M'kiti wa kijiji Kilolo (CHADEMA) aswekwa lupango kwa kutochangia mwenge

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,166
1,247
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani
Iringa, Gerald Guninita
amemkamata na kumweka chini
ya ulinzi, Mwenyekiti wa Serikali
ya Kijiji cha Udekwa kilichopo
Tarafa ya Mahenge, Obadiah
Lubugo, kwa kutochangia Sh.
70,000 za Mbio za Mwenge.
Lubugo, ambaye ni Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), alionja kadhia hiyo
juzi baada ya kuelekeza fedha
hizo katika manunuzi ya chaki
kwenye Shule ya Msingi Udekwa.
Rekodi ya kijiji hicho inaonyesha
kuwa tangu Tanzania ilipopata
uhuru mwaka 1961, Mwenge
huo haujawahi kupita hapo hadi
hivi sasa, tukio ambalo linatoa
tafsiri tofauti na michango halisia
ya wananchi.
Akilalamikia hatua hiyo mbele ya
mkutano wake na waandishi wa
habari, Lubugo alisema
amehuzunishwa na hatua hiyo
ya Mkuu wa Wilaya kumkamata
na kumlazimisha kulipa fedha
hizo wakati Mwenge huo
ulishapita Juni 22, mwaka huu.
“Amenikamata na kunilazimisha
kulipa huo mchango wakati
shuleni (Udekwa) kulikuwa
hamna hata chaki na tulipeleka
kwa Mkuu wa Shule Sh. 274,000
na akasaini kwa ajili ya manunuzi
ya chaki na mambo mengine.
Lakini cha ajabu alipofika kijijini
kwetu, DC akasema kama sina
fedha hizo nikae Polisi kuanzia
tarehe 29 mwezi Juni hadi Julai
2, mwaka huu ndipo nipelekwe
ofisini kwake," alilalamika.
Lubugo alisema Sh. 274,000
zilizoelekezwa na serikali ya kijiji
kwenda kwenye manunuzi ya
chaki na masuala mengine ya
kitaaluma, zilipitishwa na
wajumbe wa serikali yake
kutokana na shule hiyo kutopata
mgawo wa fedha serikalini kwa
matumizi hayo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa barua
iliyoandikwa na Halmashauri ya
Wilaya hiyo, yenye kumbukumbu
namba KDC/A4/1/30 ya Aprili 12,
mwaka huu, kwenda kwa
maofisa watendaji wa kata,
ikielekeza maandalizi na
michango ya Mbio za Mwenge
wa Uhuru, inaagiza kila kijiji
kuchangia Sh.70,000.
“Sehemu ya barua hiyo inaeleza
hivi: "Mwisho wa kuwasilisha
michango hiyo ni tarehe 10 Mei,
2012 na kila Mtendaji wa Kijiji
anapaswa kupatiwa risiti.
Ningependa mhimize suala la
uchangiaji wa Mbio za Mwenge
kwa vijiji vilivyo kwenye kata
zenu ambapo kila kijiji
kinatakiwa kuchangia
Sh.70,000.”
NIPASHE ilipomtafuta Mkuu wa
Wilaya hiyo kwa njia ya simu ya
mkononi pamoja na kumtumia
ujumbe mfupi wa maandishi
(SMS), kwa ajili ya kumtaka
kuthibitisha au kukanusha madai
hayo, lakini hakujibu.
Afisa Habari wa wilaya hiyo
aliyejulikana kwa jina moja la
Christopher, aliwajibu waandishi
wa habari kwamba hawezi
kupokea simu na ameagiza
afuatwe kijiji cha Lundamatwe.
SOURCE: NIPASHE
 
Lema alisema kuwa angewasilisha hoja binafsi bungeni iyo koroboi izimwe milele. Arusha 2nasubiri akitoka honeymoon kwani alituahidi toka kampeni zake
 
poor governance at all.tutaona vibwanga vingi sana kabla ya 2015.tuzidi kuomba uzima.
 
Wenyeviti wa vijiji igeni mfano huu, kuliko kukimbiza masanamu (Hii koroboi ina nini hasa). Mwenzenu kanunua chaki watoto wanasoma. Huyu anaingia kwenye mashujaa gruop of Tanganyika.
 
Binafsi ata mi mwenge una faida gan had utumie garama zote izo sijui, anaejua anijuze tafadhari
 
Hivi mwenge ni suala la kiserikali? Mimi miaka yote huwa naona wahusika wakuu wa shughuli hiyo ni makada wa CCM na hasa UVCCM which means ni suala la kichama zaidi. Kama ndivyo, ni muhimu sasa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinavyoongoza Halmashauri, kata, au vijiji mbali mbali kuwaandikia wenyeviti husika kutowachangisha wananchi wa maeneo yao kwa ajili ya mwenge.

Tungependa pia kuona CHADEMA wakitoa msimamo wao hadharani na matangazo kwenye vyombo vya habari juu ya msimamo wao rasmi juu ya suala hili na hatua zipi zichukuliwe kwa watendaji wa serikali watakao wanyanyasa wananchi kuhusiana na hili kama alivyofanya huyu Mkuu wa Wilaya.

Hii nchi ni huru na kila mtu ana haki ya kufuata itikadi au kuabudu chochote anachoona kinafaa. Wanaotaka kuabudu/kukimbiza mioto waachwe wafanye hivyo kwa utashi na gharama zao wenyewe na sio kulamizisha wananchi.
 
asante sana mwenyekiti chadema kwa kuwanyima hela hao kunguni wanyonya damu. Fedha za elimu za wilaya wale wao pasipo kuleta hata kiduchu kijijiji na michango nayo wapelekewe ili wakale kwenye mwenge wapi na wapi?
 
Manunuzi ya chaki ni jambo jema kuliko hilo analolishikilia DC ambalo halina tija kwa taifa,watoto wasisome mwengeupte?
 
Huyu mwenyekiti awe mfano kwa wenyeviti wote wa chadema wanaaongoza vijiji.

Mkuu, huyu mkuu wa wilaya ametutengenezea penati mhimu kupitia mwenyekiti wetu, hivyo CHADEMA wilaya watume timu kuifuta ccm katika kijiji hicho bila kusahau kupeleka msaada katika shule ya kijiji watoto waelimike. Badala ya kuchangia mwenge uliowapelekea ukimwi.
 
DC elimu yake kama ya luc na prof Maji,anajsikia wivu kuona watoto wadogo wanaelekea kumzidi elimu
 
Tumshali kwa false imprisonment plz. Wasiliana nami privately nikusaidie
 
Back
Top Bottom