Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

KWANZA lazima ujue kwanini anakataa, ukishajua sasa utapambana na hiyosababu yake ya kukataa. PILI elewa kuwa wanaume wengi hatutaki kuelekezwa elekezwa na akina mama, wazo litoke kwangu sio kwako,sijui ndo mnaita mfumo dume sijui. TATU wanaume wengi issue sio kupima tatizo ni kupokea matokeo, wakati huo unaambiwa kaa hapa majibu yako haya. we? he? Nikikuta positive sijui nilie? kweli nilie mbele ya mke wangu?.
Hizo ni baadhi ya sababu.
Cha kufanya;
1. Kupima isiwe issue kwenu kila mkikaa kapime kapime kapime kutwa nzima, mtafute rafiki yake wa karibu anaempenda na kumsikiliza ndie amweleze
2. Anaweza akakataa kwa vile anahisi ameathirika, changudoa wake Mwajuma kafa kwa ukimwi mwaka jana na walikuwa wanacheza pekupeku.
kwenda kupima kwake ni kama kwenda nyumba ya kuhifadhi maiti na kuuliza wahudumu nimemletea mgonjwa wangu chai.Hataenda. Hapa anapaswa kuelezwa tena na rafiki yake kuwa unajua kufa kwa mwajuma si lazima uwe na ukimwi, watu wana ukimwi na wanazaa watoto wasio na ukimwi ,hapo ataenda
aaaaah mbona mbinu nyigi tu, ningekueleza zote tatizo time, muda.Pamoja na hayoo yoteee wanaume wenzangu TUKAPIMENI.
 
on top of that, kuishi na nyoka ndani bila kujua kuwa yuko ndani, ni bpora mara elfu kuliko kujua kuwa yuko ndani lakini ukashindwa kumfukuza/kumuua, nadhani hata kusinzia huwezi. now you know why we don like hayo mambo ya angaza.

Mkuu AK hakuna kitu kibaya duniani kama kujua, we ni bora uendelee kuto jua maana ukijua tu hapo hapo inakuongezea mastress n.k mfano wewe ukijua mpenzi wako ana UKIMWI na umewahi mega mara kadhaa sijui kama utakuwa katika hali nzuri mm naona bora kwendelea kutojua na sipendi nijue afya yangu wkt mm mwenyewe najiona nipo fit.
 
unahitaji counselling y a nguvu tu..... utaenda mwenyewe bila hata kulazimishwa.

Hahahaha nani aende watu tunamisimamo kama jiwe haendi n'tu kupima watu wanaenda wanakula kona kuchukua majibu wanamwachia Dr. na mshauri nasaha shaaaaaaa. Mimi nipime ili iweje? Zaidi zaidi mtanisababishie niwe namega ovyo ovyo.
 
KWANZA lazima ujue kwanini anakataa, ukishajua sasa utapambana na hiyosababu yake ya kukataa. PILI elewa kuwa wanaume wengi hatutaki kuelekezwa elekezwa na akina mama, wazo litoke kwangu sio kwako,sijui ndo mnaita mfumo dume sijui. TATU wanaume wengi issue sio kupima tatizo ni kupokea matokeo, wakati huo unaambiwa kaa hapa majibu yako haya. we? he? Nikikuta positive sijui nilie? kweli nilie mbele ya mke wangu?.
Hizo ni baadhi ya sababu.
Cha kufanya;
1. Kupima isiwe issue kwenu kila mkikaa kapime kapime kapime kutwa nzima, mtafute rafiki yake wa karibu anaempenda na kumsikiliza ndie amweleze
2. Anaweza akakataa kwa vile anahisi ameathirika, changudoa wake Mwajuma kafa kwa ukimwi mwaka jana na walikuwa wanacheza pekupeku.
kwenda kupima kwake ni kama kwenda nyumba ya kuhifadhi maiti na kuuliza wahudumu nimemletea mgonjwa wangu chai.Hataenda. Hapa anapaswa kuelezwa tena na rafiki yake kuwa unajua kufa kwa mwajuma si lazima uwe na ukimwi, watu wana ukimwi na wanazaa watoto wasio na ukimwi ,hapo ataenda
aaaaah mbona mbinu nyigi tu, ningekueleza zote tatizo time, muda.Pamoja na hayoo yoteee wanaume wenzangu TUKAPIMENI.

