Mkuchika na Pumba Zake: Aifananisha Timu ya Sudani na Idd Amin..!

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Wakuu Samahanini nilipotea kwa muda kwenye kutafuta katika hali yetu ya kawaida. Nimerudi na naomba mniruhusu kuendelea kuchangia, yangu leo machache.

Hivi ni kweli huyu ajulikanaye kama Mheshimiwa Captain Kamanda Mkuchika ndiye Waziri wetu wa Habari tunayemtegemea? Nimemshangaa kwa muda maana namsikia kwa muda akiongea mambo ambayo siyaelewi. Kwanza nilimsikia akisema anapiga marufuku wimbo wa Taifa kwenye simu, pili leo namsikia akitema pumba nyingine wakati anakabidhi bendera ya taifa kwa timu yetu kwenda Sudani, kasema Baba wa Taifa alivyofanikiwa kumtoa Idd Amin alienda hadi kwake Uganda kumchapia hukohuko. Je, huo ndio mfano halisi wa kuwapa timu yetu ya taifa? Je, timu ya taifa ya Sudani yaweza kufananishwa na Idd Amin?

Swali langu la msingi hili hapa, hivi haya yote ni matamshi ya Serikali au ya huyu Mheshimiwa saaaana Captain Kamanda Mkuchika?
 
Imetulia hiyo. Kwani wewe una shida gani na hiyo kauli kufananisha na Idd Amin? Of course wimbo wa Taifa amechemsha.
 
mashindano ya mpira hayawezi kufananishwa na vita, tena ya Nduli Idd Amin. Inaonyesha ukosefu wa sera kwa wale tunaosema ni mawaziri wetu. Majeshi ya Tanzania yalivuka kwenda kumchapa Idd Amin kwa kuwa alikuwa ni NDULI, MSHENZI asiye na heshima.

Sudani walikuja Tanzania kimchezo, na sisi tunaenda kwao kimchezo, sio vita.
 
I dont think it worth any critique!, alichokuwa anajaribu ni kuhamasisha tu, sasa kama hupenda the way alivyo fanya hivyo then that's non of our bussiness...hofu yangu ni kuwa we are trying to 'politicize' the thing!, lets leave FOOTBALL TO SPEAK FOR ITS OWN! (Ni mtizamo tu.....)
 
Back
Top Bottom