MKUKUTA Phase I: Maoni yako

Ningependa kupata mawazo yenu kuhusiana na mchakato wa kupitia MKUKUTA kuona mashiko yake katika kuleta maendeleo, mafanikio hadi sasa, vikwazo vilivyopelekea malengo yasifikiwe n.k
Kama mtakavyokuwa mmesikia, huo mchakato unaendelea na kuna sababu kadhaa za kuupitia huo mpango (MKUKUTA) kama nitakavyonukuu hapo chini:

Several reasons justify the review of MKUKUTA , including
(i) the need to set new targets to be implemented from July 2010
(ii) to draw lessons of their implementation (what worked and what did not work) and refine interventions accordingly;
(iii) to assess accomplishment of reforms, alignment of systems, processes and programs in light of MKUKUTA and MKUZA implementation
(iv) to accommodate new and emerging challenges at both national and global levels and reposition successor strategies accordingly
(vii) to address challenges facing LGAs and other challenges related to service delivery
Wachumi,wanaharakati, wanasiasa, mna maoni gani?

Thanks Mazee

Some of us have limited insight of Mkukuta, we only have a few review notes and most of them from REPOA, which makes it tircky when it comes to faiew views of the mpango; is it possible kutupa a few hints or links ili tupate kashule kwa mbali?

BTW, whats up with the brand changes? from WoS, to tWoS and now VC?
 
Kwanza ni kiri kuwa pamoja na kwamba sikufahamu napenda arguments and assertion zako maana zinaenda na facts na siyo myth.

Kwa mchango wa poverty issues kwanza kabisa Tanzania haitaendelea kwa ku copy na ku paste policies za wazungu; discoursed ideas bila kuangalia how they express the institutions realities za Tanzania. Pamoja na kuwa kwenye karatasi Tanzania inaonekana economy yake ina kuwa lakini qualitatively si kweli maana inequality gap inakuwa welfare ya watu wake si nzuri; mashule kibao quality questinable etc. Nachokiona setback kubwa ni institutions za tanzania zilizo formal haziko legitimate to the locals (watanzania) na informal ndo hasa ziko in operation. Sasa usipotambua hilo basi mwendo utakuwa huu tu. Chanzo cha semina ni mshahara mdogo wa wawatumishi wa umma; maisha ya ghali ambayo bila ujanjaujanja hakuna anaeweza kusurvive so kwa ujumla wote tu my fisadi tunatofautiana degree tu.

Policy zote ni za vitabuni hakuna hata moja ina operate in reality why kwasababu hazitambua particularities za wananchi wa Tanzania ziko based on theories ambazo ni western derived. Kuna bias katika development priorities na hii inasababishwa na beuraucrats ambao wana weza ku influnce government to act on their favour. Pesa nyingi zinaishia mijini hakuna trical down na huku mlipa kodi wa uhakika ni rural majority. Sasa usipoweza ku raise income ya majority tax payers basi saving yako itatoka wapi? Unamkamua ng'ombe majani hutaki kumpa. As a result kwasababu the elite can survive kwa huo ujanja they see it okay wako kwenye comfort zone not rich not poor ila uncertain na kwasababu hiyo mjanja zaidi lazima ahakikishe anavyo vingi zaidi ili kureduce uncertainty. Swali ni je for how long can we continue like this?

Until we all agree by doing these we are all worse off operating under low utitlity in general na tusipo legitimize hizo informal institutions na kufanya rearangement tutaishia scramble and then partition of the resources kila mbuzi anakula kamba yake itakapo ishia.

Felister, Zakumi, Masanja na wengineo mlioshiriki mjadala huu - HAPPY NEW YEAR 2010 kwanza!

Pili, ndugu zanguni, sijui kama mmeshiriki kuingiza inputs zenu kwenye process ya MKUKUTA II maana MKUKUTA I is coming to an end this July!

Wapendwa nadhani mmeshasikia kuwa maoni yanapokelewa hata kupitia e-mail - mkukutamonitoring@gmail.com

Tafadhalini, chondechonde leteni mawazo tuyapeleke huko ili tuchangia kuweka mkakati bora!
 
Let me share some of my thoughts on this japo kwa kuuliza maswali;

can we fight poverty and eradicate it without changing the political system of governance?
Can we create a wealth society without tackling the way wealth is being produced and distributed?
Can we really fight poverty without fighting corruption? What if to some people corruption is a way of getting out of poverty as we have witnessed in so many ways and times?
 
Is there any relationship between poverty and corruption?
Is there any relationship between foreign aid and corruption and subsequently with poverty?
Is there any relation between governance and corruption or governance and poverty?

in other words, can we eradicate poverty without looking at governance, corruption and foreign aid?
 
Let me share some of my thoughts on this japo kwa kuuliza maswali;

can we fight poverty and eradicate it without changing the political system of governance?
Can we create a wealth society without tackling the way wealth is being produced and distributed?
Can we really fight poverty without fighting corruption? What if to some people corruption is a way of getting out of poverty as we have witnessed in so many ways and times?

MMKJJ,
Asante kwa maswali yako mazuri na pertinent.
Hicho ulichokiuliza ndicho haswa MKUKUTA/NSGRP wanakiangalia chini ya Cluster 3 ON GOVERNANCE AND ACCOUNTABILITY ambayo ina outcomes zifuatazo:
1. Good governance and the rule of law are ensured
2. Strategic, responsible & trustworthy leaders and public servants in place
3. Democracy, political stability and social cohesion sustained
4. Economic governance enhanced
5. Peace, security and national unity enhanced

Pia ina goals zifuatazo:
  • Structures and systems of governance as well as rule of law are democratic, participatory, accountable and inclusive
  • Equitable allocation of resources with corruption effectively addressed
  • Effective public service framework in place to provide foundation for service delivery improvement and poverty reduction
  • Rights of poor and vulnerable groups are protected and promoted in the justice system
  • Improved personal and material security, reduced crime, elimination of sexual abuse and domestic violence
  • National cultural identities enhanced and promoted.
Hii ina maana kuwa pasipokushughulikia utawala uwe bora usiokuwa na rushwa basi itakuwa ngumu sana kuuondoa umaskini.

Swala hapa ni je, ni kwa kiwango kipi Governance and accountability imefanikiwa MKUKUTA I?
 
Thanks Mazee

Some of us have limited insight of Mkukuta, we only have a few review notes and most of them from REPOA, which makes it tircky when it comes to faiew views of the mpango; is it possible kutupa a few hints or links ili tupate kashule kwa mbali?

Mkuu tuko pamoja hapo juu.
 
MMKJJ,
Asante kwa maswali yako mazuri na pertinent.
Hicho ulichokiuliza ndicho haswa MKUKUTA/NSGRP wanakiangalia chini ya Cluster 3 ON GOVERNANCE AND ACCOUNTABILITY ambayo ina outcomes zifuatazo:
1. Good governance and the rule of law are ensured

In our country we don't have anything that is related to good governance and rule of law na kuna mifano mingi sana ya kuthibitisha hili na hali hii imeshamiri sana kuanzia awamu ya Mzee Rukhsa, Mkapa na hadi sasa kwa Kikwete

2. Strategic, responsible & trustworthy leaders and pub

These are also lacking in our beloved country. Mikakati yetu mingi huwa mizuri kwenye makaratasi ikija kwenye utekelezaji ni sifuri. Mifano ya hili ni sera za ubinafsishaji, sera za kuwaruhusu "wawekezaji" katika ralisimali zetu, sera zetu kuhusu kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na hata "kilimo kwanza" nacho mapapa mafisadi Jeetu na Manji wameshavamia na hakuna kinachoendelea na Serikali imekaa kimya huku ikiogopa kuwagusa maana hawa wote wameiweka Serikali mifukoni mwao.

Viongozi wetu wengi si waaminifu wameweka mbele maslahi yao ya kujitajirisha haraka haraka kupitia dhamana za uongozi tulizowakabidhi na kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hili. Kwa maoni yangu sioni mafanikio yoyote ya kuridhisha tangu awamu ya Mzee Rukhsa hadi sasa pamoja na kwamba ssa hivi hatufuati tena sera ya ujamaa na kujitegemea, ukiondoa Watanzania wachache waliopata mafanikio kihalali na wengine kupitia ufisadi.

Kwa kifupi hivi vipengele viwili vina umuhimu mkubwa sana katika kuhakikisha mafanikio ya MKUKUTA, bila mafanikio ya vipengele hivi viwili basi yaliyomo ndani YA MKUKUTA yataendelea kuwa mazuri kwenye makaratasi tu lakini utekelezaji wake utakuwa ni sifuri na Watanzania hatutafanikiwa kwa lolote kutokana na MKUKUTA I au MKUKUTA II.
 
Kwa faida ya wale wasioelewa undani wa MKUKUTA:

MKUKUTA I ulianza 2005 basically mpango kabambe wa kuondoa umaskini na kutekeleza Malengo ya Millenium yaliyopitishwa na Umoja wa mataifa ambayo Tanzania nayo iliridhia.On MILLENIUM DEVELEOPMENT GOALS pls google ili upate undani wake zaidi.

Huu Mkukuta una Clusters 3:

Cluster I - Growth and Reduction of Income Poverty, - hapa ndio ukuzaji wa uchumi - sustainable broad based growth ina an equitable manner

Cluster II- Improvement of the Quality of Life and Social Well-Being - hapa sasa ndio mambo ya kupata huduma kama afya, elimu na kumuondelea mwananchi zahama za maisha ya kila siku aweze kuishi na kujikimu

Cluster 111: Governance and Accountability - hii inaangalia mfumo mzima wa utawala kwa maana ya taratibu, kanuni, mifumo ya utoaji haki pamoja na utawala wa sheria, ushiriki katika siasa, kuondoa rushwa, mambo ya security yaani usalama wa mtu na mali zake nk.
Kwa undani zaidi google upate the full document.

In short MKUKUTA au Mpango wa kuukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini, ni mpango kabambe uliowekwa na serikali kama dira ya kupambana na umaskini wa nchi yetu uliokithiri.

Mpango huu awamu ya kwanza itaisha July 2010.Sasa hivi kuna kazi kubwa sna ya kuu review na kufanya maboresho ili MKUKUTA II uwe bora zaidi.Utaratibu unaotumika ni kushirikisha wataalamu na pia wananchi kwa ujumla.Kwa wale wenye kusikiliza redio au kuangalia TV mtaona matangazo kuhusu kupokea maoni na kuyawakilisha serikalini hata kupitia e-mail - mkukutamonitoring@gmail.com

Tutumie fursa hii ili tusiwe wapiga kelele tu humu JF bali tupeleke maoni yetu huko kunakohusika.
 
Nakushukuru sana kutufahamisha wapi pa kupata maelezo ya kina kuhusu MKUKUTA I

Jirani, hapo chini kabisa nakuomba kitu kimoja maoni ambayo yatawekwa hapa na wachangiaji wote ambao watapenda kufanya hivyo unaweza kuyakusanya na kuyapeleka kwa wahusika ili wafayanyie kazi.

Je, kama hakukuwa na mafanikio yoyote katika MKUKUTA I unadhani kutakuwa na mafanikio katika MKUKUTA II au ni ufujaji tu wa fedha and at the end of the day there would be nothing to show off!?
 
Nakushukuru sana kutufahamisha wapi pa kupata maelezo ya kina kuhusu MKUKUTA I

Jirani, hapo chini kabisa nakuomba kitu kimoja maoni ambayo yatawekwa hapa na wachangiaji wote ambao watapenda kufanya hivyo unaweza kuyakusanya na kuyapeleka kwa wahusika ili wafayanyie kazi.

Je, kama hakukuwa na mafanikio yoyote katika MKUKUTA I unadhani kutakuwa na mafanikio katika MKUKUTA II au ni ufujaji tu wa fedha and at the end of the day there will nothing to show off!?
Ninashukuru kwa michango yako wewe na wengine.