Tall,
Asante sana... umetoa points nzito mno..nashukuru sana.
Jamani... wale wanaoshughulika na mambo ya VCT nadhani mnachota maarifa na mbinu humu.
Tuendelee kupeana mawazo jamani....
 
mfano wewe ukijua mpenzi wako ana UKIMWI na umewahi mega mara kadhaa sijui kama utakuwa katika hali nzuri mm naona bora kwendelea kutojua na sipendi nijue afya yangu wkt mm mwenyewe najiona nipo fit.

kaka signature yako inasema UKIUZA UTUMBO USIOGOPE...........
nadhani ni bora pia ukimegamega usiogope kucheki afya yako
hahahahahahahah lol
 
Chris..leo ni mimi na wewe tu hadi kieleweke!
Bado narudi tena palepale - imagine kuna vyombo viwili vyenye maji... kimoja maji yake yametiwa sumu ukinywa utakuja kufa baada ya muda mfupi na cha pili maji yake ni salama unaweza kunywa. Unachotakiwa ni wewe kuomba tu wayapime ujue yapi ni salama.

Je, ukiambiwa hivyo utasema ngoja nibahatishe ninywe nione kama nitakufa, au utaomba yapimwe ujue yapi ni salama uyanywe?

Si unaona hapo sasa WOS? Kitakachopimwa hapo ni MAJI siyo? Siyo mimi!
With serious note:
Ni bora kupima kama kuna uhakika wa kupata solution ya tatizo. Hivi hujiulizi kwanini hatuogopi kupima malaria, typhoid etc etc? Ni kwa sababu tiba zipo. Sasa hili la kupima halafu ukiukwaa unaambiwa uishi kwa matumaini ndio tatizo kubwa. Mi tiba ya UKIMWI ikipatikana ntakuwa wa kwanza kubisha hodi ANGAZA!

Kwa sasa naishi kwa matumaini kabla sijapima. Na assume nimeshakanyaga miwaya, so naishi kwa matumaini. Refer mfano wa akili kichwani. Ni heri ulale nyoka akiwa chumbani bila wewe kujua kuliko ujue yupo lakini kumuua huwezi! Utaikimbia nyumba yako bila kutaka!
 
kaka signature yako inasema UKIUZA UTUMBO USIOGOPE...........
nadhani ni bora pia ukimegamega usiogope kucheki afya yako
hahahahahahahah lol

Yeah mm namega siogopi ukimwi naendelea kumega na kumega.
Lakini naogopa kujua kilichopo ndani kama nimeoza wacha niendelee kuoza lakini nisijijue kuwa nimeoza.
 
Hahahaha nani aende watu tunamisimamo kama jiwe haendi n'tu kupima watu wanaenda wanakula kona kuchukua majibu wanamwachia Dr. na mshauri nasaha shaaaaaaa. Mimi nipime ili iweje? Zaidi zaidi mtanisababishie niwe namega ovyo ovyo.
Fidel.... taratibu... HIV and AIDS ( Prevention and Control) Act ya 2008 ushaisikia weye? utafungwa!
 
Si unaona hapo sasa WOS? Kitakachopimwa hapo ni MAJI siyo? Siyo mimi!
With serious note:
Ni bora kupima kama kuna uhakika wa kupata solution ya tatizo. Hivi hujiulizi kwanini hatuogopi kupima malaria, typhoid etc etc? Ni kwa sababu tiba zipo. Sasa hili la kupima halafu ukiukwaa unaambiwa uishi kwa matumaini ndio tatizo kubwa. Mi tiba ya UKIMWI ikipatikana ntakuwa wa kwanza kubisha hodi ANGAZA!

Kwa sasa naishi kwa matumaini kabla sijapima. Na assume nimeshakanyaga miwaya, so naishi kwa matumaini. Refer mfano wa akili kichwani. Ni heri ulale nyoka akiwa chumbani bila wewe kujua kuliko ujue yupo lakini kumuua huwezi! Utaikimbia nyumba yako bila kutaka!
Nakuelewa na woga uliopo kwenye suala zima la kupima.... bahati mbaya sana hapa itakuwa vigumu kuweka kila kitu bayana na kukufanya woga wa kupima ukutoke... but the bottomline is its better to know ur status mapema kuliko kukaa hujui..... mfano - ukijua una virusi utajitahidi kuzuia maambukizi mapya - ukiwa hujui unaendelea kukuna huku na kule na kuendelea kuongeza virusi kwa idadi na aina.Hii itakufanya uugue mapema na kupoteza maisha baada ya mateso makali.
 
Fidel.... taratibu... HIV and AIDS ( Prevention and Control) Act ya 2008 ushaisikia weye? utafungwa!

