Mkongo wa mawasiliano mikoani tutegemee nini?

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Imefahamika kwamba mradi wa mkongo wa mawasiliano wa kimataifa utakamilika na kuunganishwa na mtandao wa ndani kuanzia mwezi ujao. Kwa kuanzia mikoa minane itaunganishwa na kupunguza gharama za kupiga simu na kutumia internet kwa 50%.

Ningependa kufahamu kama hizo gharama za kupiga simu na kutumia internet zitapungua kwa kwa mikoa hiyo tu au na kwa mikoa nje ya hiyo minane.
 
Usambazaji wa mkongo wa mawasiliano unatarajiwa kukamilika kwenye mikoa na wilaya zote hapa nchini ifikapo mwezi wa tatu 2012
 
Mi naona kama issue hii ipi kisiasa siasa tu, sioni lolote na kama lipo ni kwa kiwango kidogo sana kiasa kwamba you cant feel
 
Mimi nilishauliza sana humu habari ya huu mkongo. Niliwahi kujibiwa kwamba gharama za mawasiliano zimeshashuka sana kwa kulinganisha na miaka michache ilopita kutokana na mkongo! Sasa maelezo yanachanganya kabisa! Mara zilishashuka, mara zitashuka- which is which! MWENYE UWEZO WA KUTUELIMISHA VIZURI KUHUSU HILI JAMANI AJITOKEZE KATIKA JUKWAA HILI MAKINI. NAJUA MPO!
 
so far huu mkongo wa taifa upo karibu mikoa yote na TTCL ndio mwenye jukumu la kutoa service kwa yeyote atakaehitaji...makampuni yote ya simu yameshajiunga huko kwa namna moja au nyingine ni vile sio rahisi kutambua na watanzania wanatumia pia bila kufahamu...cha msingi hili suala limegeuka siasa kuliko uhalisia wenyewe..mkongo sjui mkonga ni just barabara pana ambayo mtaitumia kupitishia data zenu whether internet or whatever....cha muhimu kujiuliza ni ww ukiwekewa huo mkonga what are u going to inject to create the trafic au ndo tutaishia na traffic ya 100kb ya jf na fb...watu wahamasishwe kutumia internet applications....maofis na mambo mengine km ayo....kuna sehhmu wana iyo fiber na hawana cha kupitisha zaidi ya facebook na yahoo....:behindsofa:
 
Walisema benefits za huo mkongo/mkonga ni pamoja na kuongezeka sana kwa kasi ya kusafirishia hivyo vitu, eidha kwa ku upload au ku download! Sasa kwanini basi at least tusione mapinduzi makubwa ya hiyo speed?? Actually I dont see the distinct difference ya speed niliyokuwa natumia mimi some 3 years ago na sasa!
 
Walisema benefits za huo mkongo/mkonga ni pamoja na kuongezeka sana kwa kasi ya kusafirishia hivyo vitu, eidha kwa ku upload au ku download! Sasa kwanini basi at least tusione mapinduzi makubwa ya hiyo speed?? Actually I dont see the distinct difference ya speed niliyokuwa natumia mimi some 3 years ago na sasa!
Mkuu nchi hii kila kitu kinafanywa kisiasa hakuna muongozo kwa wawekezaji namna ya kuwabana, kisingizio biashara huria, na watoa huduma hii ni wamoja kuliko tunavyofikiria, wapo hapa kutafuta huge profit, kama tume ya mawasiliano haita simamia hili eti tusubiri balancing ya soko kushusha bei tusahau, na hata kama inashuka ni kwa kiasi kidogo mno hata huwezi kui feel,
Watawala wanaishia kupanda majukwaani kwa mbwembwe eti tumefanikisha kuleta mkonga sana unawafaidisha hao wawekezaji na sio sisi end user
 
Back
Top Bottom