Nitaomba MODERATOR WA JUKWAA HILI ATUSAIDIE KUFANYA EXTRACTION YA KEY ISSUES AMBAZO NI STRATEGIC ILI IWE NI SAUTI YA JF.

Nitakuwa pamoja naye kwenye hili.
 
Jirani, hapo chini kabisa nakuomba kitu kimoja maoni ambayo yatawekwa hapa na wachangiaji wote ambao watapenda kufanya hivyo unaweza kuyakusanya na kuyapeleka kwa wahusika ili wafayanyie kazi.
Mkuu BaK,

JF itayapeleka maoni haya kunakohusika, hivyo naomba kuwasisitiza wadau hima wasisite kutoa maoni yao. Tutawafahamisha wiki mbili kabla ya kuyaunganisha kuyapeleka.
 
Mkuu BaK,

JF itayapeleka maoni haya kunakohusika, hivyo naomba kuwasisitiza wadau hima wasisite kutoa maoni yao. Tutawafahamisha wiki mbili kabla ya kuyaunganisha kuyapeleka.

Ubarikiwe Mkuu.
 
let me share some of my thoughts on this japo kwa kuuliza maswali;

can we fight poverty and eradicate it without changing the political system of governance?
Can we create a wealth society without tackling the way wealth is being produced and distributed?
Can we really fight poverty without fighting corruption? What if to some people corruption is a way of getting out of poverty as we have witnessed in so many ways and times?
that is all we need to do to stop the cirlce of pretendance that we do care
 
Companero.. that is why we are connecting the two. Mada hii ilikuwa ni ya Mkukuta 1 na sasa tunajua wamejiandaa na 2 hivyo tunataka tutoe maoni yetu..
 
Mwaka 2005 wakati MKUKUTA I inaanza haya ndiyo yalikuwa malengo yao kwa miaka mitano (hadi 2010)

  • Accelerated GDP growth rate to attain a growth ra te of 6-8% per annum by 2010
  • Scaled up participation of the informal sector and SMEs (including cooperatives).
  • Increased growth of manufacturing sector from 8.6% to 15% by 2010
  • Increased agricultural growth from 5% in 2002/03 to 10% by 2010.
  • Increased growth rate for livestock sub sector from 2.7% in 2000/01 to 9% by 2010
  • Increased technological innovation, upgrading and use of technologies.
  • Promoted regional equity in development and capacity for growth and infrastructure that enables investment and liveli hoods diversification
  • Repaired 15,000 kms of rural roads annually by 2010 from 4,500 kms in 2003.
  • Reduced negative impacts on environment and peoples' livelihoods.
  • Reduced land degradation and loss of biodiversity.
  • Increased export proportion of value adde d minerals from the current 0.5% to 3.0% by 2010.
  • Sustainable and broad based growth can only be realised through accelerated GDP growth
Kwa kiasi gani tumefikia haya.. chini nimeambatanisha Matrix ya MKUKUTA...
 
Attachments

  • nsgrpmatrix.pdf
    208.2 KB · Views: 63
Mwanakijiji maoni ya Mkukuta I yashatolewa, yaliyopokelewa yashapokelewa na yaliyowekwa kapuni yashawekwa kapuni - wenzenu wanamalizia Mkukuta II na nasikia ule mhimili wa utawala bora na uwajibikaji washautoa eti uko ndani ya mihimili mingine!
 
The whole thing appears to be a sham, how can one body achieve all of their proposed targets in the short period of time. The mammoth of the their task you'd think the organisation is receiving command straight from IKULU with ministries liasing to oversee the implemention of those policies.

MKUKUTA is just a single organisation but it has tasks that requires it, to act as an Umbrella of not more than these different groups based on their proposed goals Health Advisors, Agricultural Experts, Economist and Lastly a team of social workers (mainly consists members who understand their culture of poverty and ways of advising those aimed to improve their lives).

In a real world you'd see an experts recomendation after a careful study of the causes and ways of improving those situations. If they were serious about MKUKUTA you'd expect debates in our parliament as its not a cheap asking besides it would have been the largest employer in the country.

Ndio maana mwenye akili timamu anaona from day one just good talk, drafted by some experts on what to say just to please the donors. Lakini ukweli wenyewe amna nia or else mtu aje atuambie even a single success policy ya mkukuta maana wana nyingi.

Amini au watu wanaokaa maofisini kujikuta hawajui wajibu wao if MKUKUTA was a genuine body wangekua na cha kufanya it is a mammoth asking and this is what is meant by home politics (social policy) apart from a few other sectors period and the little attention it receives on the media na bunge letu one has to conclude the whole thing is a joke.
 
Mkuu heshima kwa taarifa muhimu kimaendeleo.

tatizo letu kubwaa kufikia hayo malengo ni uwezo wa kiuongozi kwa maana ya watu makini na wenye forward thinking approach.

hapa najumuisha viongozi (wanasiasa na watendaji wote) pamoja na jamii husika katika kuhoji vipaumbele vya taifa lao na utekelezaji wake.

ni jambo la kusikitisha kwamba serikalini viongozi wenye uelewa wa maana ya MKUKUTA leave alone mapungufu yake ni wachache sanaaa na the rest wanaizungumzia tuu kama hadithi hata work plan hawawezi kuandaa kuendana na maeneo yao achilia mbali ufuatiliaji.

nchi hii lazima tuwe na focus ya kuwa na rasilimali watu (human capital) kwani ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi. hatuwezi kujivunia maliasili na rasilimali nyingine kama ardhi kubwaaaa yenye rutuba bila kuwa na ujasiri wa kuzifanyia kazi kwa maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla.

silika yetu ya UVIVU wa kupenda kusimamiwa zaidi katika utendaji bila kuwa na minimum supervision from personal level to national level ni kikwazo kikubwa kufikia maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla.

kutwa nzima tunapiga kelele kuhusu mafisadi na upuuzi wake bila kujadili kwa mapana uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja na umuhimu wa kujenga tabia ya uwajibikaji wa tija na ufaanisiii... afterall ufisadi uliopo chanzo chake ni utawala uliochokaaa wa CCM unaotumia kama mbinu ya kuendelea kutawalaa..

tuna mambo mengi ya kuyajadili kwa mapana as our common interest and avoid our accasional difference to frustrate the REAL PROBLEMS WE HAVE AS A NATION.

mkukuta utekelezaji wake utaendelea kuwa wa kusuasua na matokeo yake kukosa kasi ya kufaa kwa sababu tuu kama taifa hatupendi kutoa changamoto ya uwajibikajiii...

natoa rai tena tujadili kwa MAPANA UKOSEFU WETU WA KUTOKUWAJIBIKA KWA VIWANGO STAHILI VYA KUFIKIA MAENDELEO.

PAMOJA NA UTAJIRI WOTE WA ASILI TULIO NAO TUMEKOSA RASILIMALI WATU KUGEUZA KUWA UTAJIRI NA HATIMAYE KUSONGA MBELE KIUCHUMIII.

Umenena Nyauba. Bila Rasilimali watu yenye ujuzi unaotakiwa tusahau kutoka hapa tulipo. Tuanze kwanza na Elimu na mengine ndiyo yafuate. Driving Force ya Kutuletea maendeleo iwe Elimu Bora, Kisha Afya na Kilimo. Nje ya hapa ni kutwanga maji kwenye kinu.

Angalieni matokeo ya kidato cha nne (2009)--Zaidi ya aslimia 87 wamepata Daraja la Nne na Zero. Ni ndoto kutoka hapa tulipo bila elimu bora hasa ya Sayansi na Ufundi. VETA hatujaipa uzito inaostahili. Kama gharama ya kujenga chuo kimoja cha VETA ni shilingi bilioni 5, kwa nini tunashindwa kujenga vyuo vya VETA angalau 20 kila mwaka.
Ukiangalia vijana wa shule za msingi waliofeli mwaka jana na hawa wa kidato cha nne waliopata daraja la nne na zero, ni hatari tupu. Vijana karibu laki 8 hawana muelekeo kielimu na mbaya zaidi hatulioni hili kama tatizo.
 
Back
Top Bottom