Mkono asalimu amri baada ya kukatwa wazazi CCM

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Hatimaye Mzee Mkono amekubali matokeo na kunywea baada ya panga kumpitia

Mmoja ya watu walijitokeza kugombea uenyekiti kupitia jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi-Taifa, Nimrod Mkono, amesema anaunga mkono kwa asilimia mia moja maamzi yote ya vikao vya uteuzi wa wagombea.

Alisema kuteuliwa yeye hakuna maana kuwa kuna jambo limekosewa bali ni taratibu za chama na kwamba kwa asilimia mia moja anaunga mkono uamuzi huo ambao umefanywa katika vikao mbalimbali vikiwemo vile vilivyokuwa chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete jana.

“Mimi ni Mwana-CCM damu. Ninaunga mkono uamuzi wa chama changu tena kwa asimia mia moja. Walioteuliwa ni WanaCCM wenzangu. Ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa kutosha hadi tutakapo pata mmoja wetu kuwa kiongozi wa Jumuiya yetu,” alisema Mkono.

Kuhusu kauli yake kuwa endapo hatapitishwa jina lake “hapatatosha” ndani ya CCM, a lisema kauli ile, “Nilisema sikubaliani na yale yaliandikwa kwenye magazeti kwani wakati mchujo unafanyika sikuwepo hivyo huwezi kusema nilikuwa wa mwisho wakati hata sikuwepo, ndiyo maana nilisema sikubali kama kweli imekuwa hivyo kwa kuwa sikuwepo ila nilijua uamuzi ninaoungoja ni wa vikao vingine na uamuzi umefanyika kwa haki na nimeridhika bila kinyongo, hivyo ni wajibu wangu kukisaidia chama changu,” alisema Mkono.

Aidha, kuhusu kauli ya mwenyekiti wake wa Taifa kuwa watakaoshindwa kupitishwa watakihama chama hicho na kuwataka waende mapema, alisema hiyo ni kauli ya kiongozi wake ambayo yeye hajawahi kuitoa popote wala kutoa vitisho vya namna hiyo kwa chama chake

Kwa hiyo hapachimbiki?atulie tu atapata mali hata kama hatokuwa kwenye nec, sisiemu ni sehemu ya kujipoatia mali.
 
Ukisikia mtu kula mata ..shi yake mwenyewe, ndiko huku!, ila pia kwa vile we have 3 more years to come mpaka 2015, wapiganaji makini wote, husubiri mpaka "the most oportune moment" ili wa hit, na wakati ukifika, at hit hard with a big blow where it hurts most!. Kanda nzima ya Ziwa gone!.
P.
 
Huyu mzee tayari nilishamdharau baada ya ile kauli yake kwamba "patachimbika" endapo asingepitishwa!
 
Kwa hiyo hapachimbiki?atulie tu atapata mali hata kama hatokuwa kwenye nec, sisiemu ni sehemu ya kujipoatia mali.

Huyu Mkono hafai kabisa kwa lolote. Alidhani CCM watamtetemekea na mihela yake. Amepigwa panga mchana kweupeee na akanywea. Nilijua hawezi kufanya kitu, maana atawezaje kukisumbua chama ambacho kila kukicha anakula mihela ya burebure kupitia kesi zisizoisha za BOT, TANESCO na Wizara nyinginezo? Akiondoka tu wanakata mrija huo tuone kama atajenga hata darasa moja huko kwao. Firm yake itapotea kwa upesi kama alivyopotea Lamwai.
 
Pasco
CCM ni chama cha kidemokrasia na kinafanya maamuzi yake kwa taratibu zake unashangaza sana unaposhabikia siasa za ukanda CCM ni wamoja hakuna ubaya kwa mzee Mkono kukubali maamuzi ya chama hiyo ni haki yake kama mwanaccm,kamanda siasa za ukabila na ukanda zina mji wake
 
Last edited by a moderator:
niliwahi kusema huyu mzee anatishia nyau, na anazeeka vibaya! ufisadi na ubadhirifu alio nao hana guts za kujitoa ccm, anashangaza kusema kuwa yeye ccm damu huku alisaini hoja ya kumn'goa waziri mkuu wa chama chake ! mizee kama hii isiyo na msimamo inapaswa kufungwa jiwe la kusaga shingoni na kutoswa baharini!!
 
Ha haa, ilijulikana toka mwanzo tu kuwa lazima atasalim amri! Chezea maamuzi magumu wewe!
 
niliwahi kusema huyu mzee anatishia nyau, na anazeeka vibaya! ufisadi na ubadhirifu alio nao hana guts za kujitoa ccm, anashangaza kusema kuwa yeye ccm damu huku alisaini hoja ya kumn'goa waziri mkuu wa chama chake ! mizee kama hii isiyo na msimamo inapaswa kufungwa jiwe la kusaga shingoni na kutoswa baharini!!

Kweli kazi anayo
 
Akubali tu kwamba ile kauli ilimponyoka. Haya mavyama ya ukombozi as long as yako madarakani, kama na wewe ni member unapaswa kuwa mpole. Wala haichukui juhudi kubwa kukumaliza, we all have some dirt under our carpets. Angalia ya Julius Malema, kutoka head wa Youth League mpaka mtuhumiwa wa Money Laundering, Corruption etc. Mkono is not stupid.
 
Ukisikia mtu kula mata ..shi yake mwenyewe, ndiko huku!, ila pia kwa vile we have 3 more years to come mpaka 2015, wapiganaji makini wote, husubiri mpaka "the most oportune moment" ili wa hit, na wakati ukifika, at hit hard with a big blow where it hurts most!. Kanda nzima ya Ziwa gone!.

:ranger:
 
When AN OPPORTUNE TIME comes before 2015 , Mkono will hit them so hard they will never recover; he knows the magamba party weakness is in the till.
 
Back
Top Bottom