!?” aliongeza.

Akitahadharisha juu ya kutokuwa na siri katika utumishi hususan serikalini katika wizara nyeti kama hazina ambayo ni roho ya nchi, Mkulo alisema kama hakuna usiri wa nyaraka katika serikali yoyote waelewe kuwa hakutakuwa na utawala.

Alisema nyaraka za serikali sasa zimezagaa mitaani hususan kwenye masoko likiwemo la Kariakoo jijini Dar es Salaam zikitumika katika matumizi yasiyo sahihi kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauza vitumbua na karanga.

Awali Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, akiwasalimia wafanyakazi katika mkutano huo jana alisema mbali na kulitumikia taifa kama mkaguzi na mdhibiti wa mali za serikali amebaini kuwa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la matumizi makubwa kuliko mapato jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo.

Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.

Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.

Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.


Source: Tanzania daima

Huyu jamaa ni fisadi mkubwa na hana uchungu na nchi hii kwa sababu si raia.
Angalia hata huko Kilosa ambapo yeye ni mbunge. Watu walipata janga la mafuriko wakapoteza mali, nyumba, mifugo na hata makazi.

Chanzo cha mafuriko hayo kilikuwa ni uzembe wa viongozi ambapo mkullo akiwa mbunge wa jimbo hilo ni mmoja wao. Viongozi walishindwa kufanyia matengenezo bwawa la kupunguza nguvu ya maji ya mto mkondoa ambao ulitiririsha maji yake kuelekea makazi ya watu.
Kingo za mto huo pia zilikuwa zimeharibiwa vibaya kwa muda mrefu hivyo nilitarajia viongozi wangechukua hatua za tahadhari mapema, lakini badala yake waliendelea kusinzia hadi watu walipopata maafa makuu.

Hata baada ya maafa Bw. Mkullo hakuonekana kutilia maanani janga hilo bali muda mwingi alikuwa Dar es salaam huku akisubiri kupewa taarifa za kwenda kupokea misaada ndio aende ili akauze sura na kuonekana kana kwamba yeye ndio ametoa hiyo misaada.

Serikali iliahidi kwa nyakati tofauti tofauti kuwalipa fidia na kuwajengea nyumba wale wote walioathirika lakini hadi leo hakuna lolote lililofanyika.
Watu waliandikishwa majina na kuahidiwa kupewa viwanja lakini hadi leo hakuna kitu. Je hii ni aina ya viongozi tunaowahitaji katika taifa letu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom