Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Za10,
Kuna jamaa yangu wa Ghana ambaye nilikuwa naye kama week moja iliyopita alinishangaa wakati namweleza kuhusu upotevu wa zaidi ya $1bn katika dili za kifisadi kupitia viongozi wa dola na wapambe wao. Alinambia kuwa wakati wa Jerry Rawlings waliunda kikosi cha kupambana na rushwa ambacho hadi sasa kinafanya kazi nzuri. Ukiacha tatizo la muundo wake kwamba wakuu wake ni maofisa wakuu wa jeshi na polisi, jamaa alisema hiyo anti-corruption unit inatisha sana. Alinambia kuwa baada ya uchaguzi kuna baadhi ya kesi za rushwa ambazo rais mpya ameagiza zishughulikiwe haraka. Matokea yake watu wanataka kufa kwa pressure na tayari waziri mmoja wa zamani kakamatwa uwanja wa ndege akitaka kuingia mitini. Jamaa anasema kuwa Anti-corruption kama yetu iliyochini ya rais haiwezi kamwe kufanya kitu. Hata kwao wanayo ya dizaini hiyo ambayo wananchi hawajui hata inachokifanya. Kwa ufupi PCCB yetu ni sehemu ya drama ya uongozi wa hovyo na ufisadi! Nadhani tunahitaji jeshi kidogo ili tupige kwata. Hata nidhamu ya wanafunzi wa Mgulani na Makongo siyo sawa na Kinondoni Muslim!!
DC:
Nilikuwa nakitazama kitu kimoja lakini sijuhi kama kuna correlation ya JMK effect. JMK sina maana na Jakaya Mirisho Kikwete. Nina maana na Jerry, Museveni na Kagame.
Kutokana na mazingira waliyochukulia madaraka, waliweza kujitenganisha wao na serikali zilizotangulia.
Labda tunahitaji mtu wa kuweza kututenganisha na serikali zilizotutangulia hili mambo fulani yaweze kufanyika.