Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6, akiniona tu anatapika na chumbani amehama kabisa!

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Wakuu, heshima mbele!

Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6 sasa, akiniona tu anaanza kutapika na chumbani amehama kabisa! Kwasasa analala chumba cha peke yake! Kadri ujauzito unavyokuwa na yeye ndiyo anakuwa mkali zaidi! Akisikia sauti yangu tu basi anapoteza amani! Zamani kabla ya ujauzito aah mambo ni mwake mwake. Nahisi ni hii hali ya ujauzito ndiyo inamsumbua. Ni ujauzito wake wa kwanza!

Ninaomba ushauri wenu ni jinsi gani ya kukabiliana na hali hii? Niwe nafanya nini katika kipindi hiki? Manake anabadirika kama kinyonga! Mood zikimjia anakuwa fresh mara zikitoka hahaha ni balaa!

Nategemea msaada wenu wakuu!
 
Kuwa mvumilivu ana miezi 3 tu ajifungue na kila kitu kitarudi mwake au sio???

Mvumilivu hula mbivu kama kwenye avatar yako hapo
 
Pole sana kwa hali inayokukuta,kama hali itazidi kuwa mbaya suluhisho ni kumpeleka kwa wazazi mpaka atakapojifungua na mambo yatarudi kama zamani,wanawake wengi wamekuwa na tabia tofauti tofauti wakati wa ujauzito na wakati mwingine huwa ni vigumu sana kudhibiti hali hiyo hasa kama mwanaume si mzoefu wa maisha ya ndoa.Huu ni wakati wako wa kutumia akili ya ziada katika kukabiliana na hili.
 
Mrudishe kwao.

Akikukosa kwa siku mbili tatu atakukumbuka na atakuwa na hamu sana na wewe.
 
Mke wa rafiki yangu alikua anataka karanga za kuchemsha na apples daily...
Ilikuwa nafuu achelewe kurudi lakini anavyo hivyo vitu kuliko awahi mikono mitupu...
 
Kuwa mpole na uvumilie kama wengine walivyosema, jitahidi kumfuraisha muda wote kwani akiwa na hasira muda wote na mtoto tumboni anathirika kwa namna fulani kama wasemavyo wanasaikolojia.
 
imenikumbusha mbali sana.. nilishakoseshwa kufanya mtihani darasa la tano kisa ticha mjamzito na kila mara ataka niwe pembeni yake...nikaambiwa eti mimba yake imenipenda.....:smile:
 
Wakuu, heshima mbele!

Mke wangu ni mjamzito wa miezi 6 sasa, akiniona tu anaanza kutapika na chumbani amehama kabisa! Kwasasa analala chumba cha peke yake! Kadri ujauzito unavyokuwa na yeye ndiyo anakuwa mkali zaidi! Akisikia sauti yangu tu basi anapoteza amani! Zamani kabla ya ujauzito aah mambo ni mwake mwake. Nahisi ni hii hali ya ujauzito ndiyo inamsumbua. Ni ujauzito wake wa kwanza!

Ninaomba ushauri wenu ni jinsi gani ya kukabiliana na hali hii? Niwe nafanya nini katika kipindi hiki? Manake anabadirika kama kinyonga! Mood zikimjia anakuwa fresh mara zikitoka hahaha ni balaa!

Nategemea msaada wenu wakuu!

unajua soln acha uzinzi nje ya ndoaunajua anetapika sio yeye mtoto anakasirika na mambo unayofanya nje ya ndoa....mi nimeona kwa mdogo wangu hili na usipoacha atatapika mpaka siku ya mwisho unampeleka kujifungua so usitafute mchawi mchawi wewe mwenyewe awa watoto wanaona maovu ya baba zao ila awatayabeba hiyo ndio baraka waliopewa rudi kwa muumba wako muombe mkeo msamaha utasamehewa
 
wewe nani kakuambia mimba zina formula? hayo ya mdogo wako ni tofauti na haya, na wala ya mdogo wako hayakusababishwa na yeye kutembea nje, ni hali ya mimba tu inavyokuja.
 
imenikumbusha mbali sana.. nilishakoseshwa kufanya mtihani darasa la tano kisa ticha mjamzito na kila mara ataka niwe pembeni yake...nikaambiwa eti mimba yake imenipenda.....:smile:
:bowl::bowl::bowl:duh!
 
unajua soln acha uzinzi nje ya ndoaunajua anetapika sio yeye mtoto anakasirika na mambo unayofanya nje ya ndoa....mi nimeona kwa mdogo wangu hili na usipoacha atatapika mpaka siku ya mwisho unampeleka kujifungua so usitafute mchawi mchawi wewe mwenyewe awa watoto wanaona maovu ya baba zao ila awatayabeba hiyo ndio baraka waliopewa rudi kwa muumba wako muombe mkeo msamaha utasamehewa
Nitakeradhi mkuu. hapa hatuongelei uzinzi! Mimi siyo mzinzi! Sijawahi kwenda huko unapoendaga wewe!!!:nono:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom