Mke wangu kaweka viatu vyake katika gari langu kiti cha mbele!

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Mke wangu naona ana wivu! Hivi karibuni ameweka pair moja ya mchuchumio wake matata sana ndani ya gari langu kwenye kiti cha mbele sehemu ya kuwekea miguu. (Muhimu: yeye pia ana gari lake lakini hajaweka kwake!!!)

Nilipomuuliza mbona unaweka hapa imekuwaje? Akanijibu kwa upole sana...'mume wangu nakupenda sana, na kama unanipenda pia basi naomba hivi viatu vyangu usivitoe hapa'.....

Habari ndiyo hiyo wakuu, nifanyeje? Nivitoe kwa nguvu? Je, anadhani mimi waga nawapa lifti wadada? Je, ni wivu unamsumbua?
 
viatu vitazuiaje wewe kuwapa watu lift?
Wewe viache tu humo kwenye gari..ila watakaopanda watajua kuwa kiti kina mwenyewe ...
 
viatu vitazuiaje wewe kuwapa watu lift?
Wewe viache tu humo kwenye gari..ila watakaopanda watajua kuwa kiti kina mwenyewe ...
hehehehehehe, utata ndiyo hapo! Nikirudi tu yeye huwa wakwanza kunipokea na kuchukua makabrasha katika gari! Nadhani huwa anachungulia kama nimevitoa!
 
kwa nini uvitoe kwa nguvu??
viache kama hicho ndo kinachompa 'relief' kuwa mumewe hata akipakia wanawake wengine watajua ana mwenyewe, ingawa hiyo michuchumio haikuzuii kufanya chochot eutakacho kwenye gari. si unaweza kuitupia huko nyuma na ukikaribia home unarudisha pale mbele??
securities nyingine bana.......tunajidanganya wenyewe na kuridhika!!
ukivitoa kwa kulazimishia unaweza kuzua la kuzua
 
Mke wangu naona ana wivu! Hivi karibuni ameweka pair moja ya mchuchumio wake matata sana ndani ya gari langu kwenye kiti cha mbele sehemu ya kuwekea miguu. (Muhimu: yeye pia ana gari lake lakini hajaweka kwake!!!)

Nilipomuuliza mbona unaweka hapa imekuwaje? Akanijibu kwa upole sana...'mume wangu nakupenda sana, na kama unanipenda pia basi naomba hivi viatu vyangu usivitoe hapa'.....

Habari ndiyo hiyo wakuu, nifanyeje? Nivitoe kwa nguvu? Je, anadhani mimi waga nawapa lifti wadada?
kazi unayo,sasa watu wengine wakipanda hiyo gari wanakaakaa vp si vinawasumbua?mkuu ulimtoa rombo nini mkeo?
 
Jaribu tu kumwambia kwa upole kuwa avirudishe chumbani kwani kama ni tukio viatu haviwezi kuzuia pete inatosha kutoa taarifa kuwa unae mwenzio. Kama ipo ipo tu mkuu
 
Mapenzi yana mambo mengi sana
Kwani wife amekushitukia Pape una vijimambo nje ya mahusiano yenu?
 
Hakuna haja ya kuvitoa lakini muhimu kama unacheza "nje cup" basi wachezaji wanzako wajue kuwa kuna mchezaji mkongwe na machachari hivyo ni viatu vyake na haviruhusiwi kutoka hapo.
Nadhani labda kama umem(wa)ficha itakuletea noma.
 
Mke wangu naona ana wivu! Hivi karibuni ameweka pair moja ya mchuchumio wake matata sana ndani ya gari langu kwenye kiti cha mbele sehemu ya kuwekea miguu. (Muhimu: yeye pia ana gari lake lakini hajaweka kwake!!!)

Nilipomuuliza mbona unaweka hapa imekuwaje? Akanijibu kwa upole sana...'mume wangu nakupenda sana, na kama unanipenda pia basi naomba hivi viatu vyangu usivitoe hapa'.....

Habari ndiyo hiyo wakuu, nifanyeje? Nivitoe kwa nguvu? Je, anadhani mimi waga nawapa lifti wadada?

