M'kiti wa kijiji amtandika fimbo mwalimu mkuu

Lakini katika tukio la mkoani Mara, mwenyekiti huyo wa kijiji alichukua hatua hiyo baada ya kupata habari kuwa mkuu huyo msaidizi wa shule alikuwa akikata miti kwenye shamba la shule kwa ajili ya kutengenezea mlango wa choo.

Huyu mwenyekiti hana ethics na wanaomtetea pia. Yeye ni mahakama hadi afikie hatua ya kutoa adhabu? Hawa ndiyo wale miungu watu wanaonyanyasa wanavijiji?

Nikiangalia hiki kipande najiuliza demarcation ya uongozi wa shule na kijiji iko wapi? Shule ikiwa ndani ya kijiji inamaana mwenyekiti wa kijiji ni administrator wa shule na mali zake? Tunaweza kumuuliza Mwenyekiti wa kijiji alikuwa wapi hadi mlango wa choo whether cha mwalimu mkuu, walimu au wanafunzi unaharibika atatujibu?

Nashauri apewe adhabu kali liwe fundisho kwa wote wanaohodhi madaraka

 
Swala lisiwe waalimu tu, Tuhakikishe tunapin down vitendo vya wananchi kuchukuliana sheria mkonini wao kwa wao. Hapa tutatatua na Madaktari kuja kupigwa Ngumi pale jamaa anapofariki, Civil engr. kupigwa Risasi na mwenye nyumba pale nyumba inapoweka ufa wiki moja baada ya ujenzi!

Tunahitaji utawala wa sheria udhihirishwe na viongozi na wananchi wauzingatie!!!. Kinachoendelea ni wananchi kusombwa na mmomonyoko wa utawala wa sheria, na kila mtu kuamua na kuhukumu yeye mwenyewe, kwa utashi wake mwenyewe!!.

Tatizo liangaliwe kwa upana!! Kwa sababu huyu bwana hakumtandika huyu mwalimu kwa sababu yeye ni mwalimu, La! bali kwa sababu amekata miti miwili ya shule! Ina maana hata kama ungekuwa ni wewe ukepata bakora kutoka kwa mkuu huyu, ila kama ulipitia judo kidogo hapo mabo yangekuwa magumu kidogo, na kama mke(mume) wako yupo jirani na watoto kidogo wangekusaidia kupigana!!. Hali ingekuwa mbaya pale Mke wa muheshimiwa na mpwae wangewakuta mnampiga huyu bwana in revenge!, nao wangeingilia kati, tena kwa mapanga,bita ni bita bwana!!. tayari machafuko!!.

So lets advocate the rule of law, with our leaders being role models!!
Naendelea kusisitiza utawala wa sheria uzingatiwe!!
 
Back
Top Bottom