Mkenya auawa katika maandamano ya CHADEMA Arusha

Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
79
Polisi imeua raia mmoja wa Kenya Ndugu Paul Njuguna Kaiyehe (Polisi walitumia jina la uongo kuficha uraia wake - George Mwita Waitara).

Huyu ndugu ni raia wa Kenya kwa uthibitisho wa balozi mdogo wa Kenya anayehudumu jijini Arusha Ndugu Mathenge raia huyo wa Kenya aliyeuawa ni Mwanaume umri wa miaka 26 na alipigwa risasi ya moto tumboni na hii imedhibitishwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha.

Vilevile kuna taarifa za kuaminika kutoka kwa wahanga wa machafuko ya juzi kuwa polisi iliwaua raia wengi takribani zaidi ishirini na saba na maiti zao zimesambazwa katika mochuari za mikoa ya manyara, Arusha na Kilimanjaro uthibitisho halisi ni hospitali ya KCMC maiti mbili za wanaume zimepelekwa na polisi siku ya tarehe 6 januari 2011 zina majeraha ya risasi rekodi inaonyesha "unknown".

Mgonjwa mmoja amelazwa KCMC wodi surgical one alipigwa risasi na polisi maeneo ya Meru primary jijini Arusha akiwa katika shuguli zake alizirai na kujikuta yupo KCMC ana maumivu makali kifuani na amepigwa risasi ya moto mguuni!
 
du, hii mpya tena...mi nimeanusanusa na kutonywa kuwa waliokufa ni 8, kati yao polisi wa3, raia wa5...lkn hiyo inayojiita intelijensia imeamua kuficha hbr hiyo ili kudanganya jamii ya kimataifa kuwa haikufanya uharibifu mkubwa.

Hiyo ndiyo intelijensia yetu wabongo bana.
 
Duhh! Fanya utafiti utupe taarifa kamili. Maiti ngapi ziko Manyara hospital, ngapi ziko Moshi na ngapi ziko Arusha? Je, kuna ndugu wanaotafuta watu waliowakosa huko Arusha. Idadi ya wanaotafutwa ni wangapi?

Infact, haiingii kwenye akili kuwa waliuawa watu wawili tu wakati risasi zilifyatuliwa kama mvua na zililenga makusanyiko ya watu.
 
Ni kweli Polisi waliua watu wengi sana. Marafiki zangu wanaofanyakazi katika Manispaa ya Arusha wameniambia hayo.

Inabidi kituo cha haki za Binadamu kufanya utafiti wa haraka katika mikoa ya manyara,Kilimanjaro na Arusha ili kuujua na kuanika ukweli.

Baada ya hapa IGP, Nahodha wajiuzulu na wapelekwe kwa OCAMPO
 
Polisi walitumia nguvu kubwa pasipostahili.
Wameua watu halafu wanatutumia vibaraka wakisema kwamba haya ni matukio ya kisiasa tuyatatue kisiasa...

Madhara ya kuiba kura ndo haya.... (wanaogopa mpaka raia wasio na silaha)
 
Polisi wanajifanyaga wananjanja sana kwa kuficha mambo.

Nina ndugu zangu 2 ambao ni polisi wa kituo cha central-nimewauliza wanipe idadi kamili nao wamenipa data kama zilizotangazwa, nikaona kwasababu nimewapigia simu kuwauliza watakuwa na woga wa kuanza kunipa data; nitawafuata kesho physically nijue habari nzima inasemaje kuliko kupata hiz secondary data
 
Halafu Nahodha anasema wataanzisha mazungumzo baada ya kuua raia wasio na hatia wengi hivyo? Mwema, Nahodha na Kikwete wajiuzulu kwanza ndio mazungumzo yaanze!
 
Duhh! Fanya utafiti utupe taarifa kamili. Maiti ngapi ziko Manyara hospital, ngapi ziko Moshi na ngapi ziko Arusha? Je, kuna ndugu wanaotafuta watu waliowakosa huko Arusha. Idadi ya wanaotafutwa ni wangapi?

Infact, haiingii kwenye akili kuwa waliuawa watu wawili tu wakati risasi zilifyatuliwa kama mvua na zililenga makusanyiko ya watu.

Kiongozi nafikiri twapaswa wote kushirikiana katika hili na tambua sisi tulioko jikoni tafiti twazifanya kwa uangalifu wa hali ya juu kwani ikumbukwe kuna hata ndugu wananyimwa kuwaona ndugu zao ambao ni majeruhi kwa maagizo kutoka juu.

Kuna waandishi wa habari waliokuwa wanafanya coverage ya matukio ya jana wametishiwa usalama wa maisha yao na kuamriwa kuharibu film zilizokuwa na coverage ya matukio ya polisi kuwapiga risasi raia na hata wale waliofanikiwa kuwa na film zenye matukio yale ya unyanyasaji wa polisi kwa raia vyombo vya habari wanavyofanyia kazi havikuonyesha udhalimu huo wa serikali kwa kutumia askari wanafunzi wa chuo cha polisi Moshi na wengineo kutoka mikoa ya Manyara na Field Force Unit toka kule Ukonga Dar es Salaam.