...Ignore 'them' (viatu)!,
hiyo ni sawa na wale wanaoweka kibao getini eti "MBWA MKALI SANA!"
Otherwise mwambie ndio anawavutia wezi tu sasa!
 
Ulinzi huo Mkuu... Mwanamke atamlinda mume wake.. Hapo yuko kazini.. USIVITOE mpe heshima yake..
 
viatu vitazuiaje wewe kuwapa watu lift?
Wewe viache tu humo kwenye gari..ila watakaopanda watajua kuwa kiti kina mwenyewe ...

WOS, mi namshauri avichunguze vizuri hivyo viatu, anaweza akawa amevifungia ka-camera. ha ha haaaaaa! mapenzi haya bwana!
 
Mi nakushauri hivyo viatu usivitoe wala uasimwambie avitoe. Jifanye kama upo confortable tu vikiwa hapo. siku tu atatamani kuvivaa atavitoa.
Atakapovitoa mkumbushe kuweka pair nyingine; siku atakapoacha kuweka viatu mwambie (kwa upole kama yeye alivyofanya) kuwa hukutegemea kama hakuamini kiasi hicho
 
Hadi afanye uamuzi huo japo ni wa kitoto, utakuwa umempa reason pia.
 
WOS, mi namshauri avichunguze vizuri hivyo viatu, anaweza akawa amevifungia ka-camera. ha ha haaaaaa! mapenzi haya bwana!

Ndugu yangu.... ukiona mtu anafikia hatua ya kuacha animus revetendi kwenye gari ujue ana matatizo maana binadamu huwezi kumchunga...
 
Mkuu you made my Monday!!! Wengine wanaweka kitenge au kanga full time!!! Bottom line, Abiria chunga mzigo wako!!! Ila sasa sijui kama inasaidia sana maana vicheche hata kama utawawekea sijui viatu au khanga/kitenge watakuchukulia tu!! Cha msingi si khanga wala kiatu bali ni upendo na heshima kati yenu itazaa uaminifu!!! Jichunge na kujilinda na maharamia wa ndoa yako.
 
Ndugu yangu.... ukiona mtu anafikia hatua ya kuacha animus revetendi kwenye gari ujue ana matatizo maana binadamu huwezi kumchunga...

Mkuu wa mawaidha hiyo katika hughlight ni lugha gani tena?? Ni kilatini au!!! Kamusi yangu sijapitata!!
 
Ndugu yangu.... ukiona mtu anafikia hatua ya kuacha animus revetendi kwenye gari ujue ana matatizo maana binadamu huwezi kumchunga...

Ni kweli kabisa 100%, binadamu hachungiki! tena hapo anamtafutia mbinu zaidi za kumkwepa. Mwisho siku sasa atasema mtumie gari 1 kama anahisi huko wkeye gari ndo unamaliza mambo yote. Tena yeye ndo atakuwa dereva wako, kukupeleka popote uendapo
 
This is called "marking ones territory", it is a primitive and animalistic instinct aimed at establishing boundaries and hegemony over the various disputed "turfs".

Wild animals use is prevalently.Drug dealers, pimps and prostitutes are very fond of it.

Just goes to show how primitive marriage can get, not that far from wild animals, drug dealers, pimps and prostitutes.

I mean if you don't trust your husband/ wife why marry at all?
 
Hahaha.. nawe muwekee vyako kwenye kibebeo chake umwambie ze sem alivyokuambia wakati anaweka kwenye kibebeo chako ikibidi ongezea na tai kabisa....:D
 
Nilipomuuliza mbona unaweka hapa imekuwaje? Akanijibu kwa upole sana...'mume wangu nakupenda sana, na kama unanipenda pia basi naomba hivi viatu vyangu usivitoe hapa'.....

Je, ni wivu unamsumbua?

Duh! Pole sana.

Jiandae, akiona hii haifanikiwi atakwenda mbali zaidi ya hapo. Ni uamuzi wako kulizuia sasa au kusubiri makubwa zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom