Mkono wa kulia wa marehemu waibwa -Hai

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20




Thursday, September 24, 2009 10:23 AM
KATIKA hali ya kushangaza kundi la watu lisilofahamika limeufukua mwili wa marehemu Daniel Invocavit (30) mkazi wa Kijiji cha Mbweera, Kata ya Masama Mashariki Wilayani Hai na kuchukua baadhi ya viungo kutoka kwenye mwili huo.


Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo na kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari walisema kuwa, tukio hilo lilitokea katikati ya mwezi huu na kwamba baada ya kufanya tukio hilo kundi hilo lilitokomea kusikojulikana.

Walisema kuwa, walipoamka alfajiri walishangaa kuona baadhi ya mifupa ikiwa juu ya kaburi hilo na kuwafanya wafanye uchunguzi katika kaburi hilo.

Walisema kilichowashangaza zaidi juu ya kaburi hilo walikuta kinyesi cha mbuzi hali iliyowafanya wahusishe kitendo hicho na imani za kishirikina.

Walisema Katika eneo hilo karibu na makaburi hayo hakukuwa na mbuzi hata mbuzi wa kufungwa na wala hakukuwa na majani ya kusema labda walikuja kulisha majani mbuzi huyo.

Baada ya kutaka kujua viungo vilivyochukuliwa katika kaburi hilo waligundua kuwa ni mkono wa kulia haukuwepo na kubaini kuwa watu hao walikuwa wameondoka nao.

Diwani wa Kata hiyo Allly Mwanga alithibitisha tukio hilo na alisema kuwa marehemu aliyekuwa amezikwa katika kaburi hilo aliuawa mwaka jana na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuwa ni jambazi sugu


</SPAN>
 
Back
Top Bottom