Mkoa wa Kinondoni kanda ya Dar es salaam CHADEMA watoa tamko kali sana kuhusu Lema kuwa magereza

Nadhani ni wakati wa kuamka na kusema no kwa kila tendo baya la CCM..Muheshimiwa Lema kaonyesha kuwa inawezekana kabisa kutetea haki kwa njia yoyote ile....
 
Dr. Slaa please toa RUKSA tuwashe moto tz nzma, vijana mwanza na shy tupo tayari. Tumechoshwa
 
Haki ndio chanzo cha amani na utulivu na upendo kati yetu. Serikali ya chama tawala inapoanza kutumia nguvu za dola ambapo hata hapahitajiki ujue imekosa dira, inatapatapa, haina sera, haina matumaini na ya kwamba inategemea nguvu za dola kuishi na siyo ile ya wananchi. Matokeo yake chuki, kutokuaminiana, na ubabe. Hizi ni dalili za nyakati kuwaendea kombo CCM na ya kwamba jua linazama kuashiria kuwa wanakwisha kadri siku zinavyoenda. TUSUBIRI TANZANIA UPRISING tuombe tu iwe ya amani. Mungu ibariki TZ
 
Haka kweli sasa hii ni aibu.... amekuja makamu mwenyekiti UVCCM arusha akafanya na maandamano kufungua matawi ikawa ni sawa...

hawa siyo hata wamefanya maandamano ila ni hali tu ya vijana kumpa tafu kamanda wa mapinduzi... inakuwa shida....

ila wakumbuke WHAT GOES AROUND COMES AROUND...
 
Nadhani ni wakati wa kuamka na kusema no kwa kila tendo baya la CCM..Muheshimiwa Lema kaonyesha kuwa inawezekana kabisa kutetea haki kwa njia yoyote ile....

Wakati wa kuamka uku umejificha kwenye Laptop jitokeze ingia barabarani ukutane na polisi
 
tz yenyewe haina hata mapango yakujificha,
kama hayatakuwa yaleyale ya gaddaf kubana kwenye kahandaki, sijui.
 
MUNGU atuokoe bomu hili wanalolitengeneza.Hawataweza kuirudisha imani ya wananchi juu ya hiyo serikali yao kama wataendelea na tabia hii.

Nchi ina matatizo mengi kama ukame,ukosefu wa maji kwenye maeneo mengi,uhaba wa chakula,mfumuko wa bei,ufisadi ,ajali za kila siku,bidhaa mbovu(Counterfeit Product) kutoka nje ya nchi,madawa feki, huduma mbovu za afya,elimu,ukosefu wa ajira,umeme migogoro ya ardhi,ujambazi,mauaji ya albino,ukosefu wa miundo mbinu kama barabara na mengine mengi mfano hayo yanayozunguka maeneo unayofanyia kazi au kuishi.
Muda na nguvu zinazotumika kuwafanyia ukatili viongozi wa wananchi (CHADEMA) na wapinzani kwa ujumla ni bora wangezitumia kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili kama taifa.

Hii itakuwa kiama kwa nchi.Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema ''Mkiendeleza tabia hizi za kuwabagua kwa sababu wao sio wenzenu(adui zenu),wakishajitega mtaendelea kubaguana wenyewe kwa wenyewe'' Haya yameshaanza kujitokeza;kuwekeana sumu reffer kauli ya J Kikwete ''Hatuaminiani,Hauwezi hata kuacha glass ya maji ya kunywa ukayakuta salama'' yuko wapi Mwakyembe na Mwandosya,kuvuana MAGAMBA, uadui usiokwisha,fitina za kila aina Ole Millya v/s Ole Sendeka.

