Mkoa wa Mbeya ndio nchi ya ahadi?

Hakuna kitu huko ndo tunaskia wanauwana kwa uchawi
Mchungaji kakamatwa na viungo nya albino
Uchunaji ngozi ulianzia na unaendelea huko mbeya hakuna cha nini wala nini
Na wengine wamehamia hapa town karibia wote hawa mitume
Manabii
Miungu

Wakina lusekelo hawa ni wa huko mwakaleli
By the way hiyo ni biashara yao wanayoona inalipa period isifananishwe na imani
 
Wanabodi,

Kwanza naomba nisieleweke kuwa sina nia mbaya na hayo Makanisa, bali naomba kujua nini hasa chanzo cha mkoa wa Mbeya kuwa na Makanisa mengi ya waumini wa madhehebu ya dini. Pia hata waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatoka mkoani Mbeya, hivi nini chanzo?

Elimu haina mwisho..

Sababu kuu ya wingi wa madhehebu kwa mkoa wa mbeya ni kukosekana ama udhaifu wa madhehebu makubwa ya kikristo yaani Roman Catholic, Lutherani na Anglican. Haya madhehebu yalichelewa sana kufika mbeya na kukuta wenzao wa Moravian wameshatawala eneo kubwa sana la huko mbeya. Kanisa la Moravian linashabihiana sana na makanisa ya kilokole yaani kipentekoste. Makanisa ya kipentekoste hujulikana kwa wachungaji wao. Hivyo wengi walioshika dini sana mbeya walijikuta wanaanzisha makanisa yao mahali wanapokua. Hali kama hii haipo kwa mikoa ambayo ni ngome ya makanisa makubwa mfano. mwanza - RC, Songea - RC, Sumbawanga - RC, Arusha - Lutheran, Dodoma - Anglican, Bukoba - RC.

Pia wanyakyusa wana vipaji sana hasa uimbaji. Kama unyakyusani ingekua ngome ya RC tusingewasikia sana wakitoa nyimbo au kuwa wachungaji kila sehemu wanapokua. Madhehebu hayo mengine (ya kilokole) yanathamini sana nyimbo na ni sehemu kubwa sana ya ibada zao, ndio maana vipaji hivyo hukua kirahisi kwa mkoa wa mbeya.
 
Nakushukuru sana kwa kuniongezea material kichwani mwangu mkuu
 
Kukiwa na abiria wengi na mabasi yanakuwa mengi, kukiwa na waovu wengi makanisa yanabidi yawe mengi........Hata manabii wengi walikuwa wakitokea Mashariki ya kati na ndiko kulikuwa na maovu mengi.
 
ni mpango wa Mungu mbeya kuwa na makanisa mengi.kwa africa ni jiji la pili ukiachia mbali lagos.Muugu ana mipango mingi sana na huuu mkoa.mfano kumleta sugu kuwa mbunge,wananchi wake kujitambua na kuikubali CDM.SIO HIVYO WATU WAKE WENGI WANAONEWA SANA.kIBANDA tindikali,Mwangosi aliuwawa,Mwakyembe sumu,ulimboka kucha.vilevile ni mkoa uliye na mbunge kilaza kuliko wote bwana mlugo,alidiriki kusema tanzania na muungano wa tanganyika na zimbabwe.Mipango yake mola haina makosa .home mbeya home
 
Unaijua idadi ya waumini ya makanisani hayo?
La msingi wote wakristo tu. Haijalishi madhehebu maana biblia ndio hiyo hiyo.

Je unaweza kutofautisha msikiti wa Shia na Sunni? Au wote kikubwa ni Waislamu tu?
 
Duu,hii tena kali kuliko zoote,hivi mlugo ki utendaji yuko wapi siku hizi?
 
Unaijua idadi ya waumini ya makanisani hayo?
La msingi wote wakristo tu. Haijalishi madhehebu maana biblia ndio hiyo hiyo.

Je unaweza kutofautisha msikiti wa Shia na Sunni? Au wote kikubwa ni Waislamu tu?

Acha kudanganya wewe nani kakwambia shia ni waislamu!
 
Wanabodi,

Kwanza naomba nisieleweke kuwa sina nia mbaya na hayo Makanisa, bali naomba kujua nini hasa chanzo cha mkoa wa Mbeya kuwa na Makanisa mengi ya waumini wa madhehebu ya dini. Pia hata waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatoka mkoani Mbeya, hivi nini chanzo?

Elimu haina mwisho..

Ni kwa sababu MBEYA tuenda na matukio na si kwa akili zetu hebu angalia mwitikio wa vyama vingi kwa sasa hakuna chama hakina mfuasi mbeya
 
Back
Top Bottom