Ndo maana nasema nimeshuhudia wengi walio pima wakawa wanao wakaendeleza ufataki wa kuusambaza na wale walio pima na kujikuta safi nao wameendeleza libeneke kama kawa wanaamini njia waliyo kuwa wanatumia ilikuwa sahihi makamuzi yanaendelea. Kwangu mm sitaki nijue kama ninao au sina itaniletea matatizo aidha ndo mtanipoteza kabisa au nikajipotezea kiaina aikwambia n'tu yataka moyo sio rahisi kama mnavyo fikiria.
 
Kupima siyo ishu Fidel.... mbona ni kama unavyofanya medical exam nyingine tu...mwanzo kweli utaogopa lakini kama unakawaida basi haikupi shida.Kikubwa ni kupata uhamasishaji na uwe na information za kutosha ili ujue faida na hasara za kupima na kutokupima.Hii itakuwezesha kujua kipi bora na uamuzi gani ufanye.Pia kama una mienendo hatarishi mara nyingi unakuwa na hofu.Pima kisha punguza risky behaviours!
 
1. Kwanini wanaume wengi hawataki kupima na kujua afya zao ( majority wanajua kabisa kuwa wanaishi maisha hatarishi ( risky life styles)

Huo analogy ya nyoka ndani ya nyumba (aliyoitoa AK) inaelezea vizuri issues around reluctance ya wanaume kupima HIV.

Nadhani ni suala la kukosa elimu sahihi kuhusu ukimwi. Unyanyapaa pia bado ni tatizo kubwa sana.

Tulio wengi, kama hujui HIV status ya mtu, mara nyingi tunaishi (kucheza, kula, tunashare vitu nk) nao vizuri tu, lakini the moment akisema ni HIV+, kila mtu anaanza kumtizama na kujihusisha nae kwa tahadhari (hata akikupa mkono kukusalimu mwili unasisimka!).

Kama nchi bado hatujawa wataalamu na washauri nasaha wa kutosha kuweza kukabili hili janga hivyo waathirika wengi wanakosa huduma sahihi mara baada ya kupima.

2.Mbinu gani zitumike kuwashawishi wanaume wasiotaka kujua afya zao kupima kwa hiari?

Hakuna solution inayoweza kufanya kazi overnight. Inahitaji muda, ili watu wabadilike kifikra. Kubwa kabisa ni kujaribu kama jamii kujijengea utamaduni wa kucheck afya zetu mara kwa mara. Wengi wanakufa kwa magonjwa ambayo kama wangekuwa wanacheck afya zao mara kwa mara yangeweza kutibika au angalau kupunguza makali yake. Kampeni kama zile za MEWATA (kansa) zingeweza kuwa nyingi zaidi na pia kupanua wigo wake na kuangalia afya kwa ujumla.
 
Kupima siyo ishu Fidel.... mbona ni kama unavyofanya medical exam nyingine tu...!

Heee kupima sio ishu?
Ok kwa hiyo kuchukua majibu ndo ishu sasa watu wanakimbia majibu yao.
Mimi vipimo vikubwa sipimi kabisaa. Hapimi mtu .
 
Heee kupima sio ishu?
Ok kwa hiyo kuchukua majibu ndo ishu sasa watu wanakimbia majibu yao.
Mimi vipimo vikubwa sipimi kabisaa. Hapimi mtu .
Hii ishu wa wanaume kuruka kimanga.inanikumbusha wakati fulani wataalamu walikuja kanisani kwetu wakahamasisha watu wakapime.Watu walikuja kanisani na familia zao - baba, mama na watoto. Baada ya uhamasishaji kilichotokea ni wakina mama na watoto ndio walioongoza kwenda kupima.Wakina baba wakaelekea kwenye magari yao wakaenda kuwasubiri wamama na watoto wapime! Ilikuwa aibu maana maswali yaliyojitokeza dhahiri ni kuwa wakina baba hawakwenda kupima kwanini???
ingekuwa ni wewe wanao na mke wameenda kupima wewe ukasubiri kwenye gari - ungewaangaliaje wanao mkiwa mezani? wakianza kukuuliza baba kwanini hukuja kupima ungejibu nini?
.
 
Hii ishu wa wanaume kuruka kimanga..

Navyo jua mm swala la kupima ni la hiari si la kulazimisha mtu anahiari mwenyewe apime na sio lazima kama baba ameona hakuna umuhimu wa kupima mwache usimrubuni apime wkt yeye anajiona hana haja ya kujua afya yake.
 
1. Kwanini wanaume wengi hawataki kupima na kujua afya zao ( majority wanajua kabisa kuwa wanaishi maisha hatarishi ( risky life styles)
Una uhakika na hilo?
 
Back
Top Bottom