Vijana lazima tulikomboe taifa letu bila kujali itikadi.Huo ni mpango wa mafisadi kutugawa ili waendelee kuneemeka.Wakishatuibia rasilimali zote wataondoka watatuachia nchi yetu ukiwa haina chochote.si mnasikia na kuona kila siku wanashutumiana kwamba mgombea fulani si rai wa nchi hii na sasa wanataka urai wa NCHI MBILI ili iwe raisi kwao kutoroka.
Vijana,wazee,watoto tuamke...tutetee TAIFA letu hatuna pa kukimbilia.Tusiwaachie hao wanyang'anyi TAIFA letu.Lets fight for our freedom.
Lema na Makamanda wengine wameshatuonesha njia,sasa ni muda wa kamua.Tunalipenda TAIFA letu au hatutaki liendelee kuwepo.
viva CHADEMA.
Mkuu "'CCM leo Mtawanyanyasa Chadema,si hao tu wanaoteseka na ugumu wa maisha ya tanzania,tupo wengi Walaka wa Lema umenisikitisha na kunitoa Machozi Azimio la Arusha lilizaliwa Arusha 1967,na mapinduzi dhidi ya serikali iliyojiweka madarakani chiniya tume feki ya uchaguzi JK kama kweli ulichaguliwa na watanzania mbona umewaacha wanahangaika na ugumu wa maisha,kupanda kwa bei za vitu,kushuka kwa Shilingi dhidi ya Dola ya marekani,Mbona hutoi hata maelezo kwanini hali iko hivi,kila siku upotevu wa fedha za uma unaolipotiwa huchukui hatua hata ya kuwawajabisha wahusika .kwanini tusiamini lenu ni moja,Wanyama wametoroshwa KIA wewe kimya kama hakuna kilichotokea,Wafanya biashara wanapandisha bei za bidhaa wee kimya ,huoni?,Husikii ? hata Mkeo hakwambii haya hata wanao pia hawakwambii.maana inawezekana sisi hutaki kutusikia kwani kila mmoja afe na lwake.JK umeamua kutuchinjia baharini? wale wabuge waliokuwa wanatusemea Bungeni wanaumwa sijui wala sitaki kuamini nichosikia mitaani ,lakini kwanini waugue pamoja ghafla Dr Mwakyembe,Zitto,Mwandosya bado wengine wanakamatwa kila siku,Hutaweza kuzuia nguvu ya Umma utawanyamanzisha wachache tu,Hata nyie NEC Hamuoni watanzania wanavyoishi kwa shida leo mnadhani wakichoka mtasaidiwa na hao wanaowalinda.ole wenu .Mheshima LEMA TUPO PAMOJA INYESHE MVUA JUA LIWAKE HAKI YA KWELI ITAPATIKANA.ARUSHA ALUTA CONTINUA MAPAMBANO YANAANZIA HAPO.
 
kamanda kilewo kwenda kumtembelea lema magereza leo amewasili usiku wa jana baada ya kutoa tamko dar, tumebahatika kupiga story jamaa yupo for real na anamkubali Lema ile mbaya, kilewo jisikie uko nyumbani maana umekulia hapa hapa, A town.
 
Huyo OCD wa Arusha anadhani hatakufa au anapata wapi kiburi hiki? serikali ya ccm ni legelege na haina uwezo w kuhimili hasira ya watanzania wanayozidi kuikusanya. Lakini sishangai kuona mtu huyu anafanya haya na hakuna anayemkemea, maana waziri na AGP wote hawana uwezo wowote kuongoza wizara hiyo na uwezo wao wa kufikiria ni mdogo mno. Maana wandhani police na jeshi wanaweza kuwalinda, kama hivyo Gadaf angekuwa madarakani maana alikuwa na jeshi imara, kwa vitendo hivyo vya Arusha vinaonyesha mwisho wa serikali ya JK umekalibia. Tuko pamoja na wote wanaotaka haki, hatuwezi kutishwa na kundi dogo watanzania zaidi ya milioni 40.
 
