Mkuki kwa nguruwe..!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Ni kwa nini mwanamke anapofumaniwa inakuwa inauma sana na kuwa issue kuliko mwanaume anapofumaniwa?
 
wote inauma sana!

Kwanini sasa mwanaume inakuwa rahisi kumacha mwanamama kuliko yeye kufanya hivyo...au kuna kitu mungu kawaumba nacho...kama vile uvumilivu?
In most cases nimeona wanaume wanaumia sana na kuacha wanawake wao
kuliko wadada kumuacha wanaume....?
 
Sijali inauma kiasi gani ila kinachowaudhi watu wengi ni maumbile ya mwanamke kuwa kama kokoro. Hakuna mwanamume ambaye anabeba uchafu kuleta home. Ila mmhhh,... kama jamaa alikuwa na volume ya kutosha, mama ataibeba na kuja nayo hadi home! Sasa hapo kwa nini isiume sana?? Inakuwa kama anapaka pili pili kwenye kidonda. Kwanza kakandamizwa halafu bado ana huo uchafu hadi kwenye bedroom yenu!!
 
...Mh!!! Sahani ukilia chakula unatupa? au unasafisha ili na mwenzako atumie????
 
Kwanini sasa mwanaume inakuwa rahisi kumacha mwanamama kuliko yeye kufanya hivyo...au kuna kitu mungu kawaumba nacho...kama vile uvumilivu?
In most cases nimeona wanaume wanaumia sana na kuacha wanawake wao
kuliko wadada kumuacha wanaume....?

Hiyo kweli. Mara ngapi tumesikia mwanamke kaachwa, ila mwanamke anagumia tu. Na sanasana ataitiwa ndugu kusuluishwa.
Kwa nini kwa mwanamke tu na si mwanaume? Mke naye akifumania basi amwache mumewe?
 
Wanaume sio wavumilivu hata kidogo kama walivyo wanawake. Mwanaume anaona ana haki kwa kila kitu hata akifumaniwa yeye ana haki tu. Swala la uchavu hata mwanamume ana kuja na uchafu huo huo nyumbani kwani huko alikotoka pia si ailikuwa anafanya uchafu. Swala ni kuwa wavumilivu na kuchunga ndoa au mapenzi yenu na sio mmoja wenu kujiona much know kuliko mwenziwe.

Bora nusu shari kuliko shari kamili.
 
Ni kwa nini mwanamke anapofumaniwa inakuwa inauma sana na kuwa issue kuliko mwanaume anapofumaniwa?

kwakweli hata na mimi nashangaa sana,wanaume wengi tu nawajua wana nyumba ndogo,ila sasa ikija wamesikia fununu au wamewafuma wake zao, ni kosa kubwa sana,tena mwanaume anapitiliza mpaka anazaa na mtoto nje ,huo ni uthibitisho tosha ,ila mwanamama anasamehe yote hayo,

ushauri wanaume na nyie muwe mnavumilia kwakweli,wakati mwingine mwanamke akienda nje ,haishii huko,yeye lazima atarudi nyumbani tu,kwasababu ya watoto na kulinda heshima kwamba ameolewa.na mapenzi yataongezeka kwako ,so msiwe na wasiwasi,ila nanyie muwe mnajirudi,hapo mama atakuwa anahitaji attention. tuuu
 
Kuna utofauti mkubwa sana mkuu maana swali lako halijakwenda shule bado...Umeshasema mwanamke sasa hapo huoni kama kunatofauti fulani kati ya mwanamke na huyo mwanaume???Pia mwanaume ni mtu mwingine hata akifanya kosa kama hilo atambembeleza mwanamke yatakwisha lakini mwanake afanye hivyo nadhani nitamkata shingo kwa hiyo ndio kama mwanaume anasheria za mikoni zaidi kuliko mwanaume ndio mwanamke huwa anahofu zaidi.
 
Ah! Hii haijatulia,,,, tufafanulie kidogo,,,, hatukuelewi. Hapa ni nini hakieleweki?

Ok wacha nikupe story iliyonifanya niulize haya:-
Mke wa kijana mmoja ambaye si haba, mwenye utajiri wake wa kutosha alioa pia kwa familia ambayo si haba. Ugomvi unaanzia kuwa huyu mvulana alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa baba mkubwa wa msichana kwa maana ya mkewe. Mke akagundua, akamwonya mumewe na pia mdogo wake, lakini mchovya asali hachovyi mara moja, wakaendelea kuvunja amri ya sita ya wakristu. Mke akafikia hatua ya kuunda na kulipa kundi la kiharamia na kumteka mdogo wake ili afunzwe adabu. Binti wa watu akatekwa na kufanyiwa ufirauni wa haja. Kwa sasa amehama mji. Bwana hakutulia akaendeleza libeneke kwa mademu wengine, mke naye akaanza kutafuta raha aliyoifata kwa bwana ambayo anaikosa kwa mumewe. Ikumbukwe kuwa hakuna mwanamke anayekosa kitanda, chakula na yote toka kwao ila huwa anafata raha, RAHA ya unyumba na kuwa na familia, ambayo kaka yake hawezi kumpa wala baba yake. Ikabidi atafute kidume cha kumpa raha hiyo! Unajua tena mijimama inayonukia harufu ya pesa na ambaye ana kiu ya hii kitu. Kijana akawa anampida kisawasawa. Hakuna siri dunia hii, sercretary wa huyu mama akagundua, naye secretary akavujisha siri kwa Mzee. Fumanizi likaandaliwa. Siku ikafika, mama kama kawaida akaenda uwanja wa ugenini, kijana naye pia. Wakiwa katikati ya mechi wakapata ujumbe kuwa wanakuja kufumaniwa. Kijana akabadilisha chumba na akafanikiwa kutoroka lakini mama akakutwa chumbani bila kuwa na la kujitetea. Jamaa kwa hasira akamfukuza mke na kwenda kuezua nyumba alokuwa anakaa kijana mtuhumiwa pia amefunga salon mkewe aliyokuwa anaimiliki. Mke yuko kwao kwa sasa, ila bwana anashindwa kutoa talaka maana mgawano wa mali nao ni mgumu maana kichele si haba. Nikajiuliza je? Huyu bwana alipokuwa anayafanya haya mkewe yeye hakuwa na nyongo? Ama ni yale yale ya Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu?
 
Haijatulia hii!
Utaishia jela bureeeee!
 
ndio hayohayo ndugu yangu, mkuki kwa nguruwe unanoga kweli kweli lakini kwako wewe ...?
mke hata akijiiba maramoja tu hata kama kwa bahati mbaya atakiona cha mtema kuni, mume atajivinjari tena ataweka na nyumba ndogo kabisa lakini aah ...na hata kama mkewe ukifahamu yeye yupo tu, anajitetea halafu anaendelea

mi nadhani tatizo moja hapa ni mwanaume ku take advantage ya unyonge wa mwanamke... wanawake wengi wapo weak emotionally and physically, ndio maana wengi hata wakijua mume anacheat wanapambana na mwanamke anayechiti naye...japo haisadii hata kidogo kumaliza tatizo, nchi kubwa kama bongo utapigana na wangapi?...

tatizo jingine kwa mtazamo wangu ni mwanamke kutokujiamini na kuwa tegemezi kwa mumewe, binamu yangu mmoja ana mume kipanga sana...kapigana na wanawake wenzie wee, mpaka siku moja akakumbana na kadada kamoja kakampiga na kumtoa ngeu utafikiri kenyewe ndio kenye mali, akarudi ma manundu uso mzima...baada ya hapo binamu yangu hajapiga mtu tena...sasa basi nilipomuuliza binamu yangu mbona kila siku analalama tu ooh magonjwa ooh aibu ..oh presha ..roho inauma sana, kwa nini haondoki? akaniambia sababu zifuatazo
  1. miaka 39 na watoto watatu niondoke niende wapi? nani atakeyenioa tena na uzee huu, si ntaishia tu kuwa nyumba ndogo za watu?
  2. kwanza sina kipato cha kutosha mume ndiye anayesomesha na kutunza mimi na watoto kipato changu ni nyongeza tu...nikimuacha tutatunzwa na nani?
  3. talaka itaumiza wanangu, sitaki kuondoka kumuachia mwanamke mwingine anilelee wanangu
inawezekana wanawake wengi tu wanalazimika kuvumilia kwa sababu kama hizo...yaani rohoni mwao ndoa hamna tena imeshavunjika ila tu hawana ubavu wa kuondoka
 
Hata ndoa zipo za wake wengi lakini si kinyume chake!
Ndoa za waume wengi zipo pia ila sio utamaduni wetu... Ni kama vile kuna watu wanawake ndo wanalipa mahari au wengine mtoto ni wa ukoo wa mama....
 
Back
Top Bottom