Mkemia Mkuu, Ernest Mashimba is NO MORE

Ohhh,

Dr. Mashimba, a funny guy in his own way, nakumbuka alisurvive ajali mbaya sana a few year ago na akarejea kazini vizuri tu, nasikitika sana kusikia habari hizi... alikua pia mtu wetu kwa kujali vijana wenye kupenda kujiendeleza
 
Mkemia Mkuu wa Serikalki Ernest Mashimba afariki dunia hguko Tanga. Source Channel 10 bulletin at 7pm.

RIP
 
Mashimba anafahamika kwa kuwa na msimamo maana alianzia kazi Zanzibar wakati wa Dk Salmin Amour alikotofautana na serikali ya huko kabla ya kuwa Mkemia Mkuu Tanzania. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi ameen.
 
Ndo manake. Tunaambiwa huu uhai si wetu tumeushikilia kama mali ya mtu. mwenyewe akitaka anauchukua. Tujiweke tayari muda wote maana hatujui siku wala saa.

May his soul rest in peace Amen!
icon9.png
icon9.png
icon9.png
 
Poleni sana Familia ya Dr. Mashimba. Imeniuma sana hii, Dr. alikua ni muadilifu na mchapakazi wa kweli. RIP
 
Ivyo vifo vya ghafla ninawasiwasi navyo.
Kama ni mapenzi ya mungu may his soul rest in peace.Amen
R.IP Dr. Mashimba.

Unaposema "kama ni mapenzi ya mungu may his soul rest in peace.." Maana yake kuna kifo kinaweza kutokea bila mungu kupenda? Na kama si mapenzi ya mungu asipumzike katika amani ?
 
Dr Mashimba alisoma Zanzibar na alifundisha Pemba shule ya Fidel Castro katika miaka ya mwanzo wa themanini. Aliwahi pia kuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kabla ya kwenda kwa masomo ya juu (Masters na PhD) huko Australia.

Alikaa huko kwa miaka mingi kidogo baadae alirudi Zanzibar na kuwa Chief Chemist wa Zanzibar na ndio akahamia Bara baada ya kupata ile nafasi.

Mungu ailaze roho yake pahala pastahiki.
 
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hoteli ya Lushoto Executive Lodge aliyokuwa amefikia mkoani Tanga.

Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Liberatus Sababs alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema marehemu alifariki jana akiwa usingizini.
Alisema wahudumu wa hotel hiyo, waligundua kutokea kwa kifo hicho majira ya saa 4 jana, wakati wakitaka kufanya usafi wa vyumba baada ya

kugonga muda bila majibu kujibiwa, hali iliyosababisha watoe taarifa kwa uongozi wa juu wa hoteli hiyo ambao uliamua kuchukua funguo za akiba na kwenda kufungua mlango.

Kamanda Sabas alisema uchunguzi zaidi kuhusu kifo hicho unaendelea na taarifa rasmi itatolewa leo.

Habari za kuaminika zinasema, Dk. Mashimba alikuwepo Lushoto kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za binti yake anayesoma Shule ya Sekondari ya Wasichana Kifungilo, ambapo alialikwa kama mzazi rasmi, aliyewakilisha wazazi wa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu.
Katika hutuba yake, aliyoisoma kwa niaba ya wazazi, Dk Mashimba alisisizita watoto wa kike kupewa kipaumbele katika elimu, kwani ikiwa wataelimishwa wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko.

Alitoa mifano, mbalimbali ya baadhi ya wanawake walofanya vizuri katika uongozi baada ya kushika nafasi za juu akitoa mfano wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro.
Katika hafla hiyo, marehemu aliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya intaneti shuleni hapo.
Pia katika sherehe hizo, Dk. Mashimba alinunua gazeti lililoandikwa na wanafunzi kwa sh 100,000 huku akitoa sh 50,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu wa shule hiyo.


Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima.
 
Raha ya milele umpe ee Bwana;
Na mwanga wa milele umwangazie;
Astarehe kwa amani.
Amen
 
Back
Top Bottom