Na kwa habari ya uhakika kuhusu mauaji kuwa mengi kuna maiti kumi zilifikishwa kituo cha polisi tarehe 5 Januari siku ya tafrani na hizi ni kutoka kwa polisi ambae ni mhanga wa tukio hilo aliyempoteza ndugu katika tafrani hizo na hajafanikiwa kumuona nduguye akiwa maiti au majeruhi!

Polisi acheni ubabaishaji balozi Mathenge ameanza kuwaumbua jitokezeni au subirini hasira za ndugu waliofiwa kuja kuwaumbua zaidi ya Mathenge; be smart Mwema and Andengenye!
 
Poleni watu wa Arusha kwa Dhahama hii. Cha msingi ni kutafuta ukweli na kuuanika hadharani ili watu wafahamu unyama uliotendwa na Polisi wa JK ili kumlinda na ccm yake.
 
muda utaongea, na hiyo intelijensia itafeli somewhere, ndipo aibu itakapozaliwa.. wito kwa waliopoteza ndg zao wajitokeze kwny vyombo vya hbr kuripoti, mwisho tutajua nani ni mpumbavu. Na hii itarahisisha kazi ya Ocampo, maana atakuwa amepata shitaka jipya la kuudanganya umma na jumuia ya kimataifa juu ya idadi ya vifo. Maiti ya binadamu haipotei kwa kufichwa bana.
 
If we can get the name and number of people who died, and how they died ingemaliza huu utata wote. Naimani watu wa Arusha wanajua ndugu zao walioshiriki maandamano au mkutano na mpaka leo hawajapatikana then tunaweza kuanzia hapo kutafuta namba kamili ya majeruhi na waliokufa. Hii yakusema wawili wamekufa it is hard to believe lets wait for the facts to come out.:disapointed:
 
Imekuaje mkenya ashiriki maandamano ya kupinga uchaguzi wa meya wa Arusha? na mkenya huyo ni miongoni mwa marehemu waliouliwa ktk maandamano ya Arusha! Jee, inawezekana wa Kenya wengi walishiriki maandamano hayo? nani aliwaalika? na nani alilipia gharama zao za kuja Arusha kushiriki maandamano hayo? tunasubiri INTELEGINSIA ITUPASHE?

SOURCE: CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM

Makamba anahusika na Wakenya!
 
Fanya uchunguzi usiropoke tu, ni aibu kwa mwana jamiii kuwa hivyo "think before" kwani risasi zilikuwa na senser ya kuwatambua waandamanaji tu?
 
Fanya uchunguzi usiropoke tu, ni aibu kwa mwana jamiii kuwa hivyo "think before" kwani risasi zilikuwa na senser ya kuwatambua waandamanaji tu?

nashukuru kwa kumjibu na la kumuongezea na wale wagonjwa wa Kaloleni hospital baada ya kuumia kwani nawo waliandamana!
 
polisi waliwapiga risasi raia yoyote aliyekua barabarani!sijui watu wangehudhuriaje mkutano bila kutembea?
 
Imekuaje mkenya ashiriki maandamano ya kupinga uchaguzi wa meya wa Arusha? na mkenya huyo ni miongoni mwa marehemu waliouliwa ktk maandamano ya Arusha! Jee, inawezekana wa Kenya wengi walishiriki maandamano hayo? nani aliwaalika? na nani alilipia gharama zao za kuja Arusha kushiriki maandamano hayo? tunasubiri INTELEGINSIA ITUPASHE?

SOURCE:1) CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM
SOURCE:2) HabariLeo | Marehemu maandamano ya Chadema Mkenya

Hao ndio chadema, wako tayari kuleta mamluki ili wahahakishe kuwa fujo zinafanyika.
 
Imekuaje mkenya ashiriki maandamano ya kupinga uchaguzi wa meya wa Arusha? na mkenya huyo ni miongoni mwa marehemu waliouliwa ktk maandamano ya Arusha! Jee, inawezekana wa Kenya wengi walishiriki maandamano hayo? nani aliwaalika? na nani alilipia gharama zao za kuja Arusha kushiriki maandamano hayo? tunasubiri INTELEGINSIA ITUPASHE?

SOURCE:1) CHADEMA yagomea mazungumzo na CCM
SOURCE:2) HabariLeo | Marehemu maandamano ya Chadema Mkenya

Nani kasema risasi na mabomu yaliwadhuru waandamanaji tu?

Je unataka tuamini maandamano yalifanywa na wakenya?

Hivi hujui kuwa kuwa risasi na mabomu huwa havichagui kama wewe ulikuwa muandamanaji au ni bahati mbaya waandanaji walikuwa wanapita pale ulipokuwa muda huo!

TAFAKARI!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom