Mke wangu unichukulie, mumewe unanivunja mkono!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Mkuu wa kituo cha Polisi Kiteto, amempatia kipigo mwanaume hadi kumvunja mkono mwanaume huyo. Kituoko hicho kilitokea wakati mke alipoenda kumuona mkuu wa kituo, eti kushtaki mumewe hataki kumpa talaka.

Kwa bahati mbaya, wakati mke akiwa anatoa mashataka kituoni, mume wa huyo mke alikuwa akijipitia bila hata kujua kuwa mkewe yuko polisi. Alipomuona huyo mume akijipitia kwa mbali ktk mihanjo yake, ndipo Mkuu wa Kituo alipomuuliza mwanamke kama huyo nidiye mumewe, mke akajibu ndiyo.

Ndipo mkuu wa kituo alipomuita, mume alipokuja kichapo kikaanza hadi mume akavunjika mkono. Uonevu gani huu jamani. Polisi wetu wa ajabu sana. Yaani mkuu wa kituo anamchukulia mke jamaa, lkini kaon ahitoshi hadi amvunje mkono mtu anayemuibia mkewe. Noma sana jamani hawa polisi wetu, tena mtu mkubwa kufanya kituko kama hiki.
 
Unao uthibitisho wa hii habari? Msaidie huyo mwanaume kufuata sheria...........bado kuwa watu waadilifu walio namoyo wa huruma kwa wanyonge
 
Nchi hii ina sheria ni lazima zifuatiliwe, kwahiyo afungue tu mashtaka ya kupigwa na afande huyo.
 
Pole Ndyoko ndo ukubwa.
Wanamme tumeumbwa mateso - TX Moshi Wiliam

heri mateso ya kuhangaikia maisha mazuri ya familia yako kuliko hayo ya kupata kilema kwa starehe ya mwingine
 
Huyo mwanamke umemuokota? mpaka amefikia kudai talaka wewe unamng,ang,ania wa nini?? utakuja kufa sasa. Take your time!
 
jamani hii kitu haijanikuta mie, ni tukio lililomkuta mtu huko kiteto sio mie jamani. Mie mzima wala sina kilema chochote
 
Huyo mwanamke umemuokota? mpaka amefikia kudai talaka wewe unamng,ang,ania wa nini?? utakuja kufa sasa. Take your time!

mkuu hii kadhia haijanikuta mie, ni mtu mwingine plz mie nimemuongelea tu
 
Duuuuuu!....haiwezekani,yaani ni lazima tu nimkate kidevu.
 
Atambambikia kesi kuwa yeye (mkuu wa kituo) ndo aliyepigwa halafu mume atafungwa maisha ili mkuu wa kituo ajisevie vizuri.Si hataki kumuacha kwa hiari?Duh! Andha kanoon!
 
subutuuu huyo mwanaume lae falaaa,yani najua mkuu wa kituo ananichukuliaa mkee wangu siku zotee na kaa kimyaaa,labdaa sio michalii nilie zaliwaaa arachugaaa,hilo vyarangatiii.kwanzaa na walia timing then nikiwa na uwakikaa hata wa pichaa au live,na mzibuaa mbayaa huyo mkuu wa kituo hata kama simuwezii na charangaa marungu,then twende mbele kwa mbelee na mkee na mwachiaa
 
peleka taarifa katika vyombo vya habari ili walitangaze ndipo huyo mkuu wa polisi atapochukuliwa hatua baada ya suala lake kujulikana
 
Back
Top Bottom