Mtumiabusara
JF-Expert Member
- Nov 18, 2009
- 473
- 40
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amewashukia watendaji wa ofisi yake kwamba wanahatarisha maisha yake kwa kuvujisha siri za wizara hiyo.
Mkulo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili hivi karibuni kuripoti kuwa alikodi ndege kwenda Dodoma na kumuagiza dereva wake amfuate kwa shangingi lake aina ya G8.
Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo kwenye ukumbi wa BZ, ulioko nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Bila kutaja majina, waziri huyo mwenye dhamana ya fedha, alisema utafiti wake umeonyesha kuwa wavujishaji wakuu wa siri katika wizara yake ni wakurugenzi, makamishina na watendaji wa kati..
"Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo," alisema.
Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.
Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.
"Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!?" aliongeza.
Akitahadharisha juu ya kutokuwa na siri katika utumishi hususan serikalini katika wizara nyeti kama hazina ambayo ni roho ya nchi, Mkulo alisema kama hakuna usiri wa nyaraka katika serikali yoyote waelewe kuwa hakutakuwa na utawala.
Alisema nyaraka za serikali sasa zimezagaa mitaani hususan kwenye masoko likiwemo la Kariakoo jijini Dar es Salaam zikitumika katika matumizi yasiyo sahihi kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauza vitumbua na karanga.
Awali Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, akiwasalimia wafanyakazi katika mkutano huo jana alisema mbali na kulitumikia taifa kama mkaguzi na mdhibiti wa mali za serikali amebaini kuwa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la matumizi makubwa kuliko mapato jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo.
Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.
Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
Source: Tanzania daima