Mkopo wamkosanisha na mpenzi

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Kuna Jamaa ana mpenzi wake, wanakaa tofauti lakini wapo karibu sana. Jamaa anafunguo za nyumba ya mpenzi wake kwa hiyo asipomkuta hufungua na kukaa akimsubiria halikadharika na demu hivyohivyo. Sasa kasheshe imejitokeza kumbe jamaa alichukua kadi ya gari ya demu bila kumwambia kaenda kuchukulia mkopo yapata mwaka sasa. Na jamaa hali mbaya sasa ameshindwa kumalizia deni, watoa mikopo wamekuja juu wanataka gari tu. Hapo demu ndio amejua kumbe kadi yake ilitumika kukopa huo mkopo nae kaja juu ile mbaya na hamtaki tena huyo jamaa.

katika hali hiyo wa JF mnashauri nini?
 
Tutamshauri nini wakati dem hamtaki TENA mshikaji-kama vip aende ustawi wa jamii.
 
tabu ya kudate ma-opportunist ndio hiyo.

Mmmh, benk gani inayokubali collateral bila consent ya mwenye jina?? Labda kama alifoji kiapo cha huyu dada.

Anyway, wanasheria wapo awatumie.
 
kwani akimkataa ndo wakopeshaji hawataitaka hiyo gari!!wakae na jamaa watafute namna ya kumaliza mkopo,baada ya hapo kitakachofuata watakijadiri!
 
Huyo kwanza unapeleka polisi unaweka ndani! Halafu bank unawaambia kadi iliibiwa bila kujua manake huo ni wizi! Tena mkane kabisa kuwa ni rafiki tu tapeli! Insurance ya mkopo itafanya kazi!
Hata angekuwa mume wa ndoa ningemtoa na rambo yake kama zile za Smile na Fidel80! Mtu mwizi staki hata kumsikia! Uwiii!
 
Last edited by a moderator:
tabu ya kudate ma-opportunist ndio hiyo.

Mmmh, benk gani inayokubali collateral bila consent ya mwenye jina?? Labda kama alifoji kiapo cha huyu dada.

Anyway, wanasheria wapo awatumie.
Hakukopa Benki alikopa kwa watu binafsi
 
Story ya kutunga hiyo tena ya kusadikika, unawezaje kutumia kadi au hata hati ya mtu mwingine kuombea mkopo na Kampuni gani itafanya ujinga kutoa huo mkopo.Huyo msichana hana cha kuogopa adunde na gari lake mtaani na siku akija kukamatwa na hao ambao huyo kaka alikopa awaulize ni lini yeye kama yeye aliwahi kuomba mkopo period
 
tabu ya kudate ma-opportunist ndio hiyo.

Mmmh, benk gani inayokubali collateral bila consent ya mwenye jina?? Labda kama alifoji kiapo cha huyu dada.

Anyway, wanasheria wapo awatumie.

Like, like like ...
 
kadi ya gari iliandikwa jina la nani? la binti?

kama ni jina la binti benki waliikubali vipi hiyo kadi? maana kwa uelewa wangu benki wangeikubali tu kama huyo binti angesaini kuwa guarantee ya mkopo iwe gari yake?

na kama alikopa kwa mtu binafsi kama usemavyo then mbona ni simple sana? ashirikishe wanasheria na polisi ...ingawa napata taabu kuamini mtu binafsi amkopeshe third party bila consent ya mwenye gari.....
 
Kongosho na BADILI TABIA, hakukopa bank. Loan sharks wa mitaani hawana hiyana, unaweza kuweka rehani hata sufuria na blender! Yaani hiyo kitu kama imelogewa aisee, watu wanatapeliwa magari hivi hivi mjini.
 
Last edited by a moderator:
Story ya kutunga hiyo tena ya kusadikika, unawezaje kutumia kadi au hata hati ya mtu mwingine kuombea mkopo na Kampuni gani itafanya ujinga kutoa huo mkopo.Huyo msichana hana cha kuogopa adunde na gari lake mtaani na siku akija kukamatwa na hao ambao huyo kaka alikopa awaulize ni lini yeye kama yeye aliwahi kuomba mkopo period
ni story ya kweli , huyo demu ana jina la kilugha, kama Bumi, Gwantwa huwezi kujua kama demu au mwanaume. alitumia jina la demu kama jina lake
 
duh! ! ! !

Sasa hata huyo mtu binafsi yeye hakujiuliza?? Anakopa Yohana collateral Mariam??

Hapo bila msaada wa wanasheria atasumbuka.
jina la kilugha huwezi jua kama ni la demu au la
 
kama ndo hiyo nadhani msaada wa kisheria unahusika hapo.......
watachukuaje dhamana ambayo mhusika hajasign?

ila kama hela anazo akomboe tu gari lake........

walaahiiiiiii mwanaume wa namna hiyo unaweza kumchinj aisee.....

halafu abadili vitasa vya nyumba yake.....

Kongosho na BADILI TABIA, hakukopa bank. Loan sharks wa mitaani hawana hiyana, unaweza kuweka rehani hata sufuria na blender! Yaani hiyo kitu kama imelogewa aisee, watu wanatapeliwa magari hivi hivi mjini.
 
kama ndo hiyo nadhani msaada wa kisheria unahusika hapo.......
watachukuaje dhamana ambayo mhusika hajasign?

ila kama hela anazo akomboe tu gari lake........

walaahiiiiiii mwanaume wa namna hiyo unaweza kumchinj aisee.....

halafu abadili vitasa vya nyumba yake.....

Mke wangu umesemaje eti?
 
Back
Top Bottom