Mkenya: Oa mwanamke wa kitanzania upate ardhi Tanzania

steering

Member
Nov 28, 2011
71
12
Baada ya kuona post ya jana juu ya kuoana kwa Watanzania na Wakenya, imenikumbusha mkenya mmoja niliyekuwa naye mjini Iringa ambaye alisema Tanzania inabana ardhi yake sana kiasi cha kuwawia vigumu wao, wakenya, kupata ardhi hasa ikizingatiwa, uhuru kenyata ana ekari zaidi ya 500,000 achilia mbali ma-settler wengine.

hivyo, njia mbadala ya kuipata ardhi baada ya sera ya Tanzania kuwa ngumu ni kumwoa mwanamke wa Kitanzania na kulowea Tanzania kwa kumshawishi amiliki ardhi kupitia fedha za Mkenya....kwa mujibu wao, hiyo ndiyo technic iliyobakia, je, itawezekana?
 
Mkuu hiyo mbona inawezekana tena sana tu.Na siyo wakenya tu hata mataifa mengine wamefanya hivyo.Kuna jamaa mmoja ni Mzambia,ameoa Mtz na ana nyumba na viwanja tanzania kupitia dada yetu wa kitanzania.
 
Ndivyo ilivyo. katika moja ya safari zangu niliwahi kukutana na dada wa kikenya, akawa anasema sisi watanzania ni mambumbumbu mno, wakenya watatumia gia ya kuoa na kuolewa kama njia mojawapo ya kujipatia ardhi. watu wengi sana hawajashtukia hilo.
 
Point of correction, ardhi ya Tanzania mtu amilikishwi, anaazimwa tu kwa muda. At any time ikitakiwa, inachukuliwa kwa wewe kupewa fidia tu, ni tofauti na Kenya.

I stand to be corrected.
 
Ndivyo ilivyo. katika moja ya safari zangu niliwahi kukutana na dada wa kikenya, akawa anasema sisi watanzania ni mambumbumbu mno, wakenya watatumia gia ya kuoa na kuolewa kama njia mojawapo ya kujipatia ardhi. watu wengi sana hawajashtukia hilo.

So na wewe ukakubali kuitwa ivyo na ukachekelea siyo! acheni kujidhalilisha, mi sioni cha ziada walichonacho zaidi ya TZ. Ukiamini basi hiyo ni wewe si waTZ.

Mambo hayo mbona hata wa-Africa wengi tu wameoa wazungu ili wawe raia wa nchi hizo. Huwezi sema wa-zungu ni mbumbumbu hizo ni haki za kisheria sioni umbumbumbu hapo.
 
Cha msingi ata ukioa sister uraia bado wa Kenya ukivuta kwenuuuuuuuuu sisi twabaki na Ardhi.
Nimeona iyo ni common practise kwa sasa naona kuna haja ya kuifanyia kazi
 
waTZ tuamke maana wengi wetu hawajui umuhimu wa rasilimali tulizonalo, hao wakenya wanajua umuhimu ndo maana wanatumia gia hiyo na pia kwao ardhi ni ishu kubwa sana.
[penye miti hakuna wajenzi]
 
Sasa hizo ndoa kuna kuwa na mapenzi ya dhati kweli?Wakenya kwao ardhi inamilikiwa na mtu binafsi lakini Tanzania ardhi ni mali ya serikali,sisi tunakodishwa tu ndiyo maana kisheria kila mwaka tunatakiwa kulipia kodi!!
 
Baada ya kuona post ya jana juu ya kuoana kwa Watanzania na Wakenya, imenikumbusha mkenya mmoja niliyekuwa naye mjini Iringa ambaye alisema Tanzania inabana ardhi yake sana kiasi cha kuwawia vigumu wao, wakenya, kupata ardhi hasa ikizingatiwa, uhuru kenyata ana ekari zaidi ya 500,000 achilia mbali ma-settler wengine.

hivyo, njia mbadala ya kuipata ardhi baada ya sera ya Tanzania kuwa ngumu ni kumwoa mwanamke wa Kitanzania na kulowea Tanzania kwa kumshawishi amiliki ardhi kupitia fedha za Mkenya....kwa mujibu wao, hiyo ndiyo technic iliyobakia, je, itawezekana?

washtuka leo wakati Mungiki washazaliana na wabongo..? hiyo ni kwa wote..hata wanawake wa kenya wanaolewa/wanazaa kwa fujo na watanganyika waboreshe fursa zao kupata ardhi tz.. binafsi nawafahama kama wadad 2 wa kenya walfanya hii makitu
 
Mbona poa ardhi mmeikuta nyie hakuna tatizo as long as wanaitumia kuzalisha siyo ku-own tu mapori kama kule kwao..
 
Sio wakenya tu,hata wazungu wanaoa watanzania kwa sababu za kiuchumi,BTW kila mtz ana haki ya kuoa au kuolewa na mtu wa taifa lolote
 
So na wewe ukakubali kuitwa ivyo na ukachekelea siyo! acheni kujidhalilisha, mi sioni cha ziada walichonacho zaidi ya TZ. Ukiamini basi hiyo ni wewe si waTZ.

Mambo hayo mbona hata wa-Africa wengi tu wameoa wazungu ili wawe raia wa nchi hizo. Huwezi sema wa-zungu ni mbumbumbu hizo ni haki za kisheria sioni umbumbumbu hapo.

upo sahihi kabisa sema kuna wengine wanakurupuka kuchangia bila kufikiria vizuri
 
Back
Top Bottom