Wakati wa kuamka uku umejificha kwenye Laptop jitokeze ingia barabarani ukutane na polisi

hivi hawa polis wa Tanzania wana nini cha ajabu kuwazidi wale wa Tunisia, Misri na Libya??? Polisi wenyewe ndo hawa hawa vitoto vyao vimejazana "shule" za kata au ni wengine??? ndiyo hawa hawa nawaona wanatembelea viatu soli upande sababu ya wizi na ufisadi wa ccm???? au????!!!! polisiiiii polisi, utafkiri wewe na kale kamke kako mwaishi msumbiji na si tanzania!!!!!!!....tumbafu sako.....
 
kama walidhani kumpeleka jela kungezima mapambano ya Mh Lema, wameshindwa moto umeongezwa petrol,
 
hii nchi imeshakuwa kama nchi ya KUSADIKIKA tunakolekea ni kuvaa mabovu tu na kujitoa mhanga zidi ya uonevu huu ccm nyny cyo miungu m2
 
hali ya Arusha mitaani siyo shwari kila mtu anataka kuwa shahidi ya kuwa zuberi alitukana .
 
Mkoa wa Kinondoni kanda maalum ya Dar es salaam umetoa tamko kali sana leo walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho zilizopo maeneo ya mwananyamala ujiji.

Tamko hili hapa.



MKOA WA KINONDONI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

Tamko la katibu wa mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam

kilewo.jpg


Ndugu zangu wanahabari

Nimewaita hapa leo kwa lengo la kuwapa watanzania msimamamo wangu na wa chama ngazi ya mkoa kuhusu tukio la kukamatwa na kupelekwa magereza kwa Mhe. Godbless Lema Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini.

Imekuwa ikizoeleka kwa muda mrefu sasa kwamba waheshimiwa wabunge wa CHADEMA na wale wanaaotokana na vyama vya upinzani wamekuwa wakinyanyaswa sana kwa lengo la kuwafanya wajute kuingia katika siasa za upinzani Tanzania.

Hii kwa CHADEMA haitokei tu kwa waheshimiwa wabunge bali hata kwa viongozi wa ngazi zote. Inaonekana kuwa sasa serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeamua kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuwatesa kwa siri na kwa wazi wale wote wanaoipinga siasa kandamizi na zisizowalazimisha watawala kuwajibika kwa wananchi.

Mkakati huu umetungwa na CCM, unasimamiwa na usalama wa taifa na unatekelezwa na jeshi la polisi. Kwa hakika hatuhoji tena kwamba jeshi la polisi ni kitengo cha kusimamia maamuzi na maelekezo ya CCM badala ya kulinda raia na mali zao.

Mheshimiwa Godbless kama mbunge wa wananchi wa jimbo la Arusha Mjini amekuwa akifuatwafuatwa na jeshi la polisi kila mara na kufanyiwa vitendo vingi vya udhalilishaji na unyanyasaji hasa kwa kupitia OCD wa Arusha Mjini Zuberi.
Mathalani wiki iliyopita siku ya ijumaa tarehe 28/10/2011 Mhe. Godbless lema akitoka mahakamani alisindikizwa na wananchi wake kutoka mahakamani hadi ofisini kwake. Wafuasi wake walipomfikisha ofisini waliondoka na kurejea makwao. Huko ofisini aliwakuta wananchi wakimsubiri ili awahudumie kama mbunge wajimbo lao. Wakati akiongea na wananchi ghafla polisi walifika na kuwakamata wananchi wote waliokuja kuomba usikivu wa mbunge na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi.

Mbunge Lema alipokwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea dhamana naye aliwekwa chini ya ulinzi kwamba eti amefanya maandamano bila kibali.

Tunahoji: Ni maandamano yapi hayo ambayo Lema aliyafanya na wananchi wake akiwa angali ofisini kwake? Je maandamano wanayoyazungumzia ni kuondoka na wananchi mahakamani hadi ofisini kwake? Je kama kuondoka kwake na wafuasi wake mahakamani ni kosa kisheria; Je kwa Mhe Ole Sendeka alipokuwa akitoka mahakamani, alikuwa akiondoka na kundi kubwa la wafuasi wake na kusindikizwa na OCD huyu huyu? Vile vile Mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Arusha amekuwa akienda kituo kikuu cha polisi akisidikizwa na kundi kubwa la wafuasi wake wa CCM. Polisi hawakuwahi kuwakamata wala kuwaonya. Sasa haya yote yalikuwa maandamano ama matembezi ya hisani? Maana Arusha kuna msiba mkubwa wa CCM kukataliwa na wananchi.

Kwa hakika tukio la kukamatwa kwa Mhe Lema, kupelekwa mahakamani na hatima ye kupelekwa gerezani ni ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la polisi sasa linakamilisha sehemu kubwa wa wajibu wake wa kuibaka demokrasia.

Hata hivyo tunalitaka jeshi la polisi na serikali ya CCM wajue kwamba kitendo cha kumpeleka Lema magereza ni ushindi tosha katika harakati za ukombozi wa taifa hili. Maana hakuna silaha yoyote duniani ama jeshi la polisi popote pale duniani ambavyo viliweza kushinda vita dhidi ya ukweli, haki na uwazi.

Ndugu zangu watanzania
Tunawaunga mkono wana Arusha kwa kumpata mbunge ambaye anayatetea maslahi yao kwa mzigo hata pale inapobidi kwenda gerezani kwa ajili ya watu wake na hata ikibidi kifo anaweza kusimamia hilo. Alisema Martin Luther King Jr. 1963 "A man who wont die for something is not fit to live" na akaendelea kusisitiza "Nobody can give you freedom, nobody can give you justice or right or anything. You take it!" (STAND UP; STAND UP 4, UR RIGHT) Hayo yalikuwa maono ya bob marley ambayo aliyaona mwaka wa 1973,baada ya kuwa amekaa katika mto mmoja huko jamaica akaona samaki wanapita katika maji lakini samaki wakubwa wakawa wanawaonea samaki wadogo,hivyo akaona hata hapa duniani hata wa2 walio juu wanawaonea watu wa hali ya chini.

Kwa watu wanaopinga ama kukejeli maamuzi ya Godbless lema kukataa dhamana, Wathubutu kufanya ziara huko Mahospitalini wavae sura za uhasilia wa kibinadamu wakaone watu waliokuwa kama wao jinsi wanavyotaabika kwa kukosa matibabu ile hali ni walipa kodi wa taifa hili. Kwanini Godbless asiende jela wakati anasimamia mambo ya msingi na hayatekelezwi, tukiandamana tunaonekana tunavunja sheria ni afadhali kwenda sehemu wanayodhani tunaogopa kuliko kukaa kimya kumbe hatuogopi. Mungu yupo upande wetu na tunaelekea kushinda unyanyaswaji huu.

Kama ambavyo alivyowahi kusema Martin Luther king jr, ndivyo tunavyo wahakikishia wana wa Arusha, we will work together; we will stand up together, we will go to jail together, until justice runs down like water. maana mateso tunayoyapata ni makubwa kuliko huko jehanam tusipopajua.

Kwa kuonyesha tuko pamoja katika harakati hizi za kudai demokrasia ya kweli tunampogeza Godbless lema mbunge wa Arusha mjini kwa kupeleka ujumbe kwa watawala wanaodhani wanaweza kutumia magereza kama sehemu ya vitisho kurudisha harakati zozote zile nyuma.

Ujumbe huu uwafikie watawala yakuwa jela sisehemu ya kumtishia mtu yeyote Yule mwenye akili timamu, mpenda haki bali ni sehemu ya kawaida ambapo binadamu yeyote Yule anaweza kwenda.

ASANTENI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI WATANZANIA WENZANGU!


Henry J Kilewo
KATIBU (M) Kanda Maalum
01/11/2011




maoni yangu:

Maoni yangu haya matamko siyo ya kupuuzia hata kidongo, lazima tuwaunge mkono hawa makanda.

Makamanda wapo police kushughulikia watu waliyo wekwa ndani jana, anaongoza kilewo
 
Back
Top Bottom