Mkono akubali kufukuzwa CCM!

Kuna mwanga unaanza kupatikana..nadhani ni vema sasa tumuongeze Mkono katika ile list ya wabunge wa CCM walioomba kuwekewa nafasi CHADEMA.

Pamoja na hatua hiyo murua ,ningepeda kuona Mkono & Filikunjombe wakijitoa CCM.
Kudai tu kuwa wapo tayari kufukuzwa haitoshi!maana ya kauli zao ni kuwa,hata kama wao wakiendelea kuweka mazingira ya kufukuzwa ,kwa kutoa matamshi ya "kuwakera" wenye chama na ikatokea wenye chama chao wakaogopa kuwafukuza,wao watachagua kuendelea kubaki CCM!No!

Kama kweli wao ni Wanamapinduzi wa kweli hawana sababu ya kusubiri kuondolewa katika chama,badala yake,waondoke wenyewe kutii dhamira zao.
 
Nyerere is raising from the grave! Kwamba upinzani wa kweli utaibuka baada ya CCM kubomoka.

Sasa pasuko la tetemeko ndani ya chama ni zito! Watu hawaogopi kusema wakifukuzwa wanahamia chadema wanarudi bungeni kama kawa.

Kuridhisha ni wananchi na is chama sasa!
Eti kazee kawatu walikasingizia magonjwa makubwa na ya aibu!! Tunataka post moterm yake iwekwe wazi!
 
anguko la CCM limefika mkapa ajiandaee tu, maana mimi nataka lile tofali la dhahabu alilopewa
 
Kinachonishangaza kama huu ulikuwa ni msimamo wa wabunge wa CCM, Zitto anaingiaje kwenye hii movie??

Ninavyojua hawa jamaa CCM sikuzote hawataki kuona wapinzani (CHADEMA) wakilamba mali mahali popote. Ilikuwaje wakakubaliana na hoja ya Zitto? Na Filikunjombe anasema hii ilikuwa inakusudia kuinusuru serkali na chama chake!!!

Je Zitto alikuwa na taarifa kabla? Au alijua agenda hii hatimaye itaijengea heshima CCM na Mkulu JK?? Au ni coincidence?

Nisaidieni mawazo jamani.
 
ccm ni chama cha kifisadi,ambacho kinalazimika kuwa kama mafia ili kudhibiti maovu yao na dhambi wanazofanyiwa wananchi dhidi ya wafadhili wao
 
Kinachonishangaza kama huu ulikuwa ni msimamo wa wabunge wa CCM, Zitto anaingiaje kwenye hii movie??

Ninavyojua hawa jamaa CCM sikuzote hawataki kuona wapinzani (CHADEMA) wakilamba mali mahali popote. Ilikuwaje wakakubaliana na hoja ya Zitto? Na Filikunjombe anasema hii ilikuwa inakusudia kuinusuru serkali na chama chake!!!

Je Zitto alikuwa na taarifa kabla? Au alijua agenda hii hatimaye itaijengea heshima CCM na Mkulu JK?? Au ni coincidence?

Nisaidieni mawazo jamani.

Iko hivi mkuu; wabunge wengi wa CCM ni mbumbumbu na wengine wanatumia uzoefu tu kwa sababu lakini ni kwamba hawana kasumba ya kusoma. Kwa kipindi hiki ambacho CDM wamepeleka wabunge wengi ndo tumeona hoja motomoto bungeni. Hivyo wabunge wa CCM ambao hawana maamuzi binafsi wanatumiwa tu, hawafai kuwa viongozi kwa kipindi ambacho tunahitaji mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa.

Baadhi waliochangia bila kufikiria walijikuta wametumiwa vimeseji - wakaheshimu wakubwa wao na kurudi nyuma kukataa kusaini fomu.
 
Wameshaanza kupayuka wenyewe watatueleza vizuri walimuulia nini baba wa Taifa. Haya mambwa haya ni ya kunyonga yote hadharani
 
huyo fisadi hana maana kabisa, ni mwongo na anaingia kwa mlango wa nyuma....huyo hapo na chenge ndio wanaozuia ile sheria ya anti money laundering isiwe na vipengele vya kufilisi mali za mafisadi sasa wakiwa hai au itakapogundulika baada ya wao kufa...kuna mapungufu mengi kwenye sheria hii na kwenye marekebisho ya sheria, mojawapo ya watu wabaya wanaopinga harakati za kufikia sheria nzuri ni mkono..kwa ufupi, mkono, chenge na wengine wapo kwenye kundi moja la mafisadi wanaopambana kwa kina kona kulinda maslahi ya mafisadi, na kwasababu yeye anajiona mwanasheria, basi wanamtumia vilivyo...hana maana, tumkatae kama ukoma huyu.
 
Hongera Mheshimiwa Nimrod Mkono kwa hili nakuunga mikono na miguu mna ni viongozi wachache wenye roho kama yako uzi huo huo usitetereke hata kidogo....karibu sana kwenye chama chetu cha CUF kma upo tayari......
 
Hongera Mheshimiwa Nimrod Mkono kwa hili nakuunga mikono na miguu mna ni viongozi wachache wenye roho kama yako uzi huo huo usitetereke hata kidogo....karibu sana kwenye chama chetu cha CUF kma upo tayari......


Mkono hawezi kujiunga CUF ambayo inakufa sambamba na Muungano. Mkono anajiunga Chadema, chama chenye mwelekeo wa ukombozi mpya baada ya kuua fikra za Nyerere!
 
Kuna mwanga unaanza kupatikana..nadhani ni vema sasa tumuongeze Mkono katika ile list ya wabunge wa CCM walioomba kuwekewa nafasi CHADEMA....
Keshaondolewa kwenye ile orodha maarufu ya mafisadi Mwembeyanga?
 
Hapo patamu tunasubili ukombozi na watatafuta nafasi wakati tumeshajaa njooni mapema mliowasafi.
Mkono na wenzake hawatafukuzwa kwa sababu za kutia sahihi ya kutokuwa na imani na Pinda.Ukiwafukuza unatangaza vita na wananchi.Labda CCM wabuni njia nyingine ya kuwatafutia kosa.Lakini sidhani kama wao wataamua kuondoka CCM,bado kuna maslahi binafsi wakikaa CCM.
 
Filikunjombe CCm Unajilazimisha tu. kama ni haki wewe ulistahili kuwa waziri. ila kwasababu hufanyi mambo kwa maslahi ya chama uwaziri umenyimwa.

Viva Filikunjombe. CDM tunakusubiri kwa hamu kubwa, huko ndio kwako bana.
 
Keshaondolewa kwenye ile orodha maarufu ya mafisadi Mwembeyanga?

Ndugu Gagnija,sina taarifa kuhusu 'status' yake kwa sasa.
Sidhani,hata hivyo,kama hicho ni kikwazo kwake kupokelewa CDM.
Kama alivyopata kutamka Mwenyekiti wa chama ,watu wa aina hiyo,watakubaliwa katika chama upon 'vetting ' na 'utakaso'.Sasa.Kupita ama kutokupita katika mchakato wa 'vetting' &'utakaso' hilo lipo mikononi mwa chama.
Nilizungumzia uwezekano wa Ndugu MKono kujiondoa CCM na pia na uwezekano wake kuvaa GWANDA.
 
Kama wanakubalika hata wakivua gamba wanaweza kuwa wagombea binafsi iwapo katiba mpya itakuwa na hicho kipengere!
 
watu wanaanza kujikosha taratibu..cdm ingekua sio imara kama chama cha upinzani sidhani kama wabunge wa ccm wangekua na nguvu ya kuongea hadharani..sasa hivi wanajua wakivuliwa gamba....wanavaaa???....
 
Back
Top Bottom