Mkopo wa milioni 10 CRDB

mm nilikopa nikanunua gari.....ni tofauti tu ya vipaumbele, taabu ya usafiri ilinishinda......

mbona fresh tu, kuna mtu kakopa gari na kila siku akienda kazini anakula vichwa na akirudi anakula vichwa pia,mafuta,matengenezo na hela ya kula anaipata hukohuko
 
Mkopo wa wa kiwanja ama kujenga unauma sana kwa kuwa huwa hauzalishi...ila kama unachanzo kingine cha mapato machungu yanapungua. Chukua CRDB si wabaya mimi nimekuwa nakopa hapo kwa zaidi ya miaka 6, kibaya ni pale walipoongeza kipengele cha mkopo kinachosema iwapo mdaiwa atashindwa kulipa deni lake lote muajiri atawajibika kulilipa.

Siku hizi mikopo inabima hivyo hakuna kuhofu saaaana. Kopa ukiwa na sababu maalumu maana kwa hii mishahara kusave had I pesa uitakayo huchukua muda saana.
 
Kama ukiweza kuinua biashara ili biashara ndio ijenge na kununua viwanja. Sasa hivi concentrate kutengeneza channel stable ya pesa kwanza
 
Mkuu ukichukua 8,00,000Tsh ukatoa 3,90,000Tsh unabakiwa na 4,10,000Tsh ambayo ni hela inayokupasa kutumia mwezi mzima kwa miaka mitatu,
sio tatizo unaweza kujibana kwa miaka hiyo mitatu, MKUU OMBI LANGU NI KUWA UTENDEE HAKI HUO MKOPO,
usijaribu kwenda kuweka heshima Bar na kutafuta dogodgo wa kukukanda asubuhi na jioni kwa hiyo hela utakayo itabikia kwamiaka mitatu
Hivi mwaka 2011 Mulugo alikuwa ameshakamata wizara ya ELIMU? Huo uandishi Wa tarakimu fedha ni Wa ki-Mulugo kabisa!!
 
Save laki 5 kila Mwezi kwa miezi kumi then fungua Biashara ambayo una uzoefu nayo,Baada ya hapo chukua Mkopo Benki Ikibidi zaidi ya Mil10 Ingiza kwenye Biashara yako.....!Baada ya Muda mchache utapata fedha ya kununulia Kiwanja, kujenga Nyumba, Kulea familia na nyingine za kula ujana..,

Kuwa mvumilivu Ndugu yangu ,Kumbuka mambo mazuri hayaitaji Haraka.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom