Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
* Asema uroho wa madaraka unawamaliza
* Vigogo waikimbia CHADEMA wajiunga CCM
Na David Paul, Biharamulo (Uhuru)
UMAARUFU wa vyama vya upinzani nchini umekuwa ukishuka kadri siku zinavyokwenda kutokana na malumbano ya kila mara ndani ya vyama hivyo, yanayosababishwa na viongozi wakuu kungangania madaraka.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), George Mkuchika, alisema hayo kwa nyakati tofauti, alipohutubia mikutano ya hadhara katika kata za Lusahunga na Biharamulo Mjini, kumnadi mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa.
Alisema kuporomoka kwa umaarufu wa wapinzani kunatokana na malumbano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi yanayosababishwa na uroho wa madaraka.
Kutokana na hilo, alisema wapinzani wasipewe ridhaa ya kuongoza, kwani nchi itaharibika.
Hawa wenzetu wa upinzani wamekuwa wakisimama majukwaani na kuwaeleza wananchi kuwa mmekichoka CCM, nasema si kweli, Watanzania bado mna imani kubwa na CCM, na ushahidi tunao, angalieni wenyewe takwimu za matokeo ya uchaguzi uliopita kuanzia mwaka 1995.
Mwaka 1995 mgombea wa CCM Benjamin Mkapa, alipata asilimia 62 ya kura zote na mwaka 2000, alipata asilimia 72. Mwaka 2005 Rais Kikwete (Jakaya) alipata asilimia 80, ni wazi kuwa wananchi bado wana imani kubwa na CCM, alisema.
Akizungumzia viti vya ubunge, alisema mwaka 1995 vyama vya upinzani vilipata 49, huku katika uchaguzi wa mwaka 2000 idadi ikipungua na kuwa viti 29.
Mkuchika alisema hali iliendelea kuwa mbaya zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2005, ambapo vyama vya upinzani viliambulia viti 26 kati ya majimbo 232 yaliyopo.
Kutokana na takwimu hizo, Mkuchika aliwaomba wakazi wa Biharamulo Magharibi kuhakikisha hawapotezi kura zao kwa kuwachagua wapinzani, ambao kimsingi wameonekana kupoteza mwelekeo na imani kwa wananchi.
Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika Julai 5, mwaka huu, ambapo wapigakura wamehakikishiwa usalama wa kutosha ili kuwawezesha kujitokeza kupiga kura kwa wingi.
Wakati huo huo, CHADEMA kimeendelea kupata pigo katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Biharamulo Magharibi, baada ya CCM kuendelea kukisambaratisha.
Licha ya hivi karibuni wanachama wake takriban 60 kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kutoka maeneo ya Soko Kuu la Biharamulo, majuzi Katibu Mwenezi wake wa wilaya alijiunga CCM.
Katibu Mwenezi huyo wa CHADEMA, David Mayala, alikihama chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kuhudhuria mkutano wa kampeni kumnadi mgombea wa CCM, Oscar Mukasa, uliofanyika kwenye kijiji cha Luziba.
Akizungumza kwenye mkutano huo baada ya kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa viongozi wa CCM, Mayala alisema ameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi baada ya kuvutiwa na sera zake.
Mayala alidai CHADEMA hakina dira na kuongeza: Jamani msidanganywe hata kidogo, kule upinzani hakuna kitu kipya ni kupoteza muda tu.
CHADEMA wana malengo binafsi si kama ilivyo CCM ambayo inalenga kuwasaidia wananchi, alisema huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo.
Kwa mujibu wa Mayala, pia amekerwa na sera za CHADEMA zinazolenga vurugu, akisema chama hicho hakistahili kupewa kura.
Mwingine aliyejiunga na CCM kutoka CHADEMA ni Katibu wa tawi la Nemba, lililoko kata ya Nyabuso, ambayo ni ngome ya chama hicho, Lucas Nyamegoro.
Nyamegoro alijiunga na CCM juzi, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbindi, kata ya Nyabusozi.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Nyamegoro aliwataka wananchi wasitishwe au kurubuniwa na wapinzani, hususan CHADEMA kwa kuwa chama hicho kinajali maslahi binafsi.
Nyamegoro alisema hakuna chama kinachoweza kuwaletea maendeleo wananchi na kutatua kero zinazowakabili zaidi ya CCM.