Mkopo wa Milioni 15.

Logo

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
588
48
Wadau,

Naombeni msaada, mimi nina business plan yangu bomba sana juu ya Social Enterprises Business. Nataka niwasaidie wanajamii na wanaDodoma kwa ujumla. Ukweli imepangiliwa vizuri na inakila kitu.

Sasa basi nahitaji mtaji wa Tshs 15,000,000/= ili nianze, je kuna shirika lolote linaloweza kunikopesha hizo pesa? Au je kuna kampuni au shirika lolote linalosaidia watu wenye vitu kama hivi?

Je, watakubali kukopesha bila kuwa na mali isiyohamishika? Maana sina nyumba, wala kiwanja wala gari1

Msaada Wadau!

Marry.
 
ngoja wadau waje kutoa majibu yenye kuweza kukupa msaada
 
Kuna thread inaelezea mikopo bila collateral. Jaribu kuitafuta hapa hapa business forum
 
Na uzuri wako mwanangu marry,
kweli kwenye miti hakuna wajenzi,
pole watakuja tu watakusaidia.
 
Unataka kufanya biashara gani?
Nimeelezea hapo juu nataka kufungua social enterprises ya media ambayo 1. Itakuwa inazalisha vipindi vya radio na Tv, 2. Itakuwa inazisaidia radio zingine kutoa ujumbe sahihi kwenye jamii kama vile kutoa mafunzo n.k, pia itakuwa inaomba grants kwenye mashirika ya umma ndani na nje ya nchi nayenywe inakuja inatoa fund kwenye radio mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya projects na mwisho itakuwa na kituo cha radio ya jamii.

Msaada wenu.
 
biashara gani!? jieleze vizuri

Hongera kwa Ujasiriamali,
- Vipi unataka kuendesha kama kampuni?
- au ni non profit business?

Make kama ni non profit business bank hawawezi kukupa mkopo, na kama ni non profi it means ucheki na mashirika yanayo toa grant and fund kwa NGOs.

- Na hayo mashirika mengi hayatoi mikopo make hayafanyi biashara yenyewe ni kutoa fund tu,

ILI UPATE MKOPO AU GRANT NI LAZIMA UWE UMEANZA HATA KIDOGO, NI VIGUMU SANA KUKUPATIA MKOPO AU FUND UKIWA NA PROPOSAL TU MAKE LAZIMA UONYESHE UNA BIDII NA BIDII SI KWENYE PROPOSAL
,
 
Back
Top Bottom