MKOBA azushiwa kusaini kitabu cha mahudhurio

Status
Not open for further replies.
Kiongozi wa chama cha walimu (CWT) ametajwa kuweka sahihi yake katika kitabu cha mahudhurio ili kuepuka adhabu. Huu ndio usanii wa walimu na mgomo wao feki.

Source: Magazeti asubuhi hii

Hivi hicho kitabu kiko wapi? Kwani jamaa anafundisha?
 
wewe acheni propaganda zenu atasaini nini na wapi hali yeye si mtumishi wa umaa? Acheni uvivu wa kufikiri!
 
Hii kama ni kweli basi inatakiwa kuona ni jinsi gani watu hawa walivyo wanafiki na wazandiki! Hii ni kuwachuza wale anaowaongoza....kwanini akasaini ikiwa wamekubaliana kugoma?!

Ina maana, ikiwa serikali itaamua kuchukua hatua; yeye aseme "sikugoma, si mnaona hata kwenye kitabu cha mahudhurio nipo!" Kama ni kweli, basi huyu mzee Ni Kenge Mzee ndani ya msafara wa Mamba Vijana!! Huu ni usaliti wa hali ya juu!

Usaliti ambao walimu wanapaswa kufahamu wazi kwamba, wao wametangulizwa mbele kama ngao! Hakika; kama walimu wangekuwa wanafahamu wanachokifanya, basi wangekutana mapema iwezekanavyo na endapo itabainika ni kweli Mukoba amesaini kitabu cha mahudhurio basi wampige chini bila kuchelewa. Yeye alitangaza wazi kwamba walimu wote wabaki nyumbani; sasa amesaini vipi wakati yupo nyumbani?!

Hofu yangu nyingine ni kwamba, habari hii inaweza isiwe ya kweli....inaweza isiwe kweli kwamba Mukoba amesaini. Lakini kama kweli amesaini, basi anastaili kuondolewa kwenye nafasi yake bila kusubiri!
 
hakuna kitu kama hicho hawezi akawa amesaini,kwani ye haogopi walimu wa sasa sio wa miaka ya 47,na kama amefanya hivyo cha moto atakiona.
 
Anawezaje kuongoza wanaofundisha kama yeye hafundishi. Ni Mwalimu wa Ben Mkapa Sec. School.

Hebu walimu watujuze kuhusu nafasi ya Mukoba ndani ya CWT. Je nafasi yake inatokana na sharti la kuwa mwalimu? Hii inawezekana maana nafasi ya ajira ndani ya cwt ni ya Katibu, huyu ndo tunapaswa kusema hana mahali pa kusaini. Kama kweli ni mwl kwenye shule ya Sir. Ben Mkapa (O.B.E) Je! Shule hiyo ni ya Serekali ya magamba au binafsi? Maana shule za binafsi zinadunda mzigo kama kawa
 
Gazeti la habari leo-la serikali Dhaifu....!
Mi naamini wamezingua tu hili gazeti,naamini kwenye hiyo shule hayupo pekee,naomba anaefanya kazi na MKOBA shule moja atuambie kuwa jamaa alifika...Gazeti la uhuru na habari leo waache usanii..Waalimu waendelee kukaza tu.
"Vox populi,Vox dei"
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom