BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Kuna kitu ninakiona na sikielewi kabisa.Mwanaume akifungwa jela, mke anapaswa naye kuwa kifungoni angalau cha nje.Jamii inamtegemea amsubiri mumewe arudi nyumbani hata kama anatumikia kifungo cha miaka 50! Sheria hata hivyo inamruhusu mke kudai talaka kama mume atafungwa kifungo cha muda mrefu.
Lakini mke akiwa na kesi tu..(hapo hajafungwa)...mume ataanza kujitafutia liwazo kwa kisingizio ati mke hayupo nyumbani anahangaika na kesi.Akifungwa ndiyo kabisaaa asahau kumkuta mumewe akimsubiri.
1.Hivi ni kwanini jamani?
2.Kwa wanaume tu...mkeo akifungwa utamsubiri amalize kifungo?
WoS, watu wanavinjari hata wake zao au waume zao hawajafungwa na wanaishi nyumba moja! Sasa kwa wanaume mke akifungwa kwa miaka 10 au zaidi si atakuta jamaa kishajichukulia kimwana kingine jumla jumla? Kwa wanawake anaweza asihamishie mtu ndani ya nyumba lakini akawa na nyumba ndogo yake ya kwenda 'kujiliwaza' kila anapojisikia kufanya hivyo.